Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Chondechonde Biashara ya mkaa inaleta shida!!!!! Ruhusuni jamani!!!!!!
 
Good Idea. Ila Kuna Maaskari Watakaotumia Same Same Privilege Kuonea,Kuua Raia Wasiokua Na Hatia. Maana Askari Nao Ni Watu Wana Mioyo Wana Wivu Na Wanaweza Kuwa Na Visasi. Ku-Abuse Hiyo Power To Shoot An Alleged Robber At First Sight Is Very Vulnerable
 
Haya ni ya kufikirisha. Hivi yalikuwapo toka zamani au ni wakati huu ambao watu wengi wana hasira na ukata? Wanachi wanalia na kukata tamaa, vitu vyapanda bei wakati pesa haipo. Inawezekana kweli kila mtu alikuwa mpiga dili hata huku uchochoroni? HAPANA.
Ujambazi huu wa kuua walinzi wetu na kuchukua silaha zao si jambo la kuangalia tu hivi hivi laziama INTELIJENSIA ya kipolisi itumike kuzidi ile watumiayo kuzuia mikutano ya wanasiasa wa upinzani. Silaha zinapelekwa wapi ili zikafanye nini??
Inasikitisha polisi wana resources zote za kuwezesha kuwasaka hawa maharamia na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.......
AU pengine ni desparation kuona kuna double standard katika kutoa justice. Kama mtu kapoteza kibarua chake kwa sababu ya ubashiteism wakati bashite yuko anakula bata, WHAT DO YOU EXPECT?
Vyanzo vya uchunguzi havipewi ushirikiano na wananchi kwa sababu wana hasira na uchungu mwingi sana inakuwa vigumu kupeleleza jambo wakati wananchi wana vinyongo njaa na pressure nyingi, pia polisi wengi huwa na Tabia ya kamatakamata hovyo hovyo ili wapate Rushwa kwa kutumia kisingizio cha kusaka wauaji ni mojawapo ya njia mbaya ya kuongeza chuki juu ya polisi na serikali kwa ujumla, magufuli anapaswa atambue wananchi wake hawana raha na mengi moyoni pia wanachukia sana Bashite kukumbatiwa kisha kutengeneza kafara mbalimbali za kuwasahaulisha watanzania juu ya vyeti vyake.
 
Kwa pale pwani kuna kitu ambacho kinaendelea,na wazawa wanakijua,sababu viongozi wamekua wakiuliwa toka may mwaka jana,na leo hii polisi na hakuna aliyekamatwa....kwanin viongozi,kwanini pwani??kuna kitu kilichotendwa na wale viongozi,mtu hawezi amua kuua makatibu kata,wajumbe,madiwani,arisk maisha yake na silaha usiku bila sababu,polisi waohoji hata ndugu za marehemu kujua....lasivyo tutaona mengi mabaya
Mi naona kuna chezo hapa. Yaani ishu ya hapo pwani imeongelewa sana now ni almost a year na hakuna la maana linafanyika .....kunani?
 
Good Idea. Ila Kuna Maaskari Watakaotumia Same Same Privilege Kuonea,Kuua Raia Wasiokua Na Hatia. Maana Askari Nao Ni Watu Wana Mioyo Wana Wivu Na Wanaweza Kuwa Na Visasi. Ku-Abuse Hiyo Power To Shoot An Alleged Robber At First Sight Is Very Vulnerable
mkuu hii ni kawaida kwa Tanzania na hutokea mara nyingi sana hususani huko wilayani mikoani ndiyo maana wananchi wengi huko wanawachukia sana polisi, hata hilo tukio la mauaji ya jana endapo waziri wa mambo ya ndani hatawatahadhalisha mapema wataenda kuwakata kamata hovyo watu kusha kuwabambikia kesi ili wapate Rushwa, blackmail za Bashite zimejaa ndani ya jeshi la polisi na wengi hutumia fursa kama hizi kujinufaisha kwa rushwa.
 
Mi naona kuna chezo hapa. Yaani ishu ya hapo pwani imeongelewa sana now ni almost a year na hakuna la maana linafanyika .....kunani?
polisi wamekuwa wakiwabambikia kesi wananchi matokeo yake wakati wa uchunguzi wa matukio hupata wakati mgumu kuchunguza kwa kuwa wananchi wana vinyongo vya kubambikiwa kesi.
 
hii hali si ya kupuuzwa/kufanyiwa siasa...Serikali iwe sikivu sasa...ijadili hali ya usalama nchini

nionavyo...abiria wameichoka safari ya lori
 
Tanga,Pwani,Lindi na Mtwara haya maeneo ni yakuangaliwa sana,kuna vijana wako misituni wanapata mafunzo ya kijeshi na kigaidi,siku waki graduate mtaisoma namba vizuri.mbaya zaidi mamlaka husika zinafahamu lakini wameamua kukaa kimya.
Ndio maana nakwambia hili.la.pwani ni chezo. Maana haiwezekani kama mamlaka zinajua halafu ziko kimya...huo ni usalama wa aina gani??? Nini kinaandaliwa hapa ambacho hatukijui...Je wanatengenezwa ******** ndio maana hakuna hatua....Mbona wale wasomali kipindi kile walivyoua polisi waliisoma namba dakika tu kutoka kwa jwtz?? Imekuwaje hapo pwani katikati ya nchi watu wanafanya mauji tangu mwaka jana wanaua viongozi but watu wako kimyaaaaa as if kuna sio roho za watu zile.
 
Wewe mbona akili yako finyu sasa swala la 'uislam' na kuwahusisha viongozi wa kiislam limekujaje? Kwa hiyo una-assume watu waliouwa askari ni waislamu? Sasa ikitokea wakawa wakristo utasemaje? Kwa hiyo kwa statics zako unafikiri sehemu lilikotokea tukio ni sehemu wanaishi waislamu watupu. Kwani ujambazi au ugaidi unaweza kufanywa tu na watu wa sehemu lilipotokea tukio? Haiwezekani watu wakatoka sehemu nyingine? Wewe na Paskali wote mnashindwa hata kuongelea pia vipi wale raia waliokutwa wamekufa Pwani, mpaka leo hatujui walikufaje na wala miili yao imezikwa bila kufanyiwa uchunguzi.
ni kweli mkuu wauaji hawana uhusiano na imani ya Dini yeyote wao kazi yao ni kutekeleza kafara za Bashite tu, na bashite alijua akiwatoa kafara polisi atamkomoa waziri Mwigulu nchemba atumbuliwe jipu baada ya kumuunga mkono Nape, hizi simema za Daud Bashite bado zipo nyingi endeleeni kusubiria tu.
 
Wakiua raia ni sawa tunasema walikua kwenye operation maalum, lakini wao wakionjeshwa umauti ni ugaidi....

Auwae kwa panga atakufa kwa upanga
Na siku za karibuni wameua sana Raia kisha kusingizia ni majambazi na kwa kuwa magufuli anawapenda sana hana mda wa kuhoji chochote kile, kipindi cha JK licha ya mapungufu yake alipiga marufuku polisi kuua ua majambazi alitaka wakamatwe pia kuwabambikia watu kesi ilipungua sana, lakini kipindi cha magufuli Tabia za Uonevu wa polisi kwa wananchi imerejea kwa kasi kubwa wengi wanabambikiwa kesi, wanauawa hovyo kama wale wafanya biashara wa mahenge na kuchukuliwa pesa zao, hii ni mojawapo ya kilichojenga chuki kwa wananchi.
 
Polisi ni muhimu wakawa rafiki wa raia katika kutoa taarifa za uhalifu unapofanyika.
Polisi wamekuwa wakiwabambikia kesi ndiyo maana wananchi hawataki kutoa ushirikiano kabsa, hata hivyo leo hii wananchi wengi wamekimbia eneo la Tukio wakihofia zoa zoa kumbakumba ya kuwabambikia kesi ili watoe Rishwa.
 
Yule kijana aliemtolea Nape pistol, hii sasa ndiyo kazi yake....
Aende akachunguzeee then awamaluze wale mahili kwa pistol yake!
 
Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefu Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!

RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali
Update 1.

Thanks very objective.

Paskali
Update 2 ya michango very objective

Thanks kwa mchango huu, very objective
Paskali
Update 3.
Huu ni mchango very objective

Thanks for this.
Paskali
Pasco mayala ww unaishi kijichi na huko kuna kota za polisi ni vyema uwambie kuwa Raia wanachukuzwa na Tabia mbaya iliyoreshwa kwa kasi, hawapendi kubambikiwa kesi, kuonewa, kunyanyaswa, kuporwa pesa zao kwa njia haramu za Rushwa, mwambie rafiki yako Bashite amwambie Baba jesca apige marufuku Tabia mbovu ya kuwabambikia watu kesi feki.
 
Midomo ya kisiasa imewafanya wananchi wawaone polisi kama maadui badala ya msaada kwao. Hakuna mtu atakayefurahia kuona mlinzi wake akifikwa na baya kiasi asitoe ushirikiano. Nionavyo mimi, mtazamo ndio wa kwanza kubadilishwa. Tusiimarishe Vikosi vya Kupiga Watu, tuimarishe uhusiano kati yetu
 
Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.

Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,

Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.

Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.

Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefu Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.

Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.

Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!
Kwanza tusipuuze wananchi wakilalamika kuhusu usalama wao pili ifanyike operation kali huko yaliko tokea mauwaji Naamini serikali ina mkono mrefu Tatu naona nguvu nyingi inatumika kuwashughulika upinzani tena kwa upande mwingine unawapa kiki wapinzani
RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali
Update 1.

Thanks very objective.

Paskali
Update 2 ya michango very objective

Thanks kwa mchango huu, very objective
Paskali
Update 3.
Huu ni mchango very objective

Thanks for this.
Paskali
 
Hadi pale Waislam watakapoacha kutetea magaidi, kuyasifu na kuyapa hifadhi. Hadi pale waislam watakapoanza kukemea ugaidi kwenye mihadhara na kila sehemu. Hadi pale waislam watakapoanzisha kampeni ya kuwakana magaidi kutoka katika miongoni mwao. Hadi pale magaidi watakapokoma kuwa sehemu ya waislam. Hadi pale Magnidi watakapokomeshwa kujibainisha kwamba wanafanya ugaidi kwa jina la allah.

Kinyume cha pale sahau!

We una kichaa cha udini, ,,kwaiyo hao walioua police,,,wameua kwa misingi ya kidini unamaanisha au
 
Mkuu Panzi Mchanga, kwanza asante kuchangia uzi huu. Pili asante kunifuatilia tangu enzi za Kiti Moto.

Huu uzi ni uzi wa swali, hivyo solutions inatokana na michango ya wachangiaji.

Hiyo link umeifungua na kuisoma uone nilisema nini lini na leo kimetokea nini? .

Hii thread ni ya kichonganishi kumchonganisha nani na nani? .

Paskali

Hajielewi Huyo,,,mpuuze
 
Back
Top Bottom