Mavazi ya wazazi hospitali

Mavazi ya wazazi hospitali

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Huwa najiuliza hivi kwanini wazazi sie wa kibongo haturuhusiwi kuvaa martenity dress zetu hospitali muda wa kwenda kujifungua na baada ya kujifungua, badala yake tunaambiwa kuvaa khanga.
Baadhi ya picha za watu wengine huko kwingine naona wana mavazi yao mazuri tu, kwanini sisi???
tanzania-maternity-ward.jpg
54753_ibu_ibu_menyusui_bayi_mereka_di_manila_641_452.jpg
preggo-hospital-1024x682.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa infection control labour ward na acute care wanashauriwa kuvaa nguo za hospitali ambazo zinafuliwa na kupigwa pasi na kila asubuhi unapewa safi.

Rehabilitation na wagonjwa wengine kama wazee kuvaa nguo zao safi kunasaidia kujenga familiarisation na nyumbani pia inapunguza gharama za ufuaji kwa hospitali
 
Hapo ndo tatizo lilipo Dada yangu,
we fikiria tu usafi wa chini tu wa Hosp zetu ulivyo pamoja na mashuka ya hosp, je wataweza kufua na kupiga pasi hizo nguo za labour.

Hii ni tanzania, msisahau hilo
 
Kwa infection control labour ward na acute care wanashauriwa kuvaa nguo za hospitali ambazo zinafuliwa na kupigwa pasi na kila asubuhi unapewa safi.
Rehabilitation na wagonjwa wengine kama wazee kuvaa nguo zao safi kunasaidia kujenga familiarisation na nyumbani pia inapunguza gharama za ufuaji kwa hospitali
Hizo kanga zenyewe haziwezi kuleta infection? Kama sababu ndio hiyo
 
Unaweza vaa utakavyo hukatazwi ila tunaendeleza utamaduni wa wazee wetu walioasisi kanga kama vazi la mzazi
 
Hairuhusiwi, ukiingia tu wodini utamsikia nesi "vua nguo zote "
Nao ni wale wale wanafuata ya bibi zetu ila hawana sababu yoyote ya kufanya hivyo

Hebu siku ukienda zaa[emoji2] [emoji2] au ukisindikiza mzazi[emoji106] muulize nesi kwanini tufanye hivyo usipoona anababaika tuu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Haileti maana kama Labour mtapendeza na Mavazi rasmi, na mkirudi nyumbani mnaanza kupambana na hari zenu...!!

Doesn't make sense...!
 
Nao ni wale wale wanafuata ya bibi zetu ila hawana sababu yoyote ya kufanya hivyo

Hebu siku ukienda zaa[emoji2] [emoji2] au ukisindikiza mzazi[emoji106] muulize nesi kwanini tufanye hivyo usipoona anababaika tuu
Sidhani kama wana sababu, mwaka juzi nlivaa kitambaa kichwani baada ya nywele kuwa vululu vululu, nlikua nmeenda wodi ya watoto kunyonyesha nikaambiwa mama vitambaa haviruhusiwi toa kitambaa kichwani, nkabaki nimetoa macho kwamba nikinyonyesha huku nna kitambaa kuna shida gani teh
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom