Mawasiliano ndio kigezo kikubwa kinachoonyesha kama kuna mapenzi au ndio yamejifia

Mawasiliano ndio kigezo kikubwa kinachoonyesha kama kuna mapenzi au ndio yamejifia

Unaweza kaa asubuhi hadi usiku bila maongezi marefu na mpenzi wako sawa lakini siku haiishi bila kumcheki ama yeye kukucheki kama ufanyavyo hii haina shida ila sasa kuna wale ni hakutafuti hata siku kadhaa na ukijaribu tu kumcheki ndio unakutana na habari za yupo busy 24/7. Unajua fika hapa hamna upendo.
Nakubaliana na wewe kwa 100%
 
Hiyo ya week mapenzi yanakuwa yameisha au sina shida nae tena.
Hapo wewe ni wazi unapenda ila unakuwa bize ila unatafuta muda kuchat jioni au usiku. Hiyo ni sawa.

Mjadala hapa ni juu ya wale mtu ana mute wiki yote au mwezi eti yupo bize!
 
Mnaweza kuwasiliana mda wote na bado mapenzi ya kweli yakawa hayapo, MAPENZI NI UFALA TUU.
 
Hii point huwa mnaiendekeza sana ila kiuhalisia haisimami sawia kwa 100% katika kila muktadha.
Yeah, inatokea mtu anakuwa busy kiasi cha kuona kushika simu na kuchat ama kuongea anapoteza muda, ila haimaanisha hampendi mpenzi wake.

Mimi kuna siku naweza kaa from saa 2 asubuhi hadi night bila maongezi marefu nae, it's either single txt au nimtafute jioni au usiku, lakini deep down nampenda sana.

INATEGEMEANA.
Muambie Nampenda sana pia,
no mara waa am going through, aah' no mara waa, no mara how busy I am, aaam, no mara how many times anazurura, Lindi ni nyumbani atarudi tu..!!😂😂
 
Kama una mpenzi/mke/mume/ partner lazima uyape mapenzi kipaumbele, angalau mapenzi yachukue nafasi ya 3 kwenye vipaumbele vyako.

Kama mko mbali walau msgs 3 kwa siku. Simu moja au 2.

Kitafiti, binadamu wa sasa hawezi Kukaa masaa 8 bila kushika simu, sasa katika kushika kwake simu hajaona haja ya kumtania mwenza wake, au kumsalimia au kumuagiza (kutegemea na stage ya mahusiano yenu) something must be fishy!

Tena siku hizi kuna reels na memes, siku nzima haujapata cha kumtumia mpenzi, ahhh subutu sio kweli (kwa sauti ya tabu mtindiga)

Love is byuriful thing. 😍
Sisi wengine ni Waumini wa Nofap ndomaana hatuyapi sana mapenzi nafasi ya kwanza wala ya tatu.
 
Kuna siku nimekutana na post moja ambapo mwamba anasema anamtext mrembo halafu hujibu baada ya masaa mawili au matatu. Mwamba akawa anauliza, "Hivi imekaaje?"

Wakati unatafakari juu ya jambo hilo la mwamba, nami nimejikuta natafakari yangu. Kuna mrembo mmoja alikuwa anaitwa Zawadi. Hatukuwahi kuduu lakini tulikuwa very close, yaani kilichobaki ilikuwa ni kuunganisha viungo vyetu vya uzazi tu. Ila katika hili, mimi nilizingua, nilikuwa naleta mambo mengi kama ya kwenye movie, hahaha.

Inaelekea mrembo hakutaka mambo mengi. Mawasiliano yakaanza kupungua taratibu, na mwisho wa siku nilimuona Kariakoo ana mimba. Nikapata majibu kwanini alikuwa sio active katika mawasiliano.

Turudi kwenye mada. Iko hivi: hakuna ubize kwa mtu unayempenda. Hata uko bize kiasi gani, lazima utatafuta muda wa kuwasiliana naye. Ukiona mtu anakwambia yupo bize, basi fahamu yupo bize na mtu wake mwingine, period.

Kwahiyo, wakati mwingine jiongeze mwenyewe. Chap basi acha ujinga. Hata kama yupo bize, akipata muda atakucheki na kukufahamisha kuna moja mbili tatu, na hata kukuomba radhi anaweza ili mradi tu akuweke sawa. Lakini kama mtu hajibu simu kila mara na hata akipokea haonyeshi kujali wala kutoa sababu, ujue una mboa, jiongeze mapema. Hajibu meseji kwa wakati na mara nyingi haonyeshi kujali, jiongeze chap.

Mawasiliano ndio msingi mkubwa wa mapenzi. Anayekupenda atatafuta muda kwa ajili yako, iwe mvua iwe jua. Atahakikisha mnakuwa karibu siku zote.

Kwahiyo usipoteze muda wako kwa mtu ambaye hana muda na wewe. Tambua thamani yako. Kama yeye anasema "wa nini", wenzake wanasema "watakupata lini?"


Ni hayo tu!

Pia soma:Je, mapenzi yanaweza kuishi bila mawasiliano ya kimwili?
Leo nimekuelewa sana kaka yangu
 
hakuna ubize kwa mtu unayempenda. Hata uko bize kiasi gani
Hoja yako imejikita zaidi kwa watu wanoishi mbali, vipi wanaolala na kuamka pamoja?? Namaanisha mke na mume nyumba moja!

Unatakiwa ufahamu mapenzi ni hisia ambazo huja na kupotea! Wamagharibi waliliona hili, wakaja na ndoa za mikataba! Waarabu wakaaamua kuongeza idadi za wanawake huku wakimsingizia Mungu!

Ujumbe: Usilazimishe hisia!
 
Copy and paste


Mambo 5 Muhimu Ya Kuyajua Kambla Hujaamua Kumchunia Mpenzi Wako Na Kuacha Kujibu Meseji Zake!

Unakaa wiki nzima hujibu hata meseji ya mpenzi wako, anakutumia meseji unaziona unajifanya uko bize, akipiga simu humpi nafasi unakuambia nitakutafuta kisha unampotezea! Unafanya hivyo halafu unajishaua sijui mke, mpenzi, mume au mchumba wangu! Kama una hii tabia naomba nikukumbushe mambo matano;

(1) Sio wewe peke yako mwenye simu, kuna watu kibao wanasimu, kama hujibu meseji zake uko bize unamuacha mpweke hajui kama ushamuacha au bado upo naye basi jua kuna siku atapata mwingine wakuchart naye na atasahau kuwa kuna mtu kama wewe.

(2) Huna chochote cha maana ulichonacho kaamua tu kukuvumilia; Wakasti mwingine unajiona keki labda kwakua anakutafuta kila siku yeye, ila nikuambie, huna cha maana chochote ulichonacho kuna mabaharia kibao wanavyo na kama ni wewe dada jua kuna wengine wanavyo siku akishtuka na kujitambua akaondoka ndiyo utaaanza kulalamika!

(3) Mawasiliano ni kitu cha muhimu, unapoaha kujibu meseji zake unamchanganya mwenza wako, anashindwa kujua kama bado upo naye, ushamuacha au unamiapngo gani, kama umemuacha muaambie aingie zake chooni alie mpaka basia kitoka amepona, na kama bado unampenda unatest kiberiti basi huo ni utoto, atakuvumilia wakati akitafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi yako.

(4) Kama wewe ulimuona ukamatamani basi jua kuwa kuna wengine watamatamani na usishani kwako kafika, kama alikutongoza ukakubali basi jua kuna wengine nao anaweza kuwatongoza wakakubali, anaweza kuwa anakuvumilia sikwakua una maajabu sana bali kwakua anajiheshimu tu hataki kuhangaika na leo huyu kesho yule.

(5) Mwisho hata kama uko bize namna gani basi mtumie meseji hata kumuambia Baby nimekumiss. Ule wakati unaingia chooni unakata gogo badala ya kufunga macho kusikilizia maisha basi mjibu meseji zako. Hakuna kitu kinaumiza kama kumtumia mtu meseji, unaona kabisa kaisoma halafu hata hajahangaika kuijibu na baadaye anaongea na wewe kawaida kama vile hakuna kilichotokea. Ndugu yangua cha kuringa hivyo hata huna maajabu yoyote ni kuvumiliana tu watu wanavumiliana!
 
Hoja yako imejikita zaidi kwa watu wanoishi mbali, vipi wanaolala na kuamka pamoja?? Namaanisha mke na mume nyumba moja!

Unatakiwa ufahamu mapenzi ni hisia ambazo huja na kupotea! Wamagharibi waliliona hili, wakaja na ndoa za mikataba! Waarabu wakaaamua kuongeza idadi za wanawake huku wakimsingizia Mungu!

Ujumbe: Usilazimishe hisia!
Mawasiliano ni mawasiliano,,,tunatarajia walio mbali ndio watawasiliana zaidi lkn hata wanaoishi pamoja kama mchana hamuonani si mbaya kuchekiana walau mara moja,,kumjulia hali mwenzio kuonyesha unamjali na huo ndio upendo wenyewe

Hisia zinashuka au kupotea kwasababu ya kuishi kwa mazoea,,mkiwa na tabia ya kuonyeshana upendo basi tambua hisia zitakuwepo siku zote na lau mkiamua kuishi kama kaka na dada basi mtapoteza hisia kabisa

Mapenzi ni kumjali mwenzio na kumuonyesha upendo,ndio maana tunahimizwa sana kupeana zawadi hakika inaongeza sana mapenzi,,kwahiyo ni kwa kiasi gani hisia zinakuwepo itategemeana na jinsi mnavyo ishi

Ngoja nikuelimishe kwanini waislamu au wanaume wameruhusiwa kuwa na wake wengi tena na Allah ingawa wewe humuamini

Kwanza ni kutuliza kiu ya mwanaume ,wote tunajua sisi wanaume kutulia na mke mmoja ni mtihani sana labda uwe una ucha mungu na hofu ya Allah,,kwahiyo tumepewa ruhusa hiyo ili tuchague wanawake wanne ambao tutaridhika nao,kama wataka mweupe kuwa naye,mwembamba kuwa naye,bonge,au mweusi itategemea na utashi ili mradi usizini na uwe katika njia ya Allah

Pili wanawake baadhi yao wanachangamoto sana katika swala zima la kujahamiana,,mwingine akiwa na mimba tu basi ujue unyumba utautafuta kwa tochi,,sasa mazingira kama haya huyu mume lqzima atatafuta pa kupunga oil chafu mwilini na hapo amezini na kumuasi Allah,,,lkn akiwa na wake wengi hatakuwa na hizo changamoto,huyu akiwa hana mood ya kutoa mzigo mke wa pili atakupa mzogo saaafi kabisa

Tatu kuna watu wamejaaliwa nguvu ya matamanio yaani hao ni bakora kwa kwenda mbele haina kulala yaani kila siku lazima apige bakora,,sasa hiyo inakuwa kero au shida kwa mkewe na mateso,,so akiwa na wake wengi wanashare bakora za mume saafi kabisa na hakuna dhiki kati yao

Na nne huenda mke mmoja asiwe na kizazi basi sio ndio umuache laa! Ongeza mke mwingine na mambo yaendelee huku kizazi kinaendelea.

Najua litakuja swali ha! Mbona wanawake wao hawaruhusiwi kuwa na waume wengi,kimaumbile mwanamke anaridhika na mume mmoja,,muhimu muonyeshe mapenzi ya dhati na mridhishe katika unyumba yaan huyo ni wa kwako

Pili mwanamke akiwa na waume wengi je kizazi kitakuwa cha mume gani? Haya mambo Allah amefanya kwa hekima kubwa sana

Tatu kama mke atakuwa na waume wengi,je siku ndio zamo ya Etugrul Bey kulala naye na mke yupo katika ada yake ya mwezi je huyu mume huoni kuwa atakosa haki yake?

Tafakari hayo!

Linaweza kuja swali mbona wanaume wasio waislamu wana mke mmoja na wameridhika,,jibu ni kwamba kuna mengi nyuma ya pazia ambayo yamejificha,hao ndio wanaongoza kwa mahawara huko mitaani
 
Back
Top Bottom