Basi msiwe mnauliziaulizia sana mishahara jamani kha kwani mnaotoa picha mbaya sana kwamba mnafanya kazi kwa kujilazimisha tu na sio kwa wito kama ulivyosema na hiyo mishahara mnayolipwa ni kiduchu sana haiwezi kuwatosheleza kwa mwezi mzima.
Any way poleni nawaonea huruma jamani mnavyolalamikalalamika kuulizia mishahara.
Nakumbuka nilivyokuwaga muajiriwa mshahara wangu nilikuwa nautumia kukopea benki na kufanya uwekezaji tu nilikuwa sina time na mshahara kwa kweli.
Nawashaurini kopeni kwenye mabenki mfanye biashara muwe mnaingiza kipato kingine.
Naamini kabisa katika mazingira unayoishi huwezi shindwa kubuni biashara yeyote , jaribuni hata biashara ya bodaboda huwezi kosa kijana mwaminifu wa kufanya hiyo kazi.
Na pia jitahidini kuishi maisha ya kujibana ya kujinyima vitu ambavyo sio vya msingi ili kupunguza matumizi yasiyokuwa na ulazima.
Nawashauri msome kitabu kinaitwa the richest man in babylon na uzifanyie kazi theory zake, nyingi ni simple na zipo kiuhalisia kabisa na maisha yetu ya kila siku.
Nyie ndio injini ya Serikali mnapokuwa na malalamiko madogomadogo haya ya kulalamikia mishahara kuchelewa wakati mwisho wa mwezi haujafika mnatia mashaka kwa sisi wananchi wa kawaida kwamba injini ya serikali yetu haipo sawa.
Eeh Mungu Baba Mwenyezi liangalie kundi hili la hawa watumishi wa umma wanaouliziaulizia mishahara kabla ya mwisho wa mwezi na kwa jinsi itakavyoona inafaa waondokane na kero hii .Amina