Maulid Kitenge ni tajiri kiasi gani hadi asafiri mataifa mbalimbali kiasi hicho?

Kusafiri ni jambo la kawaida tu.

Si utajiri.

Kuna wakati nilikuwa nafanya kazi na masela New York, ikifika weekend wanaenda Iceland au Jamaica, just for the weekend, wanaruka majoka, Jumatatu wanarudi kazini na stories za Reykjavik na Montego Bay.

Sema nchi ikiwa masikini sana, kuwa na passport tu ni jambo lisilo la kawaida, achilia mbali kusafiri.

Kitenge ana connections za kimataifa, hivyo hakuna cha ajabu.

Mengine yanaweza kuwa siri zake za kibiashara, kwa habari zaidi mtafute mwenyewe.
 
Kama kusafiri kungekuwa ni utajiri basi Madereva na Makondakta wangekuwa wana Ukwasi wa hatari!
acha kuwa na fikra potofu. kusafiri hakumpi mtu utajiri wa fedha na mali bali unampa mtu utajiri wa maarifa(knowledge).

akili ya mtu ambaye anasafiri mara kwa mara katika mataifa mengine ipo sharp. uelewa wake wa masuala mbalimbali ya kimataifa ni mkubwa.

pia exposure yake huwezi kuilinganisha na exposure ya mtu ambaye anaishi eneo moja kwa mda mrefu bila kusafiri.

wamatumbi tuna usemi wetu unasema "the world is a book and those who do not travel read only one page.”
 
Mimi namkubali sana huyu mtangazaji Mana ni mweledi kwenye kazi yake. Kwa ufupi ni fundi Sana.

Wiki hii yupo Finland na huwa kila wakati ni kuruka kwa ndege mataifa mbalimbali.

Sina nia mbaya lengo ni kujua tu basi
Mkuu Kusafiri sana mataifa mbalimbali ni hobby wala sio utajiri,tajiri kama Warren Buffet huwa hana hobby hiyo pamoja na utajiri wake
 
Mimi namkubali sana huyu mtangazaji Mana ni mweledi kwenye kazi yake. Kwa ufupi ni fundi Sana.

Wiki hii yupo Finland na huwa kila wakati ni kuruka kwa ndege mataifa mbalimbali.

Sina nia mbaya lengo ni kujua tu basi
Na inakuhusu nini
 
Kusafiri ni jambo la kawaida tu.

Si utajiri.
Hebu tuwekane sawa hapa!

Kusafiri ni utajiri. Huwezi kusafiri ukiwa kapuku.

Mimi mshahara wangu tu kwa mwezi laki saba. Hayo mamilioni ya kusafiri angani asubuhi na jioni nayatoa wapi?

Ni matajiri tu ndio wanaomudu safari za aina hiyo!

Tofauti na hapo lazima utakuwa muuza ngada au jangili!
 
Hebu tuwekane sawa hapa!

Kusafiri ni utajiri. Huwezi kusafiri ukiwa kapuku.

Mimi mshahara wangu tu kwa mwezi laki saba. Hayo mamilioni ya kusafiri angani asubuhi na jioni nayatoa wapi?

Ni matajiri tu ndio wanaomudu safari za aina hiyo!
Wewe unanitania? Ushawahi kukutana na watalii wa Ukraine Zanzibar?

Watalii wamepigika ova wanakula kwa Mama Ntilie.

Utajiri ni dhana ndefu na pana.

Kuna siku, wakati nafanya kazi mjini kati hapo Dar, nilikuwa namtembelea mteja wangu mmoja jengo la IPS.

Jamaa mmoja Mchaga ana biashara zake nzuri tu.

Sasa nimefika ofisini kwake, kabla ya kukutana naye, nikakuta watu wanapiga stories.

Wanaulizana, wewe ukipata pesa kiasi gani utaridhika ustaafu kazi utulie?

Basi alikuwepo jamaa mmoja tarishi hivi, yeye akasema akipata shilingi milioni 100 ataridhika na kujiona yuko safi na kustaafu (hiyo shilingi milioni 100 ya late nineties)

Jamaa mwingine bosi akawa anashangaa sana, inakuwaje mtu aweze kuridhika na hela ndogo hivyo.

Lakini, kwa mahesabu yao wote inawezekana walikuwa sawa, huyu tarishi gharama za maisha yake Uswahilini sh milioni 100 ingekuwa utajiri, huyu mwingine akifikiria mzunguko wa pesa katika biashara zake, kodi serikalini, kodi ya ofisi, mishahara ya wafanyakzi, etc, anaona sh milioni 100 hela ndogo tu.

Kwa hiyo mara nyingine inategemea na uliposimamia.

Unaweza kumuona mtu tajiri kumbe mwenzako anatembelea madeni akifukuza utajiri.
 
Kwahiyo utajiri ni dhana ya kufikirika zaidi? (subjective?)

Utajiri unaanzia shilingi ngapi?
 
Kusafiri ni jambo la kawaida tu.

Si utajiri.

Kuna wakati nilikuwa nafanya kazi na masela New York, ikifika weekend wanaenda Iceland au Jamaica, just for the weekend, wanaruka majoka, Jumatatu wanarudi kazini na stories za Reykjavik na Montego Bay.

Sema nchi ikiwa masikini sana, kuwa na passport tu ni jambo lisilo la kawaida, achilia mbali kusafiri.

Kitenge ana connections za kimataifa, hivyo hakuna cha ajabu.

Mengine yanaweza kuwa siri zake za kibiashara, kwa habari zaidi mtafute mwenyewe.
Umejibu vizuri sana na ukaeleweka, paragraph ya mwisho haikuwa na ulazima.
 
Back
Top Bottom