Mawakili wa utetezi punguzeni muda wa cross examination, kesi ya Mbowe yaweza kuamuliwa kwa haki kabisa hapa ilipofikia

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Baada ya ushahidi wa Luteni Denis Urio kwa upande wa Jamhuri kesi ya Mbowe ambayo imefikisha mashahidi 12 sasa inaweza kuamuliwa na Jaji. Shahidi aliyekuwa muhimu kuliko wote na ambaye anaweza kuitwa nyota au kiungo muhimu wa mchezo ni Urio ambaye amekwisha toa ushahidi wake.

Kwa muelekeo wa mashahidi waliopita mambo mengi yatakuwa ni ya kujirudia rudia tu kutoka upande wa mashahidi wengi waliobaki. Kupunguza urefu wa hii kesi Mawakili wa utetezi wafanye cross examination isiyozidi saa moja kwa baadhi ya mashahidi wa kawaida na wasifanye cross examination kabisa kwa angalau mashahidi sita.

Kwa mpango huu itafanya uwezekano wa kuwepo angalau shahidi mmoja kila siku na na kumaliza upande wa mashahidi wa Jamhuri ndani ya wiki tatu ila upande wa utetezi uanze kuletea mashahidi wake na kuimaliza kesi mapema.
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] Unajidanganya ndugu naona hujafahamu umuhimu wa Cross Examination! Hapo huwa inatumika ili kuutikisa ushahidi uliotolewa, bila kufanya hivyo ni kukubaliana na ushahidi wa michongo uliotolewa! Nakushauri ushauri wako utunze kisha utampatia ndugu yako BASHITE kesi yake inaanza leo!
 
Ni vyema waulize maswali yote. Kwenye kuuliza pia unaweza ukagundua vitu kama ukiukwaji wa taratibu, mashahidi wengine haswa maaskari wanaweza shitakiwa baada ya hii kesi kupitia shahidi zao n.k
 
Baada ya ushahidi wa Luteni Denis Urio kwa upande wa Jamhuri kesi ya Mbowe ambayo imefikisha mashahidi 12 sasa inaweza kuamuliwa na Jaji. Shahidi aliyekuwa muhimu kuliko wote na ambaye anaweza kuitwa nyota au kiungo muhimu wa mchezo ni Urio ambaye amekwisha toa ushahidi wake...
Tunataka ile Kitu Beyond Reasonable Doubt
 
Baada ya ushahidi wa Luteni Denis Urio kwa upande wa Jamhuri kesi ya Mbowe ambayo imefikisha mashahidi 12 sasa inaweza kuamuliwa na Jaji. Shahidi aliyekuwa muhimu kuliko wote na ambaye anaweza kuitwa nyota au kiungo muhimu wa mchezo ni Urio ambaye amekwisha toa ushahidi wake...
Mkuu Yoda heshima kwako kwanza. Cross examination ni muhimu sana linapokuja swala la kumpima na kumtikisa shahidi. So unaposema wapunguze muda na kuachana na cross examination kwa baadhi ya mashahidi maanaake ni kukubalianana na ushahidi alioutoa. Kwa upande wa utetezi hilo haliwezekani kamwe.
 
Ni vyema waulize maswali yote...kwenye kuuliza pia unaweza ukagundua vitu kama ukiukwaji wa taratibu, mashahidi wengine haswa maaskari wanaweza shitakiwa baada ya hii kesi kupitia shahidi zao n.k
Lazimz tuhakikishe Jaji hapati kigugumizi cha kufutilia mbali hii kesi. Kila kitu kiwe wazi. Hii kesi imekuwa darasa.
 
Mkuu Yoda heshima kwako kwanza. Cross examination ni muhimu sana linapokuja swala la kumpima na kumtikisa shahidi. So unaposema wapunguze muda na kuachana na cross examination kwa baadhi ya mashahidi maanaake ni kukubalianana na ushahidi alioutoa. Kwa upande wa utetezi hilo haliwezekani kamwe.
Swadakta. Bila long examination tungejuaje kama Khalfani Bwire na wenzake ndio walikuwa walinzi wa Tundu Lissu? Mpaka kesi inafika hapa hatukuwahi kujua
 
Baada ya ushahidi wa Luteni Denis Urio kwa upande wa Jamhuri kesi ya Mbowe ambayo imefikisha mashahidi 12 sasa inaweza kuamuliwa na Jaji. Shahidi aliyekuwa muhimu kuliko wote na ambaye anaweza kuitwa nyota au kiungo muhimu wa mchezo ni Urio ambaye amekwisha toa ushahidi wake...
Kwa statement yako hii maanake Mbowe na wenzake watatiwa hatiani.
 
Baada ya ushahidi wa Luteni Denis Urio kwa upande wa Jamhuri kesi ya Mbowe ambayo imefikisha mashahidi 12 sasa inaweza kuamuliwa na Jaji. Shahidi aliyekuwa muhimu kuliko wote na ambaye anaweza kuitwa nyota au kiungo muhimu wa mchezo ni Urio ambaye amekwisha toa ushahidi wake...
Walio mdaganya Raisi kwamba Mbowe ana kesi nzito na atafungwa, Raisi akaanza kuongea uko BBC wajitafakali tu au wajiuzuru, kwa ushahidi ulioletwa so far, Jaji anaona tu aibu kusema kwamba hapa hamna kesi ya kujibu na hamna haja upande wa utetezi kuleta mashahidi.

Kama Urio ndo key witness ana ushahidi manaake hata wale wote tigo airtel wali base kwenye huo ushahidi dhaifu wa Urio eti " mda unaisha" huo ndo ushahidi wa ugaidi ufunge mtu, Raisi wa Tz msiwe mna amiini sana wateuzi wenu sasa ona hi aibu ya Taifa, wewe umeuziwa kesi na mwendazake.
 
Ni kweli! Lakini lazima wahoji ili kutoacha shaka yo yote kwenye Utetezi.
 
Baada ya ushahidi wa Luteni Denis Urio kwa upande wa Jamhuri kesi ya Mbowe ambayo imefikisha mashahidi 12 sasa inaweza kuamuliwa na Jaji. Shahidi aliyekuwa muhimu kuliko wote na ambaye anaweza kuitwa nyota au kiungo muhimu wa mchezo ni Urio ambaye amekwisha toa ushahidi wake...
... I have a different opinion; they shouldn't leave any stone unturned.
 
Back
Top Bottom