Mawakili wa ‘Mfalme Zumaridi’ waomba ahamishwe Gereza

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
1655489603931.png

Mawakili wa upande wa utetezi katika inayomkabili Mfalme Zumaridi na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kama itawezekana mteja wao awekewe ulinzi au ahamishwe katika Gereza Kuu la Butimba alililopo hivi sasa kufuatia kuwepo kwa taarifa za kuuawa kwake ndani ya gereza.

Ombi hilo la Mawakili wa upande limewasilishwa hii leo Juni 17, 2022, ambapo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Monica Ndyekobora, akawataka Mawakili hao kufikisha malalamiko hayo kwa uongozi wa Gereza Kuu la Butimba kwa ajili ya hatua zaidi huku akiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 30 ya mwezi huu.

Mfalme Zumaridi pamoja na wenzake wanakabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali na imeanza kutolewa ushahidi ambapo leo hii shahidi namba moja ametoa ushahidi mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza.

Chanzo: EaTV
 
Mungu anataka kuuwawa

Ila kawaida...mbona y,su alifanyiwa the same ,[emoji16]
Acha kejeli mkuu!

Yesu ndo wa kumfananisha na zumaridi kweli!? Umetumia kigezo gani kufanya comparison?

Tuombe msamaha wakristo wote!
 
Kesi inaahirishwa ili aendelee kuchakaa.
Chezea kingine sio serikali.
Kama lengo la kuahirisha kesi ni kumkomoa tu, hii sio haki na ni dhambi na wahusika watailipia (karma italipiza)
 
Kawa mweusi tiii na vile ana sura mbaya😂😂😂
 
Mawakili wa upande wa utetezi katika inayomkabili Mfalme Zumaridi na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kama itawezekana mteja wao awekewe ulinzi au ahamishwe katika Gereza Kuu la Butimba alililopo hivi sasa kufuatia kuwepo kwa taarifa za kuuawa kwake ndani ya gereza.

Ombi hilo la Mawakili wa upande limewasilishwa hii leo Juni 17, 2022, ambapo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Monica Ndyekobora, akawataka Mawakili hao kufikisha malalamiko hayo kwa uongozi wa Gereza Kuu la Butimba kwa ajili ya hatua zaidi huku akiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 30 ya mwezi huu.

Mfalme Zumaridi pamoja na wenzake wanakabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali na imeanza kutolewa ushahidi ambapo leo hii shahidi namba moja ametoa ushahidi mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza.

Chanzo: EaTV
Mungu anahofia kuuawa!!
 
Back
Top Bottom