Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?

Ooh kumbe utaratibu wa Kukamata unafahamika?
 
Je kuna anayefahamu sababu ya dogo kukamatwa?
 
Naungana na Malisa GJ kwamba MULIRO J4 ameingizwa chaka kwenye taarifa au hakuelewa vizuri maelezo ya Malisa .

Maelezo ya Malisa yapo CLear ,hakuna sehemu yeyote alipolaumu jeshi la polisi kuhusika ila Muliro anasema watamkamata Boniface exmayor na Malisa kwa Kupotosha kifo cha "Babu G".

Wakishupaza shingo kuwakamata kina Malisa watajivua nguo kabisa ,inakuwaje Polisi wahifadhi Mwili then ndugu wamtafute kisha waseme hawana taarifa yeyote ina maana vituo havina mawasiliano? Hawana News Bulletin kupeana Update ya kila tukio linalotokea? Kwa ajali ni tukio ambalo lazima Polisi wawe na record ilikuwaje Ndugu wakati wanamtafuta hawakuwaambie siku ile ile au kesho yake kwamba kuna ajali ilitokea waende mochwary kilwa road wakatambue mwili? Taarifa zinasema alikamatwa K/kooo ila Muliro anasema aligongwa "Buguruni - Kimboka".
 
Daah Yan hawa Polisi ni Mbwa kabsa hivi kweli unaenda kumkamata kijana Innocent hivi na kudhulum uhai wake na wakati kuna jitu linasema litapoteza watu juzi tu na liko uraiani
 
Nina wasiwasi huyu kijana alikuwa Sio Raia mwema
Ni Kwa nini Mnalazimishia POLISI Ndio waliomuua? POLISI imekataa wanafamilia wanalazimishia kuuwawa na POLISI
Kuna nini hapa? Kwani Tanzania kuna vijana wangapi walikufa Tarahe hii? Mbona wao hamna shida Huyu vipi?
There is something wrong
 
Kuna watu wa ovyo Sana hapa duniani,Mungu uwalipe kwa matendo yao.
Bila hata kauli hii Karma italipa kwa kila wanachokifanya si unaona yule mwingine kila siku anashinda kwa Wachungaji na masheihk wamuombee ila hakuna kitu anapata kila mwezi anafata viongozi wa Dini anataka kutubia kimya kimya bila kusema alifanya nini...
 
Mama Samia na yeye kaanza kunariki haka ka mchezo ka kutekana, kuumizana na kupotezana kalikoasisiwaga na marehemu.

Kama yeye si sehemu ya huu uchafu basi haraka sana aruhusu uchunguzi HURU ufanyike vinginevyo na yeye anaanza kujipakaza damu za watu.
 
Jitahidi uwe unasoma habar kwa kina kabla ya kukurupuka kuandika utajidhalilisha bure
 
Point
 
Naomba kujua yule kada wa bukoba alisema tutawapoteza na polisi msimtafute na yeye kashaenda kuhojiwa au uchunguzi unaendelea maana bado watu wanapotea anajua wanakoenda na waliko wengine ambao wanatafutwa ... Polisi mngeenza na huyo mngejua mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…