PreGE2025 Mawakili wa Lissu: Tujitokeze kwa wingi kusikiliza kesi ya Lissu, Mei 19

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Mawakili wanaomuwakilisha Tundu Lissu wakiongozwa na Wakili Jebra Kambore, Dickinson Matata wanazungumza na waandishi wa habari Mei 14, 2025.

Itakumbukwa mteja wao Tundu Lissu anakabiliwa na Kesi mbili uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.

Kesi hizo mbili zinatarajiwa kutajwa Mei 19, 2025 katikati Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

View: https://www.youtube.com/live/H_AQ6151uEQ?si=Y54pHeVeqX1zxznN
Katika Maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na Mahakama, Mahakama ilielekeza Lissu kufikishwa Mahakamani tarehe hiyo ikiwa ni baada ya kesi kusikilizwa kwa njia ya Mtandao jambo ambalo upande wa Lissu walipinga.

Sababu za kuzungumza na wanahabari
Wakili Jebra Kambore Amesema kwamba wamekutana na waandishi wa habari kwa lengo ni kueleza umma uamuzi wa Mahakama.

Amesema kwamba wanategemea uamuzi wa mahakam utatekelezwa bila vikwazo.

Wakili huyo amesema kwamba yapo mambo mbalimbali ambayo wanawahasa wanaotarajiwa kufika mahakamani kuyazingatia.

1, Kuzingatia muda, kufika mapema
2, Kuzingatia mavazi, (mavazi yenye stara)
3, Kuzingatia protocol
4, Utulivu wakati Mahakama inaendelea
5, Kutoa mlio kwenye simu wakati shauri linaendelea
6, Watu wasije na Silaha
7, Kutokuanzisha vurugu ya aina yoyote/ raia na vyombo vya Dola
8, Kutokupiga picha/vedeo wakati Mahakama inaendelea.

Wakili Dickson Matata

Amesema kwamba baada ya uamuzi wa Mahakama Mei 6, 2025, mazingira na Haki mbalimbali ambazo Tundu Lissu alikuwa anazikosa yamebadilika.

Hata hivyo amesema kwamba bado Mawakili wake hajapewa nafasi ya kukaa naye muda wa kutosha kushauriana masuala mbalimbali na kujadiliana.

Amesema kwamba ni kinyume na utaratibu wa kisheria kuwanyima haki Mteja haki ya kufanya mazungumzo na Mawakili wake.

Aidha amesema kuhusu mpango wa kuanza kuweka mgomo wa kula amesema baada ya uamuzi wa Mahakama na mambo mbalimbali kubadilika tofauti na awali, hakuteleza suala hilo.

Wakili Jebra Kambore:

Amesema kwamba wanatarajia kuiandikia barua Mahakama kuona kama kuna uwezekano kesi ya Lissu kuihamishiwa kwenye Mahakama zenye nafasi kubwa hususani 'Law school' kwenye Mahakama ya Uhujumu Uchumi au kuona namna ya kufunga spika na tv kwenye viunga vya Mahakama ili watu watakaofika wapate haki ya futauatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Pia soma: Pre GE2025 - DSM - Wakili Jebra: Hatutegemei visingizio vyovyote Lissu kutoletwa Mahakamani Mei 19, 2025
 
Ila Ccm wanakera sana.. ni suala la muda tu watanzania wataamka
 
watz wameshaamka

hayo maigizo ya kambi ya Mbowe kujitoa CDM wameyashtukia

maigizo ya uchaguzi wa bao la mkono likisindikizwa na policcm yameshtukiwa
 
Safi sana,mashahidi wa Kiccm lazima waaibishwe
 
Mawakili wanaomuwakilisha Tundu Lissu wakiongozwa na Wakili Jebra Kambore, Dickinson Matata wanazungumza na waandishi wa habari Mei 14, 2025.

Itakumbukwa mteja wao Tundu Lissu anakabiliwa na Kesi mbili uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.

Kesi hizo mbili zinatarajiwa kutajwa Mei 19, 2025 katikati Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

View: https://www.youtube.com/live/H_AQ6151uEQ?si=Y54pHeVeqX1zxznN
Katika Maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na Mahakama, Mahakama ilielekeza Lissu kufikishwa Mahakamani tarehe hiyo ikiwa ni baada ya kesi kusikilizwa kwa njia ya Mtandao jambo ambalo upande wa Lissu walipinga.

Sababu za kuzungumza na wanahabari
Wakili Jebra Kambore Amesema kwamba wamekutana na waandishi wa habari kwa lengo ni kueleza umma uamuzi wa Mahakama.

Amesema kwamba wanategemea uamuzi wa mahakam utatekelezwa bila vikwazo.

Wakili huyo amesema kwamba yapo mambo mbalimbali ambayo wanawahasa wanaotarajiwa kufika mahakamani kuyazingatia.

1, Kuzingatia muda, kufika mapema
2, Kuzingatia mavazi, (mavazi yenye stara)
3, Kuzingatia protocol
4, Utulivu wakati Mahakama inaendelea
5, Kutoa mlio kwenye simu wakati shauri linaendelea
6, Watu wasije na Silaha
7, Kutokuanzisha vurugu ya aina yoyote/ raia na vyombo vya Dola
8, Kutokupiga picha/vedeo wakati Mahakama inaendelea.

Wakili Dickson Matata

Amesema kwamba baada ya uamuzi wa Mahakama Mei 6, 2025, mazingira na Haki mbalimbali ambazo Tundu Lissu alikuwa anazikosa yamebadilika.

Hata hivyo amesema kwamba bado Mawakili wake hajapewa nafasi ya kukaa naye muda wa kutosha kushauriana masuala mbalimbali na kujadiliana.

Amesema kwamba ni kinyume na utaratibu wa kisheria kuwanyima haki Mteja haki ya kufanya mazungumzo na Mawakili wake.

Aidha amesema kuhusu mpango wa kuanza kuweka mgomo wa kula amesema baada ya uamuzi wa Mahakama na mambo mbalimbali kubadilika tofauti na awali, hakuteleza suala hilo.

Wakili Jebra Kambore:

Amesema kwamba wanatarajia kuiandikia barua Mahakama kuona kama kuna uwezekano kesi ya Lissu kuihamishiwa kwenye Mahakama zenye nafasi kubwa hususani 'Law school' kwenye Mahakama ya Uhujumu Uchumi au kuona namna ya kufunga spika na tv kwenye viunga vya Mahakama ili watu watakaofika wapate haki ya futauatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Pia soma: Pre GE2025 - DSM - Wakili Jebra: Hatutegemei visingizio vyovyote Lissu kutoletwa Mahakamani Mei 19, 2025

Alipo tupo!
 
Back
Top Bottom