Uchaguzi 2020 Mawakala wa CHADEMA Chato waeleza kuwa hawajaapishwa

Uchaguzi 2020 Mawakala wa CHADEMA Chato waeleza kuwa hawajaapishwa

21 October 2020
Chato, Geita
Tanzania

Mawakala wa Chato, mkoani Geita watoa tamko, hatujaapishwa

Mkoa wa Geita upo Magharibi mwa Tanzania na Chato ndiyo nyumbani kwa mgombea nafasi ya urais 2020 John Pombe Joseph Magufuli ambaye anawania nafasi hiyo kupitia chama cha CCM.

Source: Swahili Villa

Mama kama hawa Mungu awabariki sana.
 
21 October 2020
Chato, Geita
Tanzania

Mawakala wa Chato, mkoani Geita watoa tamko, hatujaapishwa

Mkoa wa Geita upo Magharibi mwa Tanzania na Chato ndiyo nyumbani kwa mgombea nafasi ya urais 2020 John Pombe Joseph Magufuli ambaye anawania nafasi hiyo kupitia chama cha CCM.

Source: Swahili Villa

Hao wasimamizi ni maounguani. Yaani kukata kuapisha ndio wanaona wamepatia?? Yaani hata akili tu za kitoto zinaona kuwa ni mbinu ovu wazi wazi
 
21 October 2020
Chato, Geita
Tanzania

Mawakala wa Chato, mkoani Geita watoa tamko, hatujaapishwa

Mkoa wa Geita upo Magharibi mwa Tanzania na Chato ndiyo nyumbani kwa mgombea nafasi ya urais 2020 John Pombe Joseph Magufuli ambaye anawania nafasi hiyo kupitia chama cha CCM.

Source: Swahili Villa

Mziki ni mwingine leo!! 😅😅😅
 
Mimi ni mwanachama wa ukweli na mchangiaji mzuri wa maarifa na centi, ila ni mpenzi, sio mshabiki.
Umechangia bei gani nikurejeshee kupitia , maana kuhusu hela sina wasiwasi , maana kama wanachama walikuwepo wengi sana na wameondoka akiwemo Slaa na Lijuakali , na wameondoka lakini sisi bado tupo , japo hujui majukumu yetu lakini unatuita washabiki ! yaani hata sifahamu unapigania nini ?
 
21 October 2020

TUNDU LISSU AMVAA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI CHATO "ACHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU"

Chato ni nyumbani kwao mgombea wa urais John Pombe Joseph Magufuli. Na mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato yaani DED ndiyo msimamizi wa uchaguzi Chato pia ni mmojawapo wa wateuliwa wa Rais Magufuli.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia Mwenyekiti wake, Makamu Mwenyekiti , Wajumbe wa Tume na Mkurugenzi ni wateuliwa wa Rais.
 
Maigizo ya Uchaguzi (Mock election)

SHUHUDIA UCHAGUZI WA MFANO ULIORATIBIWA NA KUSIMAMIWA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM

Source : NEC ONLINE TV - Tanzania
 
21 October 2020

TUNDU LISSU AMVAA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI CHATO "ACHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU"

Chato ni nyumbani kwao mgombea wa urais John Pombe Joseph Magufuli. Na mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato yaani DED ndiyo msimamizi wa uchaguzi Chato pia ni mmojawapo wa wateuliwa wa Rais Magufuli.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia Mwenyekiti wake, Makamu Mwenyekiti , Wajumbe wa Tume na Mkurugenzi ni wateuliwa wa Rais.

Jiwe ni Rais wa hovyo haijawahi kutokea Tanzania. Hivyo tulivuta bangi ya wapi mwaka 2015? Mingine 5 tena asahau kabisa.
 
21 October 2020
Jimbo Mbeya mjini
Mbeya,
Tanzania

Mzozo..!! baada ya wagombea udiwani 16 wa CHADEMA walioenguliwa Mbeya Mjini kujitokeza kuapishwa.

Fomu namba 12 mkurugenzi Mbeya hakuipeleka Dodoma na ndiyo maana Tume ya Uchaguzi Makao Makuu haikuweza kutoa uamuzi kwani Mkurugenzi DED (Msimamizi wa Uchaguzi)wa Mbeya alizikalia ofisini wamedai wagombea walioenguliwa.
 
21 Oct 2020
Kinondoni Hananasif
Ndungumbi
Kijitonyama
Dar es Salaam, Tanzania

WAGOMBEA UDIWANI ACT, CHADEMA WALALAMIKIA UTARATIBU WA KUAPISHWA MAWAKALA

Mgombea udiwani kata ya mwananya kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mohamed Gharib pamoja na Mgombea udiwani kata ya Hananasifu kwa tiketi ya Chadema Ray Kimbita wamelalamikia utaratibu unaotumiwa kuapisha mawakala sehemu moja Rehema Mzena mmoja wa wakala akielezea kutoridhishwa na utaratibu wa unaotumika kuapisha mawakala na kuacha nakala za viapo kwa wasimamizi wa uchaguzi Msimamizi msaidizi Jimbo la Kawe Halima Kahema ameelezea zoezi la uapishwaji mawakala pamoja na changamoto zinazojitokeza.
 
Amefanyaje mkuu
Wewe upo dunia ipi?Hujaona hii barau alioandika?
458909807.jpg
 
21 October 2020
IRINGA Mjini URBAN
Tanzania

WAGOMBEA WA CCM & CHADEMA WATOFAUTIANA ZOEZI LA KUAPISHWA MAWAKALA

Mchungaji Peter Msigwa azungumzia ujanja ujanja wa Mkurugenzi kuhamisha maeneo ya kuapisha mawakala pia mawakala wa CCM kupewa upendeleo maalum na msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkurufenzi DED
 
21 October 2020
Bukoba, Kagera
Tanzania

Polisi Watawanya Wafuasi wa Chadema Kwa Mabomu ya Machozi Bukoba-Kagera | Stori Yetu

Jeshi la polisi mkoani Kagera limelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na mgombea ubunge jimbo la Bukoba Mjini, Chief Karumuna baada ya kugomewa kuapishwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Bukoba mjini Mourice Limbe.

Mgombea huyo aligoma kutoka katika eneo la uwanja wa Kaitaba mara baada ya zoezi la kuwaapisha mawakala wa vyama vya siasa kukamilika akitaka wagombea nao waapishwe kauli iliyopingwa na msimamizi wa uchaguzi akisema wao wataapishwa kwa pamoja siku ya kesho.
 
21 October 2020
Shinyanga, Tanzania

MAWAKALA WA VYAMA VYA SIASA WAMETAKIWA KUTOKUWA CHANZO CHA VURUGU

Mawakala wa vyama vya siasa manispaa ya Shinyanga wametakiwa kutokuwa chanzo cha kuvuruga amani, badala yake wao wawe sehemu ya kutunza amani. Hayo ameyasema msimamizi wa uchaguzi Geoffrey Mwangulumbi wakati akiwaapisha mawakala wa vyama vyote wa kusimamia uchaguzi katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija, katika manispaa ya Shinyanga mkoani hapa
 
Back
Top Bottom