Mauzauza ya online dating: Tuliowahi kudate mitandaoni tusimuliane hapa mambo yalivyokuwa kinyume na tunachodhania baada ya kukutana live

Mauzauza ya online dating: Tuliowahi kudate mitandaoni tusimuliane hapa mambo yalivyokuwa kinyume na tunachodhania baada ya kukutana live

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
Ilikuwa ni mwaka 2014 nipo facebook, nilipost picha yangu kwenye group la "tafuta marafiki na mchumba", kulikuwa na comment nyingi za mabinti, nikachagua mmoja ambae nimevutiwa nae kwa kuangalia profile picha.

Mazungumzo yalianza rasmi kuanzisha urafiki na siku chache zijazo tukawa wachumba wa mitandaoni kilichobaki ni kuonana live.

Siku ikafika ya kuonana, nilichagua sehemu tulivu, kwa muda huo nilikuwa Mbeya, Kuna sehemu inaitwa Garden ipo pale kiwanja cha okoine, ni sehemu iliyowahi kuwa maarufu ila ikaja kupoa, nilifanya order mapema ya chipsi kuku huku namsubiri toto.

Basi binti akafika pale tukaenda kwenye vile vijumba vya nyasi kufanya mazungumzo, kila akifungua mdomo nikaanza kuona kuna ukungu wa njano kwenye meno, dah !! it was a turn off mazee, yani kila akifungua mdomo nikiona rangi najiuliza maswali mengi sana, hivi huyu suala la usafi vp ? hajui kupiga mswaki muda mrefu kuoga je ? huwa anaoga au ni passport ?

Yani kuna kipindi akasema tukiss ilikuwa ni mtihani mzito sana, nilisingizia tumbo limeanza kuniuma itakuwa ni chakula wacha niende chooni, nikarudi nikamwambia tumbo linaima labda kesho tukutane tutaenda hotel nzuri zaidi.

Nikampa elf 10 ya nauli, baada ya hapo nilitumia mikakati yangu ya exit strategy ikawa imeisha hivyo
 
Alinitumia picha yake nusu alikua mrembo wa kuvutia, siku tunakutana ndio nikajua ni kiwete mazeee....
Alikuja na Taxi kisha akateremka anatambaa, na kwakua nilikua uoande natazama entry door, nikaona ananipigia sim yaani nilikata na nikazima kisha nikatoweka eneo lile man...🤣
 
Alinitumia picha yake nusu alikua mrembo wa kuvutia, siku tunakutana ndio nikajua ni kiwete mazeee....
Alikuja na Taxi kisha akateremka anatambaa, na kwakua nilikua uoande natazama entry door, nikaona ananipigia sim yaani nilikata na nikazima kisha nikatoweka eneo lile man...[emoji1787]

[emoji23][emoji23]hii ni kambaa
 
Kwa sababu mimi nina hela za kutosha na pia ni domo zege niliamua kumtokea mchuchu fulani FB huko kupitia page maarufu ya habari basi tuli flow vizuri ila alikuwa so cheap nikimaanisha alinikubalia penzi haraka sana asee nikasema poa alinitumia picha ya mwili wake akifunika sura kwepi shep ipo ila wakuu sura ni mbaya kinoma yaani she is ugly asf hatazamiki kabisa nikasema ya nini kujitesa nika block kabisa na ku report namba yake WhatsApp.

N.B kutokana na utajiri na status yangu siwezi ku date na dem kibungo maana ntakuwa najidhalilisha na haitokuwa mfano mzuri kwa jamii ili hali kuna masikini wana wake na madem wazuri 😀😃
 
Online dating usipokaa sawa lazima upigwe spana za maana. Kama hutaki mauzauza zingatia baadhi ya dondoo hizi zifuatazo

(1) Hakikisha unaona picha au taswira ya uyo unayewasiliana naye na kwa uhakika źaìďi whatsapp ihusike zaidi. ukiona unaongea na mtu hlf yeye hataki umuone au au mara zote anajifichaficha aisee kaa mbali sana. Kama anadai hana whatsapp hakikisha unaona picha zake angavu za SASA tena ziwe zaidi ya moja. Zingatia neno ZA SASA. Utajuaje ni picha za sasa na sio za miaka 10 au 20 iliyopita ilo ni juu yako.

(2) Hakikisha unaona mwili wote wa uyo unayewasiliana nae. kuna wajanja unaweza kuwa unaongea nae kila siku ila yeye anahakikisha unaona baadhi tu ya sehemu mfano uso tu. ukiona hali iyo shtuka na uende kwa tahadhari usijepata sonona uko mbeleni.

3) anatumia namba nyingi na tofauti za simu. Kama anabadilisha mara kwa mara namba za simu au yeye anakuambia yupo tz lakini anatumia namba za nchi nyingine kuwa makini na uyo mtu kabla hajakunyoosha.
 
mm alinidanganya umri, siku nakutana naye nakuta ni katoto below 20, nikamuuliza we mtoto unafanya nn kwenye mitandao ya kijamii, akajbu mm siyo mtoto nimeshamaliza form four, bad thng kalikuwa na umbo dogo ila kako vzuri kichwan, nilikapeleka sehemu nikamwambia muhudumu naomba umuudumie huyo mdogo wangu, kakanuna kakamwambia muhudumu mm sio mdogo wake, baada ya kupata chochote ktu na story kadhaa tukaagana, sikuwai kukubali kuonana nako tena japo kenyewe kalikuwa kanataka sana, nilikuwa tu nakatumia pesa ya vocha. mwishowe kalikata tamaa kakaniambia ungekubali hata nije nikupe mara moja maana unanijali sana kwa vocha.
 
Back
Top Bottom