Mawakala wenzangu njoeni tuzungumze kuhusu haya makato mapya

Mawakala wenzangu njoeni tuzungumze kuhusu haya makato mapya

Kuhusu wakala kupiga pesa ii hapana ,maana gawio kwa Wakala halijaongezeka na iyo pesa iliyoongezeka ni tozo ya serikali,
Sanasana atakosa wateja maana makato ni makubwa.
Pole acha turudi bank makato kiduchu kabisa na Niko mjini ATM za kumwaga
 
Wakala atapiga sababu wengi wa wateja hawatatuma pesa tena kwenye mitandao yao. Watampelekea wakala akatume
Hili si walishalikatazaga hao wenye mitandao! Maana kila wakala ukimwambia atume yeye direct anagoma anasema hawaruhusiwi!
 
Kuhusu wakala kupiga pesa ii hapana ,maana gawio kwa Wakala halijaongezeka na iyo pesa iliyoongezeka ni tozo ya serikali,
Sanasana atakosa wateja maana makato ni makubwa.
Hata wakala akituma shida iko pale pale tu 😅 atachezea vitasa tu anayeenda kutoa huko
 
Kama ambavyo watu walikimbia makato makubwa Bank, ndio itakavyokuwa kwa Mobile transactions. Nitatumia mtandao kutuma pesa ikiwa lazima sana. Bora nipeleke pesa au mtu aifuate
 
Mawakala wenzangu naona mambo ni mazuri tu tuchapeni kazi maana hata tukilialia haitasaidia chochote
 
Hata wakala akituma shida iko pale pale tu 😅 atachezea vitasa tu anayeenda kutoa huko
Hii sasa kali yani nimejikuta nacheka tu hii counter attack ni ya kibabe mazee

Goli kufungwa na mildfielder sio ajabu wala haisikitishi ila kufungwa hatrick na goli kipa it pains
 
Nawaza kutuma hela kwenye kikoba kila mwezi hayo makato aiseee sasa hivi ni mwendo wa kutuma bank hakuna namna
 
Hiyo ndiyo bajeti ya mchumi gredi one. Namtumia mama yangu kijijini 1 milion unakata 10k, mama anaenda kutoa pesa hiyo hiyo unakata tena 10k. Kwa nini nisitumie benki kutuma?
Benki kuweka ni bure, kutoa M1 haizidi 6000/-
 
Back
Top Bottom