Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
lakini Mungu anajua kila kilichotokea, tumwachie Mungu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
imagine, wanakamata hawa waliotoa taarifa ila kada wa ccm aliyetoa kauli ya kichochezi, hakufanywa kitu. hivi ingekuwaje kauli kama ile ingetolewa na chadema au act.Naomba kujua yule kada wa bukoba alisema tutawapoteza na polisi msimtafute na yeye kashaenda kuhojiwa au uchunguzi unaendelea maana bado watu wanapotea anajua wanakoenda na waliko wengine ambao wanatafutwa ... Polisi mngeenza na huyo mngejua mengi
Hakuna namna polisi wanaweza kujinasua kwenye kesi hii ya mauaji. Watu walioshuhudia akitekwa, wanasema alitekwa na watu waliojitambulisha kama polisi. Na wakati ndugu wanamtafuta bila mafanikio, kumbe amefichwa na polisi kwenye mochwari ya polisi. Wanaponaje hapa?Tarehe 13 April, Meya Mastaafu wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob alitoa taarifa ya kupotelewa na ndugu yake Bw. Robert Mushi maarufu kama Babu G, ambaye alipotea mapema mwezi April 2024. Inadaiwa alikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa Polisi maeneo ya Kariakoo na baada ya hapo hakuonekana tena.
Ndugu walimtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio. Taarifa ilitolewa Polisi lakini walikanusha kumshikilia. Polisi walisema Robert hakuwa kwenye orodha ya wahalifu wanaotafutwa na Polisi. Na hata angekua mhalifu wangemkamata kwa utaratibu rasmi na kumpeleka mahakamani, sio kumvizia mtaani.
Baada ya hapo Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar likatoa taarifa ya kupotea kwa Robert na kwamba anatafutwa na ndugu zake. Hata hivyo ndugu walipofuatilia waliambiwa Jeshi la Polisi halijapata taarifa wala fununu zozote za alipo kijana wao, hivyo waendeele kuwa wavumilivu, wakati juhudi za kumtafuta zikiendelea.
Ndugu wamehangaika kumtafuta hospitali zote kubwa za jijini Dar, wakihisi huenda alipata ajali na akaumia kiasi cha kushindwa kujieleza hivyo akalazwa kama "unknown patient". Lakini jitihada hizo hazikuleta matokeo.
Leo wakaambiwa "nendeni hospitali ya Polisi Kilwa Road, ndugu yenu amefichwa mochwari pale". Wakaenda. Lahaula! Wakamkuta Robert akiwa kwenye jokofu la baridi. Hakuwa Robert tena bali ni mwili wake ukiwa na majeraha ya kipigo. Ni mauaji ya kikatili. Maskini Robert, hajawahi kuwa na ugomvi na mtu, kwanini atendewe haya?
Ndugu walipouliza wakaambiwa maiti ilipelekwa tarehe 10 April 2024. So ina siku 12 hapo Mochwari. Hii inamaanisha wakati Polisi wakidai kumtafuta Robert, alikua tayari Mochwari 😭.
Watumishi wa Mochwari wanasema maiti ililetwa na Askari. Walipoulizwa majina ya Askari na wanatoka kituo gani, wamewataka ndugu wa marehemu kuuliza uongozi wa hospitali. Viongozi wa hospitali walipoulizwa wakataka ndugu kuwasiliana na Msemaji wa jeshi la Polisi, kwani wao sio wasemaji.
Ni tukio la kinyama linalopaswa kulaaniwa na watu wote. R.I.P Babu G. Gone too soon. Damu yako iwe juu ya wote waliohusika.
View attachment 2971830
Pia soma:
- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi
- Utata sakata la ndugu wa Boniface Jacob: Kupotea mpaka kukutwa mochwari ya polisi, Amana wapigilia msumari!
Polisi wa nchi hii wana mambo ya kiquma sana.Kuna sababu ya kuangalia upya sheria zetu, hawa polisi ni kama vile wamepewa mamlaka ya kuua raia kwa kisingizio cha kuitwa majambazi.
Sasa panatakiwa itungwe sheria itakayowataka wakuu wa hospitali zote nchini, iwe za wilaya au mikoa, wawe na mamlaka ya kuwahoji polisi pale wanapopelekewa marehemu kwenye hospitali zao kwa ajili ya kuwahifadhi, polisi wakishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha, wakuu wa hospitali wawe na mamlaka ya kukataa kupokea marehemu hao.
Nawe uwe unaunganisha dots, usiwe kichwa panzi.Nina wasiwasi huyu kijana alikuwa Sio Raia mwema
Ni Kwa nini Mnalazimishia POLISI Ndio waliomuua? POLISI imekataa wanafamilia wanalazimishia kuuwawa na POLISI
Kuna nini hapa? Kwani Tanzania kuna vijana wangapi walikufa Tarahe hii? Mbona wao hamna shida Huyu vipi?
There is something wrong
Kafikaje mochwari ya polisi?Nina wasiwasi huyu kijana alikuwa Sio Raia mwema
Ni Kwa nini Mnalazimishia POLISI Ndio waliomuua? POLISI imekataa wanafamilia wanalazimishia kuuwawa na POLISI
Kuna nini hapa? Kwani Tanzania kuna vijana wangapi walikufa Tarahe hii? Mbona wao hamna shida Huyu vipi?
There is something wrong
Haitasaidia kamwe, ushetani huu wa Jeshi la Polisi una mizizi yake ktk Katiba ya nchi. Kama kweli tunataka kuondokana na majanga Kama haya, ni lazima Kwanza kuondokana na Katiba hii iliyopo hivi Sasa kwani inawapa mamlaka Polisi ya kuua watu kiholela bila ya kuweza kuwajibishwa kisheria.Kuna sababu ya kuangalia upya sheria zetu, hawa polisi ni kama vile wamepewa mamlaka ya kuua raia kwa kisingizio cha kuitwa majambazi.
Sasa panatakiwa itungwe sheria itakayowataka wakuu wa hospitali zote nchini, iwe za wilaya au mikoa, wawe na mamlaka ya kuwahoji polisi pale wanapopelekewa marehemu kwenye hospitali zao kwa ajili ya kuwahifadhi, polisi wakishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha, wakuu wa hospitali wawe na mamlaka ya kukataa kupokea marehemu hao.
Nakumbuka Wale walikuwa Wafanyabiashara wa Madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.Waliuawa kwa makusudi na Mapolisi huko ktk msitu wa Mabwepande chini ya OCD Christopher Bageni ambaye alitoa amri kwa Askari Polisi walio chini yake ya kuwaua hao Wafanyabiashara na Kisha kupora pesa zao. Very sad indeed! Lilikuwa ni tukio baya sana.kuna mwaka fulani wafanyabiashara walitandikwa risasi wakaibiwa fedha zao na madini na kadhalika wa kadha......harafu wakasema warikuwa ni majambazi.....sasa tukio lilitokea mbele ya ofisi ya mcha Mungu.....wakampanga yule mgha Mungu akatoe ushahidi wa uwongo......waapiii damu nziiitooo.....mcha Mungu akawaambia mie namuogopa Mungu........
NIna mashaka sana na wanaomsaidia mama.Nakumbuka Wale walikuwa Wafanyabiashara wa Madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.Waliuawa kwa makusudi na Mapolisi huko ktk msitu wa Mabwepande chini ya OCD Christopher Bageni ambaye alitoa amri kwa Askari Polisi walio chini yake ya kuwaua hao Wafanyabiashara na Kisha kupora pesa zao. Very sad indeed! Lilikuwa ni tukio baya sana.
Wito wangu kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akubali kusaini Hati ya Kifo ya OCD Christopher Bageni ili anyongwe hadi kufa, kwa sababu Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani zote tayari zimethibitisha kwamba mtu huyo anapaswa kunyongwa hadi kufa. Hii itasaidia kutoa fundisho kwa Askari Polisi wenye Nia ovu kama ya huyo Christopher Bageni
sio bukoba ndugu, ni ngara!Naomba kujua yule kada wa bukoba alisema tutawapoteza na polisi msimtafute na yeye kashaenda kuhojiwa au uchunguzi unaendelea maana bado watu wanapotea anajua wanakoenda na waliko wengine ambao wanatafutwa ... Polisi mngeenza na huyo mngejua mengi
Unasemaje???sio bukoba ndugu, ni ngara!
wahaya hawana roho ya kuua kwa ajiri ya mali au madaraka.
wanatapeli tu!
ndio mdau!Unasemaje???
Wahaya Hawaui kwa ajili ya mali au madaraka?? Una uhakika kuhusu hili?
Aliuawa na polisi wakamficha kwenye mochwari yao wakipisha upepo upite na wakati huo wakitafuta namna watakavyotunga uwongo ili kuficha ukweli.Kafikaje mochwari ya polisi?
Kwann polisi wafiche hawajui alipo?
Na kweli JPM alikuwa muuaji mkubwa sana. Ameuda watu maelfu kwa maelfu. Hadi alipokufa, watu aliwaua hawana idadi. Tazama jinsi alivyomkosakosa Tundu Lissu amemuachia vyuma mwili mzima. Ndio maana Mungu aliamua kumchukua na kumuacha Tundu Lissu akiendelea kuishi. Mungu hadhihakiwi.Enzi zile angesingiziwa JPM
Asante Kwa kunifafanulia unajua hasira tenasio bukoba ndugu, ni ngara!
wahaya hawana roho ya kuua kwa ajiri ya mali au madaraka.
wanatapeli tu!