Mawakili wa Dkt. Wilbroad Slaa, Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali wamefungua kesi kuwashitaki AG, IGP, DPP, RCO-Mbeya na OCS wa Central Polisi Mbeya

Mh SSH nakuita mara tatu ,naomba usiendelee kufuja fedha kwenye tume ya haki jinai maana haina maana yeyote!! Vyombo vilivyotajwa kunyanyasa watuhumiwa kwenye report ya haki jinai bado wanaendelea kunyanyasa, Mh SSH ulisema wazi kama upepelezi haujakamilika haia haja ya kumkamata mtu....Na sheria zipo wazi ukimkamata mtu ndani ya 24hr inabidi umpeleke mahakamani,sasa watuhumiwa wamekamata zaidi ya siku 5 bado wapo vituoni.
 
Uzuri msisitizo umeshawekwa na mawakili kwamba....

"Chochote kinachofanyika huko kwenye sello za mateso baada ya masaa24 kupita bila watuhumiwa kupelekwa mahakamani ni ubatili mtupu"

Hii kesi itaisha mapema sana. It is pre matured case.
 
Kesi ya uhaini haina dhamana.

Walidhani Serikali ya Mama imelala na wangefanya wanacho taka bila kukamatwa!!!

Serikali ipo macho na ipo makini sana.
 
Kesi ya uhaini haina dhamana.

Walidhani Serikali ya Mama imelala na wangefanya wanacho taka bila kukamatwa!!!

Serikali ipo macho na ipo makini sana.

Tafsiri ya neno UHAINI (TREASON)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaelewa huyu chawa au ana subiri uteuzi?
 
Mi napenda Aya Kama Aki Sheria zinapindishwa no wakati Sasa wanashelia kuonyesha walisoma nn na wanauwezo wa kumuwajibisha yoyote KWA Sheria walisoma ,ii inatakiwa Kila taaruma isimama kwenye professional take KWA kuitetea isiyumbishe
 
Kufungua kesi haisadii kwenye system ya majaji wa phone call
 
Hawa wameonekana ni tishio sio la nchi bali kwa sisiem,hivyo hii kesi itawasumbua mpaka 2025 huko.
 
Huyu dikteta wa kwanza wa kike nchi imemshinda, hafai
 
Nilishangaa kumuona yule Wakili wa Mtibwa Sugar Mwakilima anayemuwakilisha Mwabukusi akilia mbele ya Camera akimtaka rais aingilie kati ili wateja wake wafikishwe Mahakama.

Kitendo kile kilinifanya nijiulize sana, ni kipi kimemtokea Wakili huyu hata afikie hatua ya kumlilia rais wakati yeye mwenyewe hajatimiza wajibu wake to the fullest, ni kwanini alishindwa kutumia Habeas Corpus ili demand yake hoyo itimizwe na badala yake akaanze michezo ya kitoto ya kuingiza siasa kwenye mambo serious?

Je, wajuvi wa sheria mnaweza kunisaidia katika hili?
 
Sijui sheria nitakujibu kileimani, hivi sheria ikipindishwa kuna sheria gani itakayotumika kupindua,
kama kuna maagizo toka juu, ni nani atakayesimamia sheria huku chini?
 
Haitasaidia kitu hii nchi utawala wa sheria uliishia kwa kikwete
 
Kazi ya kutafasiri neno hilo tuiachie mahakama ndio kazi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…