Pre GE2025 Mawakili wa Samia Legal Aid kusimamia kesi za wananchi mahakamani

Pre GE2025 Mawakili wa Samia Legal Aid kusimamia kesi za wananchi mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Wizara ya Katiba na sheria imetuma Mawakili wa serikali takribani 50 ambao kwa siku nane mfululizo watakuwa Mkoani Arusha, kusikiliza na kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa Mkoa huo kupitia kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inayokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Mwanamke duniani inayofanyika Kitaifa mkoani Arusha, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kilele chake Machi 08, 2025.

Moses Matiko, Wakili na mhadhiri msaidizi Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino, Kampasi ya Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa huduma za msaada wa kisheria kwa Mkoa wa Arusha ameeleza kuwa kupitia wizara watahakikisha kuwa wote wenye migogoro wanatatuliwa migogoro yao pamoja na kutoa msaada wa mawakili kwa wananchi ambao tayari walishafungua ama kufunguliwa kesi kwenye mahakama za ngazi mbalimbali.

Matiko amewaambia wanahabari Jijini Arusha kuwa kufanyika kwa kampeni hiyo kote Tanzania ni utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alibaini uwepo wa migogoro mingi ya kijamii na inayoweza kutatuliwa kwenye ngazi ya kijamii, mingi ikihusu mirathi, ndoa, utawala bora, ukatili wa kijinsia, matunzo kwa watoto pamoja na migogoro ya ajira na mahusiano kazini.

Kando ya uwepo wa mawakili wa serikali na wadau wengine wa sheria, Kampeni hiyo pia inahusisha sekta binafsi ambapo kwa Mkoa wa Arusha kuna uwepo wa Mawakili kutoka kwenye Chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Source: Lemutuz
 
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Salum Kalli, amewataka wakazi wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa ya kipekee ya kupata msaada wa kisheria kupitia Mama Samia Legal Aid Campaign inayoendelea jijini Arusha.

Akizungumza alipotembelea mabanda ya huduma za kisheria katika viwanja vya TBA jijini Arusha, Kalli amesema kuwa kampeni hiyo itadumu kuanzia Machi 1 hadi Machi 8, 2025 na ni nafasi muhimu kwa kila mwananchi mwenye changamoto za kisheria kufika na kupata msaada bure.

"Hii ni fursa adhimu kwa kila mwenye changamoto za kisheria. Kuanzia masuala ya mirathi, migogoro ya ardhi, ndoa, na mengineyo. Napenda kuwaalika wananchi wote, hususan wanawake wanaokabiliwa na changamoto hizi, kufika na kupata msaada wa kisheria bila malipo," amesema Kalli.

Aidha, ametoa mfano wa mama mjane ambaye amenyang'anywa mali alizochuma na mume wake baada ya kufariki. Kupitia kampeni hii, mama huyo na wengine wenye changamoto kama hizo wanaweza kupata haki zao kwa msaada wa wataalam wa sheria waliopo kwenye mabanda hayo.

"Hii ni kampeni muhimu inayohakikisha haki inapatikana kwa wote, hususan wale waliokosa sauti ya kutetea haki zao," ameongeza.

Kalli amesifu juhudi za wizara ya Katiba na Sheria kwa kuwaletea wananchi huduma hii bure na kusisitiza kuwa wananchi wa Arusha wanapaswa kuitumia ipasavyo kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla.

Mama Samia Legal Aid Campaign inaendelea jijini Arusha hadi Machi 8, 2025, ikiwa na lengo la kuwasaidia wananchi kupata haki zao bila gharama yoyote

 
Back
Top Bottom