Mawasiliano ndio kigezo kikubwa kinachoonyesha kama kuna mapenzi au ndio yamejifia

Mawasiliano ndio kigezo kikubwa kinachoonyesha kama kuna mapenzi au ndio yamejifia

Eeeeh kumbe,,basi ngoja niunganishe good morning nyingine kwenye good night ya jana, ambayo hata haikujibiwa, pamoja na good morning ya jana.
Mpendwa ikiwezekana unamuonganishia za wiki nzima ,yeye si anajifanya yupo bize
 
Sio kweli uwezi kumpima mpenzi wako kwa kuwasiliana na simu mara kwa mara apana na ninaevidence ya ili.
Chief hapa hatumaanishi kila mda mnawasiliana hapana,lakini average kwa siku walau mara mbili basi,,,sasa kama hamchekiani kabisa basi ujue hilo penzi lipo ICU linapumulia gas
 
Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Nna gozi langu tunachunana miaka 45 sasa.
Mpe mpwa game. Mtoto akililia wembe sharti apewe. We kumpa mechi ya kirafiki mtoto ajionee mema ya wakubwa utapungukiwa kitu gani. We unadhani ataweza ikeshea huyo, watoto kama hawa unawapa mechi ya kibabe ili wawe na adabu pale wanapoona wakubwa zao.

Sasa unavyokimbia nani atamtia adabu ya kisawa sawa kijana wetu?
 
Mpe mpwa game. Mtoto akililia wembe sharti apewe. We kumpa mechi ya kirafiki mtoto ajionee mema ya wakubwa utapungukiwa kitu gani. We unadhani ataweza ikeshea huyo, watoto kama hawa unawapa mechi ya kibabe ili wawe na adabu pale wanapoona wakubwa zao.

Sasa unavyokimbia nani atamtia adabu ya kisawa sawa kijana wetu?
kampe wewe, unangoja nini?

Mimi siyo mama huruma.
 
Mawasiliano na muda wake kwangu ndivyo vilinifanya niamini ananipenda sana.

Kwa mwanaume aliye busy kama yeye kunitafuta kila aamkapo, breakfast, lunch, jioni, atokapo kazini na afikapo nyumbani kila siku bila kukosa ni zaidi ya yote!
Nampenda sana.

So yeah, mawasiliano imara ndiyo mahusiano imara.
hapo kuna mmoja karogwa!..😂
 
Kuna siku nimekutana na post moja ambapo mwamba anasema anamtext mrembo halafu hujibu baada ya masaa mawili au matatu. Mwamba akawa anauliza, "Hivi imekaaje?"

Wakati unatafakari juu ya jambo hilo la mwamba, nami nimejikuta natafakari yangu. Kuna mrembo mmoja alikuwa anaitwa Zawadi. Hatukuwahi kuduu lakini tulikuwa very close, yaani kilichobaki ilikuwa ni kuunganisha viungo vyetu vya uzazi tu. Ila katika hili, mimi nilizingua, nilikuwa naleta mambo mengi kama ya kwenye movie, hahaha.

Inaelekea mrembo hakutaka mambo mengi. Mawasiliano yakaanza kupungua taratibu, na mwisho wa siku nilimuona Kariakoo ana mimba. Nikapata majibu kwanini alikuwa sio active katika mawasiliano.

Turudi kwenye mada. Iko hivi: hakuna ubize kwa mtu unayempenda. Hata uko bize kiasi gani, lazima utatafuta muda wa kuwasiliana naye. Ukiona mtu anakwambia yupo bize, basi fahamu yupo bize na mtu wake mwingine, period.

Kwahiyo, wakati mwingine jiongeze mwenyewe. Chap basi acha ujinga. Hata kama yupo bize, akipata muda atakucheki na kukufahamisha kuna moja mbili tatu, na hata kukuomba radhi anaweza ili mradi tu akuweke sawa. Lakini kama mtu hajibu simu kila mara na hata akipokea haonyeshi kujali wala kutoa sababu, ujue una mboa, jiongeze mapema. Hajibu meseji kwa wakati na mara nyingi haonyeshi kujali, jiongeze chap.

Mawasiliano ndio msingi mkubwa wa mapenzi. Anayekupenda atatafuta muda kwa ajili yako, iwe mvua iwe jua. Atahakikisha mnakuwa karibu siku zote.

Kwahiyo usipoteze muda wako kwa mtu ambaye hana muda na wewe. Tambua thamani yako. Kama yeye anasema "wa nini", wenzake wanasema "watakupata lini?"


Ni hayo tu!

Pia soma:Je, mapenzi yanaweza kuishi bila mawasiliano ya kimwili?
Chai
 
Back
Top Bottom