Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

Watanzania wakati mwingine hatuwi makini. Huu uzi ni wa toka 2012, lakini wengi wetu tunadhani ni wa juzi juzi.
Pili, hakuna dhambi kwa waziri kumiliki nyumba nzuri kama tu hakutumia wadhifa wake na mali za umma katika kujenga nyumba hiyo ama katika kufanya maendeleo.

Kiongozi akishitumiwa ni wajibu wake kuthibitisha kuwa alipata mali hizo kihalali. Hizi hoja nyepesi za kusema watu wana wivu kwa kuhoji mali ya mtu fulani, hazitufikirishi na haziwafanyi viongozi wetu kuwa wawajibikaji. Jambo muhimu ni kuwa tusiingize maslahi yetu ama ya vyama katika kutetea maovu ama katika kujenga taaswira ya maovu ili Hali hayapo.
 
Wakiwa huko ccm mnawakumbatia sana na kuwakinga kama wakina chenge hata nae akienda kumjulia hali TL mtamuundia uzi
 
Reactions: bht
Hii ni hatari,tunge msamwel doe huyu laana mkubwa jk.Jamani wtz tuungane kupinga ufisadi kwa vitendo.
Hata huyo Hashim Lundenga boss wa mamiss basi angekuwa na hekalu kama hizo pesa zilitokana na umiss
 
Siyo ila siyo vizuri watu wakisoma kuwa umekwenda tofauti nao wanakubambika vyama. By the way Mbona siku hizi CUF hawaitaji au NCCR mageuzi au vimekufa?
Vyote hivyo vimemezwa na chadema kwenye ule utapeli wa ukawa
 
Milioni 600 wewe unaona ni pesa? Mbona huandiki kuhusu mikataba mibovu ya serikali gas na madini nani wa kustahili kushtakiwa? Unaelewa hasara ambayo nchi imepata? Rais aliyepita aliwahi kusema gas ikifika kinyerezi tatizo la umeme litakuwa ni historia kiko wapi sasa? tuna gas nyingi ya kuzalisha umeme na kwa matumizi mengine tuna mambwa ya kuzalisha umeme lkn mpk sasa umeme ni shida siyo wa uhakika kwanza ungetakiwa umuombe radhi mh nyalandu
 
Hiyo ni bajeti ya afya ya wilaya kwa mwaka mzima
 
Bila vielelezo kama picha na kadhalika............basi hiyo itakuwa simulizi za kutunga kama zinazowekwagwa 'FONT PAGE' za kwenye magazeti ya Tanzanite la Musiba na lile la Habibu Mnyaa Jamvi la habari
 
Bila vielelezo kama picha na kadhalika............basi hiyo itakuwa simulizi za kutunga kama zinazowekwagwa 'FONT PAGE' za kwenye magazeti ya Tanzanite la Musiba na lile la Habibu Mnyaa Jamvi la habari
Nilishakujulisheni...kuwa makini na ID zenyezaidi ya miaka 10 JF halafu zina post si zaidi ya elfu...nyingi ya ID hizi si za ' kitoto ' ( nimeeleweka)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…