Copy and paste
Mambo 5 Muhimu Ya Kuyajua Kambla Hujaamua Kumchunia Mpenzi Wako Na Kuacha Kujibu Meseji Zake!
Unakaa wiki nzima hujibu hata meseji ya mpenzi wako, anakutumia meseji unaziona unajifanya uko bize, akipiga simu humpi nafasi unakuambia nitakutafuta kisha unampotezea! Unafanya hivyo halafu unajishaua sijui mke, mpenzi, mume au mchumba wangu! Kama una hii tabia naomba nikukumbushe mambo matano;
(1) Sio wewe peke yako mwenye simu, kuna watu kibao wanasimu, kama hujibu meseji zake uko bize unamuacha mpweke hajui kama ushamuacha au bado upo naye basi jua kuna siku atapata mwingine wakuchart naye na atasahau kuwa kuna mtu kama wewe.
(2) Huna chochote cha maana ulichonacho kaamua tu kukuvumilia; Wakasti mwingine unajiona keki labda kwakua anakutafuta kila siku yeye, ila nikuambie, huna cha maana chochote ulichonacho kuna mabaharia kibao wanavyo na kama ni wewe dada jua kuna wengine wanavyo siku akishtuka na kujitambua akaondoka ndiyo utaaanza kulalamika!
(3) Mawasiliano ni kitu cha muhimu, unapoaha kujibu meseji zake unamchanganya mwenza wako, anashindwa kujua kama bado upo naye, ushamuacha au unamiapngo gani, kama umemuacha muaambie aingie zake chooni alie mpaka basia kitoka amepona, na kama bado unampenda unatest kiberiti basi huo ni utoto, atakuvumilia wakati akitafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi yako.
(4) Kama wewe ulimuona ukamatamani basi jua kuwa kuna wengine watamatamani na usishani kwako kafika, kama alikutongoza ukakubali basi jua kuna wengine nao anaweza kuwatongoza wakakubali, anaweza kuwa anakuvumilia sikwakua una maajabu sana bali kwakua anajiheshimu tu hataki kuhangaika na leo huyu kesho yule.
(5) Mwisho hata kama uko bize namna gani basi mtumie meseji hata kumuambia Baby nimekumiss. Ule wakati unaingia chooni unakata gogo badala ya kufunga macho kusikilizia maisha basi mjibu meseji zako. Hakuna kitu kinaumiza kama kumtumia mtu meseji, unaona kabisa kaisoma halafu hata hajahangaika kuijibu na baadaye anaongea na wewe kawaida kama vile hakuna kilichotokea. Ndugu yangua cha kuringa hivyo hata huna maajabu yoyote ni kuvumiliana tu watu wanavumiliana!