Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwa mujibu wa John Heche kupitiia account yake ya twitter, Waziri Mkuu analipwa posho ya shilingi 340,000/= kwa siku awapo Bungeni. Posho hiyo inahusisha sitting allowance pamoja na perdiem na bila shaka hata mawaziri wengine nao wanalipwa perdiem. Tukumbuke John Heche alikuwa mbunge.
Wote tunajua perdiem ni posho ya safari kwa mtumishi anaposafiri kikazi na si vinginevyo ili imsaidie kugharamia malazi, chakula na mambo mengine awapo safarini.
Kwakuwa Waziri Mkuu anakaa katika nyumba ya serikali na bila shaka anahudumiwa na serikali karibu kila kitu, uhalali wa Waziri Mkuu kulipwa perdiem unatoka wapi ili hali yeye na mawaziri wengine wanakaa Dodoma katika nyumba za serikali?
Hata Spika na Naibu Spika, nao wanastahili hayo malipo?
Je, wanalipwa kwasababu tu na wao ni wabunge?
Kama hiyo ndio sababu, hii ni sahihi?
Je, haya sio matumizi mabaya ya fedha za umma?
Katiba Mpya ilenge kupiga marufuku mambo ya aina hii ingawa si kila kitu ni cha kuingizwa kwenye katiba.
Pia, hii ni sababu nyingine kwanini mawaziri wasitokane na wabunge.