Maumivu ya Korodani/pumbu, kuvimba kwake na ushauri wa matibabu

Maumivu ya Korodani/pumbu, kuvimba kwake na ushauri wa matibabu

b4221d922e780b58ff48bf33b9f74df7.jpg
a3e24ad0980036c5eeb619244932149b.jpg


Kunawakati mwanaume huweza kupata maumivu ya korodani, ambapo inawezekana ikawa ni maumivu kwa korodani moja au zote mbili.

Maumivu hayo yanaweza kutokea endapo korodani zitakuwa zimeumizwa au kupata maambukizi.

Aidha, maambukizi hayo huweza kuwa makali na ya muda mfupi au makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe, lakini pia huweza kuwa ni maumivu ambayo siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayomnyima raha mhusika.

Mbali na hayo, pia maumivu ya korodani huweza kuwa makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam huitwa ‘Fournier’s gangrene’.

Kuna wakati mhusika anaweza kupata maumivu ya korodani mara inapotokea korodani ikajinyonga yenyewe na kusababisha mhusika kupata maumivu makali ya ghafla yanayoelekea hadi tumboni.

Kimsingi maumivu ya korodani huchangiwa na vyanzo mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takribani zaidi ya miezi mitatu.

Vilevile maumivu hayo yanaweza kusababishwa na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits, Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume na husababisha ugumba.

Pia korodani inaweza kuwa na vivimbe kwa ndani, pembeni au juu ya kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi vinaweza kuwa na mishipa ya damu iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo kawaida, hivyo kuchangia mbegu za kiume kujikusanya na kushindwa kutoka na mengine ya kitaalam ambayo pia tutakuja kuyaona.

Mkuu kama tatizo lako ni mfanowa maelezo ya hapo juu basi nenda kamuone daktari kwa matibabu inaweza ikawa ni serious matter
 
Kama hakuma trauma yoyote inaweza ikawa ni infections so muone daktari atafanya na physical exam
 
habar wna JF,nini tatizo la korodani kuuma sana mara tu mtu unapokuwa umemalza kutoka kushikanashiakna(romancing) na mpenzio katika harakati za kutaka ku sex lakni mwsho wa siku hamfikii lengo na hatimaye korodani hupata maumivu makali sana mpaka mtu kushndwa hta kutembea au kakaa kwa raha kwa muda wa dakika kadhaa,je tatzo hli ni kwa wanaume wote au baadhi yetu na je nn hasa huwa sababu ya korodani kuuma?
Kaka ulishapata ahueni? Maana hata mimi hutokea hiyo
 
Wadau, nnaomba kwa walioeleza matatizo haya wanipe ushuhuda ili nipitie njia hizo,

1. Korodan moja ya kulia imeanza kujaa naona imeizidi ile ya kushoto,

2. Kuna kamshipa nakasikia kwa mbali asubuh nikiamka kanavuta upande huohuo wenye ongezeko, kanauma kwa mbaaali

3. Mashine imefeli kusimama na sasa wife namuangalia tu kama picha,

Naomba kufahamu ni nini hiki na wenzangu walioeleza tatzo kama hili je? Walipata matibabu? Na je? Ntaweza kurud katika hali yangu? Maana ndo kwanza nataka nitengeneze familia. Naomba ushauri wenu,

Mungu awabariki sana ndugu zangu....
 
Habari zenu wanajamvi.
Nakuja mbele yenu waungwana naomba ushauri juu ya hili tatizo la pumbu (korodani) kuuma.

Kwa sasa ni zaidi ya mwezi na maumivu yake yamekuwa ni ya kuvuta na si muda wote kuna kipindi hutulia kabisa hata wiki na mara nyingi huwa pumbu ya upande wa kushoto.

Vilevile napenda kujuzwa kama kuna mahusiano yoyote kati ya magonjwa ya zinaa na kuuma pumbu.

Natanguliza shukrani kwa msaada
 
Hayo ni maeneo very sensitive sana usijaribu dawa kwanza kamwone daktari na umwambie historia ya hayo maumivu.Mchezea mwana kulia ulia mwenyewe.
 
nakumbuka Babu aliniambia mbupu ikiuma wewe ni kidume, alinitafutia mzizi Fulani hivi aisee mchungu sana naujua mimi
 
Back
Top Bottom