Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Wewe unaamini kuwa tajiri uishi kwenye ghorofa ya kupanga ulaya au!?
Umewazidi nini na kuishi kwako mjini zaidi ya fujo na moshi wa magari?
Ajabu ni kwamba hakuna omba omba huko lakini mjini utawakuta tele.
Elimu yako darasa la ngapi? maana unaweza kuwa umesoma nilicho kiandika lkn huwelewi maudhui yake ni nini.

Kwa kukusaidia sija maanisha waje kuishi MJINI au WAJENGE MAGOROFO tumia akili uliyo pewa na Muumba wako kufikiria.

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
 
Fanya utafiti acha upuuzi, unajua Mahakama ya EACJ ilifanya maamuzi gani hadi Serikali ya Tanzania ikacease kufanya hilo unaloamini? Tena chini ya Shujaa that time!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Familia zinaongezeka na n'gombe wanaongezeka. Hifadhi haiongezeki.

Tutailindaje Ngorongoro na Serengeti hata vizazi vijavyo viione?

Watu wamehamishwa hata kabla ya maamuzi ya kesi uliyoitaja. Labda kwasababu sio mkazi wa Ngorongoro haujajua tu.
 
Tatizo lenu mnahujumiana mtafute Kimai na wale jamaa wa Pingos ..Maa ..mtaalam Mande..

Mwalimu Manongi mtamlaumu bure tu ..Kilindi kuna maeneo mengi tu
Nonsense! Most of leaders hayana upeo kabisa ..no community based approach yanakurupuka tu..Yaee yanapata hata exposure kwa nchi za wengine..kwani Zimbabwe wamewezaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa najua Serikali wadau wake wengi wanapita hapa Jamii Forums...
Ushauri..
Serikali ipunguze nusu ya wamasai Ngorongoro.. Pamoja na robotatu ya mifugo..
Ukienda pembeni kama Loliondo au Longido kuna mapori ya kutosha kwa ajili ya mifugo yao..
Cha ziada Serikali ijenge shule na huduma wezeshi huko kabla hawajahamia huko
 
Watu wanahamishwa barabara ikijengwa, watu wanahamishwa pakigundulika ardhi Ina madini yaani nyie ni kina nani msihamishwe ???

The fact kwamba mlikuwepo hapo from 1950's haiwapi legality ya kuendelea kukaa Kama itaonekana mnaweka threat kwa wanyama pori.

As long as eneo hilo lilishatangazwa kuwa protected na sheria sioni sababu ya hao wamasai kung'ang'ania after all hakina walichojenga au wanacholima zaidi ya kufuga ng'ombe wanaonyang'anyana malisho maana wanacholazimisha ni kupata Yale mapori ambapo kwingine wanajua hawataweza kufuga kwa style Ile .

Tuwe na uchungu na taifa letu, ng'ombe wanaongezeka na familia zao zinaongezeka siku Hadi siku, better late than never.

Hii nchi tunaongozwa kwa sheria, mbona wengine wanahamishwa kupisha maslahi mapana ya Taifa?? Kwa nini wao wajione ndio wenye nchi pekee?
Hapo hapo waarabu wanapewa eneo wajenge na waishi.
Kwa nini ni wamasai tu na sio hawa waarabu?
 
Usiandike kishabiki hali ya Ngorongoro inasikitisha,inakatisha tamaa & ina huzunisha.
Ni kweli Waasai wapo ngorongoro miaka mingi wakishi na wanyama pori na mifugo yao.Wakati huo Mamlaka inaanzishwa idadi ya watu ilikuwa 8,271 na idadi ya mifugo ilikuwa 30,000.Nyumba za wamaasai zilikuwa aina ya combi

View attachment 2109828

Leo idadi ya Maasai ni 120,000 huku idadi ya mifugo yao ikifikia zaidi ya 1,000,000 na makaazi yao yakiondoka katika uasilia na kwenda kwenye usasa.Leo hii mabati msouth yamejaa Ngorongoro.Mmaasai anajenga nyumba za kisasa hadi maghorofa yamejengwa ndani ya hifadhi mgeni akitembelea Ngorongoro anakutana na Kondoo,Mbuzi na Ng'ombe kwa wingi kuliko Simba au Nyati.

Lazima Tanzania ichukue hatua kali na madhubuti kuokoa Ngorongoro.Kumezuka NGOs nyingi tena nyingine zikiasisiwa Kenya zipo pale kwaali ya kutetea ujinga na kuona Ngorongoro inakufa.Hii vita asili yake kubwa ni Kenya ambayo inaumizwa sana na uwepo wa Ngorongoro,Serengeti na Kilimanjaro.Kenya kupitia idara yake ya ujasusi inafahamu wazi ushindani wa utalii ni vivutio na wakiangalia hizo Mbuga tatu wanaona bora waiumize walau moja ambayo ni Ngorongoro.

Hizi NGOs nyingi zinawadanganya wamaasai Ngorongoro ni mali yao,serekali haina chao sasa huu ujinga ungemalizwa na vingozi wenye maamuzi mazito ikiwemo kuirejesha Ngorongoro TANAPA na kuifanya HIFADHI kama zilivyo Manyara,Serengeti,Kilimajaro au Mikumi.Wamaasai wahamishwe wote Tanzania bado ina mapori mengi.
Umeongea kwa facts.

Wengine wamebaki kimihemko.
 
Unafahamu sababu za Ngorongoro kuwa mamlaka kamili ya hifadhi inayojitegemea?....Kwani hao wamasai hawakuwa kuhamishwa miaka ya nyuma?..

...hili suala linachanganya sababu kumeibuka wimbi la wasemaji wengi na ngumu kujua ukweli upo wapi...

anyway suala la Ngorongoro kulindwa ni lazima....ila isilindwe kwa gharama ya watu kuteseka,kuumizwa na kufanywa wakimbizi wa ndani....lazima utaratibu uwekwe na ufatwe.
Wanahamishwa sio kufukuzwa.

Wanateseka vipi?
 
Hapo hapo waarabu wanapewa eneo wajenge na waishi.
Kwa nini ni wamasai tu na sio hawa waarabu?
Una uhakika na unachodai?Waarabu wamepewa eneo Ngorongoro au Loliondo?Get your facts right.Unaposema wanajenga na kuishi una maana gani?
 
Hao wamasaai watahamishwa tu ili mradi huu mradi unaenda kulinda mali asili yetu kama taifa.

Hata muende wapi hamtoweza kuizuia serikali kukamilisha miradi yake yenye tija kwa watanzania.

Kama umetumwa na wakenya ambao kimsingi wanapigana kuhakikisha Ngorongoro inapoteza uasili wake ili wao wanaufaike na madhaifu hayo basi kawambie kuwa watanzania wapo macho.
Wanahamishwa wamasai alafu wanapewa waarabu? Hapo umelinda maliasili gani?
 
Wamasai hao waondoke, na ni Lazima...
Linapokuja suala la Maslahi ya Taifa ,Ardhi Mmiliki wake Mkuu ni Rais kupitia Kamishna wa Ardhi Kama Kuna wanaopaswa kulipwa Fidia na iwe hivyo.

Tatizo suala hili ndani yake Kuna wanasiasa wananufaika nalo
Wamasai wanaondoka alafu wanapewa waarabu, Sasa hapo unakua umefanya nini?
 
Ngorongoro ni sehemu ya ajabu sana duniani, licha ya wanyama pori kuishi na binadamu ajabu lingine ni wamasai ambao ni wakazi wa eneo hilo wanaenda shule kusoma na kupata exposure kisha narudi ngorongoro anavaa lubega na kuchunga ngo'mbe. Utakutana na watu wana Bachelor, masters, na Phd ila anachunga ng'ombe na wengi wamesomea sheria na wamesoma vyuo vya nje.
 
Somebode say...AirPods journalist is looking towards being District Commissioner or equivalent in this regime.

FYI my Brother Mshambuliaji, hawa ndugu zetu pale wapo kihalali na walihamishwa toka miaka 1950's kutoka serengeti na nakukumbusha kuna amri ya mahakama ya Africa Mashariki EACJ inaikataza Serikali kuwaondoa na serikali imekuwa ikiheshimu Amri hiyo tangu sept 2018 (under Magu regime).

Kabla hujasema ya wanangorongoro chukua time ujifunze kwanza. Kwanza hushangai wanyamapori wanaweza vipi kuishi na binadamu bila kudhuriana? Hivi kweli hujui kwamba hiyo coexistance iliyopo kati ya wanyamapori na na ng'ombe ipo miaka mingi na ndio kitu mojawapo inayovutia watalii, (pengine huna exposure )na ni aibu kwa kijana wa jamii ya pale kula swala au pundamilia wakati mbuzi wapo..

Anyway ni hivi kama unalipwa pesa kufanya propaganda acha mara moja, japo tunasikia kuna kitengo cha Intel NCCA wanahusika kufanya installment ya malipo..(tutacomfirm baadaye)

Tafuta takwimu ujue kama kweli hii hifadhi ipo hatarini , nanakuhakikishia HAKUNA, na kama ipo inakinzana na hali iliopo.

Nakukumbusha acha mara moja hizi propaganda, Zitakuaharibia.

Pia soma > Hali ya Ngorongoro na wana-habari wanaoshinikiza wamasaai waondolewe hawajui chochote wanatumika vibaya bila kujua
Kaka, linapikuja suala la kitaifa inabidi Sisi Kama vijana tulitetee bila kuangalia maslahi binafsi,
Ungekuja na facts kwamba Hilo eneo tunaloliona kwenye hiyo video sio eneo la hifadhi ningekuelewa, lakini Kama ni eneo la hifadhi na watu wamejenga nyumba za mabati inaonyesha Kua huu ni uvamizi na nadhani ungepaswa kumpongeza kitenge kwa kupaza sauti.
Lakini hili swala hata Mh Rais mama Samia alishaliongelea, sasa unataka kutuambia na mama nae anatumiwa?
Au Una mifugo yako pale ?
 
Nonsense! Most of leaders hayana upeo kabisa ..no community based approach yanakurupuka tu..Yaee yanapata hata exposure kwa nchi za wengine..kwani Zimbabwe wamewezaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha Mkuu kumbe unawajuwa sasa pigania KATIBA MPYAA ....nimefanya kazi sana huo ukanda Maasailand nikiwa AWF.... huko Zimbabwe land use plan tumezipiga sana ....ukiyapandisha ya Zimbabwe na Ngorongoro ni mbingu na ardhi
 
Elimu yako darasa la ngapi? maana unaweza kuwa umesoma nilicho kiandika lkn huwelewi maudhui yake ni nini.

Kwa kukusaidia sija maanisha waje kuishi MJINI au WAJENGE MAGOROFO tumia akili uliyo pewa na Muumba wako kufikiria.

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
Hiyo akili na elimu uliyopewa inakusaidia nini kama lifespan yako ni ndogo kuliko mmasai wa ngorongoro?
Destruction kwako ndio unaona maendeleo, au kunywa maji yaliyochanganywa sukar na rangi na kuitwa soda.
 
Wanahamishwa sio kufukuzwa.
Watahamishwa lini?
Ngorongoro ni sehemu ya ajabu sana duniani, licha ya wanyama pori kuishi na binadamu ajabu lingine ni wamasai ambao ni wakazi wa eneo hilo wanaenda shule kusoma na kupata exposure kisha narudi ngorongoro anavaa lubega na kuchunga ngo'mbe. Utakutana na watu wana Bachelor, masters, na Phd ila anachunga ng'ombe na wengi wamesomea sheria na wamesoma vyuo vya nje.
Ulitaka wabakie mjini?
 
Somebode say...AirPods journalist is looking towards being District Commissioner or equivalent in this regime.

FYI my Brother Mshambuliaji, hawa ndugu zetu pale wapo kihalali na walihamishwa toka miaka 1950's kutoka serengeti na nakukumbusha kuna amri ya mahakama ya Afrika Mashariki EACJ inaikataza Serikali kuwaondoa na serikali imekuwa ikiheshimu Amri hiyo tangu sept 2018 (under Magu regime).

Kabla hujasema ya wanangorongoro chukua time ujifunze kwanza. Kwanza hushangai wanyamapori wanaweza vipi kuishi na binadamu bila kudhuriana? Hivi kweli hujui kwamba hiyo coexistance iliyopo kati ya wanyamapori na na ng'ombe ipo miaka mingi na ndio kitu mojawapo inayovutia watalii, (pengine huna exposure )na ni aibu kwa kijana wa jamii ya pale kula swala au pundamilia wakati mbuzi wapo..

Anyway ni hivi kama unalipwa pesa kufanya propaganda acha mara moja, japo tunasikia kuna kitengo cha Intel NCCA wanahusika kufanya installment ya malipo..(tutacomfirm baadaye)

Tafuta takwimu ujue kama kweli hii hifadhi ipo hatarini , nanakuhakikishia HAKUNA, na kama ipo inakinzana na hali iliopo.

Nakukumbusha acha mara moja hizi propaganda, Zitakuaharibia.

Pia soma > Hali ya Ngorongoro na wana-habari wanaoshinikiza wamasaai waondolewe hawajui chochote wanatumika vibaya bila kujua
Ukweli usemwe,
 
Back
Top Bottom