Maumivu ya kichwa yananimaliza msaada please

Maumivu ya kichwa yananimaliza msaada please

Lets Get Together

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2019
Posts
258
Reaction score
429
Habari wakuu.

Ninapata maumivu makali sana ya kichwa upande wa kushoto (sometimes kushoto na kulia kwa pamoja) kuanzia jichoni hadi kwenye sikio.

Nilipima macho nikapewa miwani lakini hainisaidii bado kichwa kinauma sana hasa nikiangalia vitu vya mwanga mkali kama simu, computer au TV.

Sina tatizo kwenye kuona, naona vizuri kabisa tatizo ni haya maumivu yaani sina raha kabisa.

Naomba msaada wa kimawazo kwenu wataalam hapa jukwaani.

Ahsante.
 
Inawezekana walikupa miwani ambayo haijendana na tatizo lako,yamkini tatizo lilikua kubwa zaidi lakini pia kama uchumi unaruhusu nenda hospital kubwa upime kipimo cha kichwa kizima, nadhani hua inabeba pesa kama kuanzia laki tatu hivi na ukiwa na bima ni msaada mkubwa,unaweza kuta hata siyo macho na una uvimbe ndani,kimbia hospital ndugu,utaleta mrejesho kwa ajili ya wengine pia wenye matatizo kama hayo
 
Je, ni kipanda uso?
Yaani kianuma kuanzia upande wa paji la uso na kwa muda maalum sema kuanzia saa fulani mpaka saa fulani.

Ikiwa ndiyo hivo, nitafute

NB. Ila mimi sio mganga wa kieneyeji.
 
Inawezekana walikupa miwani ambayo haijendana na tatizo lako,yamkini tatizo lilikua kubwa zaidi lakini pia kama uchumi unaruhusu nenda hospital kubwa upime kipimo cha kichwa kizima,nadhani hua inabeba pesa kama kuanzia laki tatu hivi na ukiwa na bima ni msaada mkubwa,unaweza kuta hata siyo macho na una uvimbe ndani,kimbia hospital ndugu,utaleta mrejesho kwa ajili ya wengine pia wenye matatizo kama hayo
Uchumi sio mkubwa so kupima kichwa kizima Itakua mtihani kwangu.

Nisipo angalia vitu vya mwanga mkali nakua normal kabisa. Nina miezi kadhaa sijaumwa Ila juzi nilitumia simu ya mtu Ina mwanga mkalii sana kwa dakika moja tu kichwa kikaanza leo ni siku ya tatu hakijapoa.

Nimetumia dicloper jana usiku kikapoa lakini anzia asubuhi kimeanza tena.
 
matumizi yako ya simu yakoje mkuu? Unatumia simu muda mwingi na huwa unatumia simu hadi usiku sana? Mwanga wa simu huwa unasumbua sana kichwa
 
Je, ni kipanda uso?
Yaani kianuma kuanzia upande wa paji la uso na kwa muda maalum sema kuanzia saa fulani mpaka saa fulani.

Ikiwa ndiyo hivo, nitafute

NB. Ila mimi sio mganga wa kieneyeji.
Hapana mkuu sio kipanda uso. Napata maumivu kuanzia jichoni kuelekea upande wa sikio na ni maeneo hayo tu ndio yanauma.
 
matumizi yako ya simu yakoje mkuu? Unatumia simu muda mwingi na huwa unatumia simu hadi usiku sana? Mwanga wa simu huwa unasumbua sana kichwa
Matumizi yangu ya simu sio makubwa sana sababu natumia simu ya torch muda mrefu kuliko smart phone.
 
Probably umepewa miwani ambayo sio compatible,that's why haifanyi kazi vzr ndo maana vitu vinavyosababisa reaction za pupils kama mwanga zinageuka aggravating factor ya hyo headache.

Nachokushauri tafuta clinic nzuri ya macho,kuna proffesor moja Wa muhimbili amefungua kituo chake tegeta anatibu macho inaitwa kwisa eye clinic nafkr pale utapewa miwani sahihi
 
Habari wakuu.

Ninapata maumivu makali sana ya kichwa upande wa kushoto (sometimes kushoto na kulia kwa pamoja) kuanzia jichoni hadi kwenye sikio.

Nilipima macho nikapewa miwani lakini hainisaidii bado kichwa kinauma sana hasa nikiangalia vitu vya mwanga mkali kama simu, computer au TV...
Inawezekana tatizo lako ni "Primary Headache" aina ya "migraine". Lets Get Together
 
Mkuu Mimi naweza sema ni tatizo la macho,,hata Mimi nimewahi kukumbana na tatizo hio,Mara ya kwanza nilienda Ndanda Hospital,nikapimwa nakugundulika kuwa na tatizo la macho,nilipewaa miwani lakini haikuwa na msaada juu yangu,baadae niliamua kwenda kwa private hospital maana kule wanakuwa makini sana kumsikiliza mteja,nilifanyiwa vipimo kwa umakini sana takribani saa mbili,

Baadae wakabaini kuwa miwani niliyopewa hapo awali haikuwa ikiendana na tatizo langu,baada ya hapo nilibadilishiwa saizi ya miwani na kupelekea kupata nafuu ya ugonjwa wangu,hadi sasa kichwa huniuma kwa nadra sana

Kitu kingine zingatia ulaji wa mboga za majani tatizo litapungua na hata kuisha

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Probably umepewa miwani ambayo sio compatible,that's why haifanyi kazi vzr ndo maana vitu vinavyosababisa reaction za pupils kama mwanga zinageuka aggravating factor ya hyo headache
Nachokushauri tafuta clinic nzuri ya macho,kuna proffesor moja Wa muhimbili amefungua kituo chake tegeta anatibu macho inaitwa kwisa eye clinic nafkr pale utapewa miwani sahihi
Nitajaribu kufika hapo.
Ahsante sana.
 
Mkuu Mimi naweza sema ni tatizo la macho,,hata Mimi nimewahi kukumbana na tatizo hio,Mara ya kwanza nilienda Ndanda Hospital,nikapimwa nakugundulika kuwa na tatizo la macho,nilipewaa miwani lakini haikuwa na msaada juu yangu,baadae niliamua kwenda kwa private hospital maana kule wanakuwa makini sana kumsikiliza mteja,nilifanyiwa vipimo kwa umakini sana takribani saa mbili...
Ahsante sana kwa ushauri.
 
Unaweza kunieleza kidogo mkuu.
Samahani lakini.
Bila samahani mkuu,
angalia maelezo haya hapa chini kuhusu Migraine

MAUMIVU YA KICHWA YA MIGRAINE (MIGRAINE HEADACHE)
-Aina hii ya maumivu ya kichwa ya awali diyo ambayo imeenea sana na watu wengi wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara huwa na tatizo hili migraine. Maumivu haya yanaweza kuwa ya upande mmoja; lakini yanaweza kuwa katika paji la uso pia na kusikika katika eneo lote la paji la uso, na shingo.

Aina hii ya maumivu ya kichwa huwa ni ya “kichwa kugonga” (throbbing pain) na huambatana na dalili kama vile kichefuchefu na/au kutapika, kizunguzungu, macho kushindwa kuona vizuri, macho kuuma yanapoangalia mwanga. Aina hii ya maumivu ya kichwa huzidishwa na kutembea au kujisogeza kwa namna yoyote, na mgonjwa hujisikia nafuu akipumzika/kulala;

kwa kawaida, maumivu haya huwa makali kwa muda wa masaa 1-2, na yanaweza kuchukua kati ya masaa 4 hadi 72.Vitu ambavyo huweza kusababisha mtu mwenye tatizo la migraine kuanza kuumwa kichwa (triggers) ni kama vile vinywaji vyenye kemikali ya caffeine au pombe (alcohol)/sigara, mawazo, uchovu/usingizi,hasira, kwa kinadada kama akiwa anakaribia siku zake, au kwenye siku zake,mwanga mkali/sauti.

Aina hii ya maumivu ya kichwa pia huwasumbua zaidi wanawake ambao wako katika umri wa kuweza kushika mimba ambao ndio wameanza kupata hedhi zao kipindi cha karibuni. Pia, migraine huweza kurithiwa kutoka kwa wazazi kwa sababu mara nyingine husababishwa na vitu ambavyo viko kwenye vinasaba (genetics) za uzao husika.

Pia, aina hii ya maumivu ya kichwa mara nyingi hutanguliwa na ‘dalili za kabla’ (aura), ambazo hutokea kwa kati ya dakika 5-20, na hudumu si zaidi ya dakika 60; dalili hizi za kabla zinaweza kuwa kizunguzungu, kichefuchefu,mwili kukosa nguvu, n.k.

Lets Get Together
 
Natamani nikutafute lakini bei nahisi sitaweza mkuu.
Halafu namba hiyo mbona kama sio ya Tanzania. Utanitibu vipi hapo mkuu? (Nauliza kwa upole na unyenyekevu wa hali ya juu sana)
Usiniogope na wala usiogope bei kwani uzima wako na pesa bora kitu gani? Uzima wako unaweza kuupata Hospitalini? Au kuna Mtu anaweza kukupatia uzima wako? Uzima ni kitu bora kuliko pesa, kwani pesa inatafutwa uzima wako utaweza kuupata wapi?

Jali afya yako kuliko. kuliko pesa. Nitafute kwa address niliyo kupa tupate kuzungumza zaidi na ikiwezekana niweze pia kukupa ushauri mzuri Mkuuu Usiniogope Ukiniogopa haya kaa na maradhi yako.
 
Bila samahani mkuu,
angalia maelezo haya hapa chini kuhusu Migraine

MAUMIVU YA KICHWA YA MIGRAINE (MIGRAINE HEADACHE)
-Aina hii ya maumivu ya kichwa ya awali diyo ambayo imeenea sana na watu wengi wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara huwa na tatizo hili migraine. Maumivu haya yanaweza kuwa ya upande mmoja; lakini yanaweza kuwa katika paji la uso pia na kusikika katika eneo lote la paji la uso, na shingo...

Umenizungumzia mimi kabisa, angalau najijua nina migrane ingawa mwaka jana nilipima macho na pressure ya macho vyote vilikua sawa, ila waliniandikia miwani sikununua, CCBRT hao.
 
Back
Top Bottom