Pole
1)lakini ujuzi wako haujaondoka bado unao.
2)mikono yako haijakatika,miguu yako ipo,akili yako ipo ,nguvu zako zipo
3)Ofisi ya watu wenye ofisi ndio wana maamuzi kulingana na mikataba,hata mtetea vifaranga vikikua vikubwa hutafuta namna ya kujitegemea vyenyewe bila kutegemea mtetea mama yao.
Wewe umekuwa mkubwa ukipambana kwa nguvu,ujuzi,akili,mikono yako Mungu atakubariki unaweza ukaja kufungua kampuni yako ukaajiri watu.Tumia kipaji na ujuzi wako Mungu aliokupa.Kama uliweza kupata kazi hapo upo uwezekano wa kupata kazi kwingine kama ulivyopata hapo.
4)Kama ofisi ingefilisika au ingekufa au ingeungua moto bado ungebaki kufanya kazi kwenye majivu ya ofisi iliyoungua /au filisika jibu ni hapana,hizo ni changamoto ambazo sio wewe wa kwanza kupitia na sio wa mwisho.Na huo sio mwisho wa maisha.Unaweza kusonga mbele bila hiyo ofisi mana mwanzo uliishi kabla hujapata hiyo ajira si ulikuwa na maisha kabla ya kuajiriwa hapo.