Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumzia suala hilo Mei 6, 2025 bila kutaja majina ya wawekezaji hao, Mavunde amesema kwamba wameainisha makampuni ambayo yamepewa leseni, kwamba Wizara inawapa siku 30 kueleza sababu za kushindwa kuendeleza maeneo waliyopatiwa tofauti na makubaliano.
Amesema kwamba baada ya muda huo licha ya leseni kuonekana zina majina ya 'watu wakubwa', lakini amesisitiza kuwa hawatasita kuzifuta.
"Leseni zimebeba majina makubwa kweli kweli lakini hizi 95 za kwanza nitazifuta, tumetoa muda wa siku 30 watuletee majibu yao, wapitie hoja zetu. Wamekuwa mabingwa wa kwenda Mahakamani kuishtaki Serikalii lakini katika hili Serikalii haijakosea"amesema Mavunde
Amesema kwamba endapo kampuni saba tu kati ya hizo zingewekeza, mitaji yao ingekuwa tiriloni 15, ambapo amesema uwekezaji huo ungeleta tija kwa Wananchi.
Mavunde amesema kwamba kwenye kampuni hizo kuna kampuni zina leseni tokea mwaka 2011 lakini hazijawai kuingiza hata koleo kwenye maeneo yao ya uchimbaji.