Ndio mana nawambiaga watu waache kukaa tu makazini kwao bila kuendelea kufanya tafiti za namna yakuongeza faida kwa kazi hizo hizo wanazozifanya.
wewe ni wakala unafunga biashara lakini kuna wakala mwenzako mtaa B anawaza kwenda kulipia frem ya 1m aweke biashara hyo hyo ya uwakala uliyoifunga.
kwanini mtu hujiulizi yeye anafanya fanyaje? iweje yeye imlipe wewe isikulipe? watu hawataki jiuliza hayo maswali mwisho hufinalize kwa kusema Flani ana Dawa flani Mchawi,nk
lakini ukweli ni kwamba katika kila biashara unayoifanya kuna njia bado hujazijua zinazoweza kukupa pesa zaidi ya hizo unazozipata.
Usiridhike na unachopata Fungua puzzle Fumbua mafumbo yaliyofungwa unufaike na unachokifanya.
MAWAKALA kwasasa ndio MA BOSS mjini ndio Biashara ambayo anamwambia mke wake Aendeleee kumenya vitunguuuu swaum anaenda kazini atamtumia Nyama na vitu vya kupika.
Ukiona wakala anauza line yake MSIKITIKIE sana muoneee huruma maana kwasasa hakuna biashara inayolipa 100% kama biashara ya Uwakala.
au nasema uongo
kingkongtz