Mawasiliano ndio kigezo kikubwa kinachoonyesha kama kuna mapenzi au ndio yamejifia

Mawasiliano ndio kigezo kikubwa kinachoonyesha kama kuna mapenzi au ndio yamejifia

Kama una mpenzi/mke/mume/ partner lazima uyape mapenzi kipaumbele, angalau mapenzi yachukue nafasi ya 3 kwenye vipaumbele vyako.

Kama mko mbali walau msgs 3 kwa siku. Simu moja au 2.

Kitafiti, binadamu wa sasa hawezi Kukaa masaa 8 bila kushika simu, sasa katika kushika kwake simu hajaona haja ya kumtania mwenza wake, au kumsalimia au kumuagiza (kutegemea na stage ya mahusiano yenu) something must be fishy!

Tena siku hizi kuna reels na memes, siku nzima haujapata cha kumtumia mpenzi, ahhh subutu sio kweli (kwa sauti ya tabu mtindiga)

Love is byuriful thing. 😍
muone sasa mbona ulinicheka
 
Hii point huwa mnaiendekeza sana ila kiuhalisia haisimami sawia kwa 100% katika kila muktadha.
Yeah, inatokea mtu anakuwa busy kiasi cha kuona kushika simu na kuchat ama kuongea anapoteza muda, ila haimaanisha hampendi mpenzi wake.

Mimi kuna siku naweza kaa from saa 2 asubuhi hadi night bila maongezi marefu nae, it's either single txt au nimtafute jioni au usiku, lakini deep down nampenda sana.

INATEGEMEANA.
Chief hiyo kumpenda unajua wewe,,lkn je yeye atajuaje?

Atajua kuwa unampenda kwa kuwasiliana nae na kumpa mda wako period

kitendo cha wewe kumcheki hata kwa sekunde 30 tu kinathamani sana kwake,,tatizo hatuko romantic wengi wetu
 
Kuna siku nimekutana na post moja ambapo mwamba anasema anamtext mrembo halafu hujibu baada ya masaa mawili au matatu. Mwamba akawa anauliza, "Hivi imekaaje?"

Wakati unatafakari juu ya jambo hilo la mwamba, nami nimejikuta natafakari yangu. Kuna mrembo mmoja alikuwa anaitwa Zawadi. Hatukuwahi kuduu lakini tulikuwa very close, yaani kilichobaki ilikuwa ni kuunganisha viungo vyetu vya uzazi tu. Ila katika hili, mimi nilizingua, nilikuwa naleta mambo mengi kama ya kwenye movie, hahaha.

Inaelekea mrembo hakutaka mambo mengi. Mawasiliano yakaanza kupungua taratibu, na mwisho wa siku nilimuona Kariakoo ana mimba. Nikapata majibu kwanini alikuwa sio active katika mawasiliano.

Turudi kwenye mada. Iko hivi: hakuna ubize kwa mtu unayempenda. Hata uko bize kiasi gani, lazima utatafuta muda wa kuwasiliana naye. Ukiona mtu anakwambia yupo bize, basi fahamu yupo bize na mtu wake mwingine, period.

Kwahiyo, wakati mwingine jiongeze mwenyewe. Chap basi acha ujinga. Hata kama yupo bize, akipata muda atakucheki na kukufahamisha kuna moja mbili tatu, na hata kukuomba radhi anaweza ili mradi tu akuweke sawa. Lakini kama mtu hajibu simu kila mara na hata akipokea haonyeshi kujali wala kutoa sababu, ujue una mboa, jiongeze mapema. Hajibu meseji kwa wakati na mara nyingi haonyeshi kujali, jiongeze chap.

Mawasiliano ndio msingi mkubwa wa mapenzi. Anayekupenda atatafuta muda kwa ajili yako, iwe mvua iwe jua. Atahakikisha mnakuwa karibu siku zote.

Kwahiyo usipoteze muda wako kwa mtu ambaye hana muda na wewe. Tambua thamani yako. Kama yeye anasema "wa nini", wenzake wanasema "watakupata lini?"


Ni hayo tu!

Pia soma:Je, mapenzi yanaweza kuishi bila mawasiliano ya kimwili?
Bugal
 
Unaweza kaa asubuhi hadi usiku bila maongezi marefu na mpenzi wako sawa lakini siku haiishi bila kumcheki ama yeye kukucheki kama ufanyavyo hii haina shida ila sasa kuna wale ni hakutafuti hata siku kadhaa na ukijaribu tu kumcheki ndio unakutana na habari za yupo busy 24/7. Unajua fika hapa hamna upendo.
Nimeipenda hii
 
Kama una mpenzi/mke/mume/ partner lazima uyape mapenzi kipaumbele, angalau mapenzi yachukue nafasi ya 3 kwenye vipaumbele vyako.

Kama mko mbali walau msgs 3 kwa siku. Simu moja au 2.

Kitafiti, binadamu wa sasa hawezi Kukaa masaa 8 bila kushika simu, sasa katika kushika kwake simu hajaona haja ya kumtania mwenza wake, au kumsalimia au kumuagiza (kutegemea na stage ya mahusiano yenu) something must be fishy!

Tena siku hizi kuna reels na memes, siku nzima haujapata cha kumtumia mpenzi, ahhh subutu sio kweli (kwa sauti ya tabu mtindiga)

Love is byuriful thing. 😍
Asante sana
 
Kuna watu wako bize 24/7 siungi mkono hoja nashikilia shilingi watu wenye pesa huo muda wa kuongea mda wote anautoa wapi mapenzi yanataka nini manara sio tajiri ila visenti anavyo ila licha ya kuwapeleka wake zake world cup ila alimwagwa tena mpaka akazimia dokta mwaka anayejiita bingwa naye hakupona elezea mambo yote ila ukifika kwenye mapenzi hapo weka nukta tega sikio usikilize hayana mtaalam wala mjanja ruge na ujanja wake wote alilia kwa zamaradi anyway sijui nilikuwa nataka kuzungumzia nini.
Naomba tuelewane hapa,,kuwa na mawasiliano mazuri haimaanishi kwamba hakutakuwa na changamoto laa! Na hatumaanishi kuchat kila mda au kupigiana simu kila mara,,kikubwa kuwe na mawasiliano kati yenu

Kuna mtu wangu nilikuwa nampigia na kumwambia "nimekupigia kukwambia nakupenda" ni simu ya sekunde 10 lkn ina impact kubwa sana kwake
 
Back
Top Bottom