Mauzo soko ya hisa Dar es Salaam yashuka kutoka bilioni 32 hadi billion 3.3

Naomba mnisaidie tafadhali. Hivi soko la hisa likishuka ndo uchumi unakuwa umeongezeka? Au Ndo anguko kuu?
soko la hisa linasaidia kukuza mitaji ya biashara na makampuni hivyo kuchochea biashara,uwekezaji,mzunguko wa pesa, ajira, kodi kma pato la serikali na faida kibao sasa kw kukujibu tu kma ulivyouliza ieleweke kuwa SOKO LA HISA LIKISHUKA NDIO ANGUKO KUU
 
Hapo bado impact ya kuzuia gafla makontena ya mchanga wa dhahabu.....nadhani DSE baada ya pasaka ndio watakua na mil. 4 tu
 
Naomba mnisaidie tafadhali. Hivi soko la hisa likishuka ndo uchumi unakuwa umeongezeka? Au Ndo anguko kuu?

Mkeo anakwenda sokoni kununua mahitaji anapokuwa na hela au asipokuwa nazo? Soko la hisa ni soko kama lingine linalouza bidhaa; watu kama hawana fedha hawawezi kununua hisa na vivyo hivyo wanaotaka kuuza hisa zao hawawezi kuuza kwani hakuna wanunuzi!! Uchumi unapokua ndio watu wanapata ajira na kuwa na fedha za kwendea sokoni kwahiyo kama soko la hisa linadorola maana yake uchumi unasinzia!!! Hii ni ishara kwa serikali kuangalia sera zake za uchumi kama zinasaidia nchi au kuididimiza!
 
Sasa hayo makampuni ya simu yanaenda kuongeza nguvu au nayo yataishia kupotea hukohuko
 
Nadhani siyo wakati sahihi wa kununua hisa

Kuna factors nyingi za kufikiria kabla ya kununua hisa. Kwa kukumegea kidogo wajuzi hununua hisa pale bei yake inapokuwa chini na huuza inapokuwa juu!!! Kama ni hisa za mwanzo IPO, angalia utendaji na weledi wa Bodi na management ya kampuni husika na hasa historia yake katika kutengeneza faida! Ukijiridhisha kuwa ukiwekeza huko utafaidika go ahead and buy the shares ama sivyo usinunue kwani biashara hii sio kama savings accunts za benk kwani inawezekana pia ukapata hasara!!
 
Hiyo inaitwa hakuna pa kushika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…