Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 349
- 805
Nianze kwa kusema tu hii nchi ina pesa za mchezo. Maendeleo yanacheleweshwa kwa makusudi lakini fedha zipo.
Ni Jambo lisilopingika kwamba Serikali inatamani sana kuviweka vyama vya kitaaluma mkononi mwake.
Kwa wasiofahamu, Serikali ilituma mawakili wa Jamhuri kwenda kuongeza nguvu kwa mgombea wao ili ashinde urais kwenye uchaguzi wa TLS. Mawakili hawa walikua wakilipwa per diem kabisa.
Pamoja na haya yote, bado mgombea wao ameangukia pua. Wakili Sweetbert Nkuba ameeleza kupinga matokeo ya uchaguzi kwa hoja kuu tatu
1. Karatasi za kura ziliisha katikati ya uchaguzi.
2. Baadhi ya watu wa mtandao X walianza kutangaza mshindi kabla matokeo hayajatangazwa rasmi.
3. Kwa hoja namba mbili, ni wazi kulikua na mawasiliano baina ya mawakala wa uchaguzi na watu wa nje, kitu ambacho ni kinyume cha kanuni za uchaguzi.
Wakili wa Boniface Mwabukusi, Jebra Kambole ameeleza kuwa wapo tayari kumkabili tena Wakili Sweetbert Nkuba Mahakamani.