Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

Tetesi: Mawaziri wa Kikwete: Lazaro Nyalandu, na Jumba la karibu milioni 600 Arusha!

Baada ya mawaziri wawili wa JK kuhusishwa na umiliki wa majumba/makazi ya mamilioini ya shilingi muda mfupi tu baada ya kushika nafasi zao Waziri mwingine anatajwa kumilimi jumba kubwa ambalo vyanzo vyetu vinakisia thamani yake kuwa ni zaidi ya nusu bilioni. Kutokana na vyanzo hivyo vya kuamika jumba hilo liko kwenye Elkirevi, Kitongoji cha Olorukwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya ndani kabisa eneo hilo linadaiwa kuwa lilipatikana baada ya Bw. Nyalandu kununua ardhi yenye eneo la Eka 3 hivi kutoka kwa wanavijiji watano. Jumba lenyewe limejengwa chini ya mwaka mmoja na kukamilikama mwishoni mwa 2011. Jumba limezungushwa na ukuta wa karibu futi 10 na juu yake inadaiwa limewekwa waya wa umeme (electric fence)

Ni kwenye jumba hili ambapo Bw. Nyalandu alifanyia Sherehe ya Mwaka mpya na bila ya shaka ilikuwa ni 'house warming' party. Taarifa hizi zinaendana na zile za mawaziri wengine ambao tayari habari zao za umiliki wa majumba yenye thamani kubwa kuliko vipato vyao na walizopata ndani ya muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Mawaziri wengine ni Bw. Maige na Ngeleja ambao wote thamani ya nyumba zao zinakaribia shilingi bilioni 1!


Hata hivyo hadi hivi sasa Tume ya Maadili ya Viongozi haijaonesha kujua mambo haya wala kufuatilia na kuyaweka wazi kama wanazo taarifa na kama kweli vyote hivyo vinaendana na mishahara yao.
Naona sasa itakuwa muda muafaka kwa Tume ya Maadili ya Viongozi kufanya kazi mkuu.
Miaka 5 baadae Wananchi wanaanza kufukua makaburi. Kuishi Tanzania kunahitaji maarifa na Nidhamu ya hali ya juu.
 
Tusiwe na double standard.
Ni nani tajiri kuliko Lowasa, Mkapa na wengine wengi.
Nyalandu ni mvuta raha tu na hajawekeza sana kwenye majumba kama hao niliowataja ambao wana majumba ya Kifahari nje ya Inchi.
Huko kwao Singida hatujasikia hata kama ana nyumba ya tembe ukiacha ya bati.
Ukisema kuhusu totos hapo atakuunga mkono na hana kificho anapokuwa nao.
 
Baada ya Nyalandu kwenda kumjulia hali Lissu huko Nairobi hapa JF makaburi yake yanafukuliwa kwa kasi ya ajabu.
 
Naona sasa itakuwa muda muafaka kwa Tume ya Maadili ya Viongozi kufanya kazi mkuu.
Miaka 5 baadae Wananchi wanaanza kufukua makaburi. Kuishi Tanzania kunahitaji maarifa na Nidhamu ya hali ya juu.
nini kimekuvutia kwenye hili kaburi la mwaka 2012
 
Pesa ndefu zipi? Au summer camp inawafanya watu kuwa matajiri haraka? Au za EOTF? Msiwe wajinga wadanganyika mwizi ni mwizi haijalishi kaiba lini na wapi, ila inavyoonekana humjui Lazaro wewe usingediriki kusema eti ana pesa ndefu kabla hajawa waziri! Ujinga mtupu.!

Lakini kwa sasa Lazaro Nyalandu ni rafiki yenu chadema baada ya kuja Nairobi na kupiga picha na Lema na Msigwa
 
Mtatafuta nyuzi zoooote za Nyalandu kisa kwenda Nairobi na bado atawashangaza haswa maana sasa hivi mazungumzo ni kwenda kule Samaratian kwa watoto wa Lucky Vicent ndio mtatia akili. Go on Lazaro Go on Nyalandu............ achana na paka wanatoa shuzi la nyama za makombo bar...................
 
Dah baada ya nyarandu kwenda kumuona Lisu tutasikia mengi sana!
 
Wakuu,mimi binafsi sioni kujenga nyumba ni issue kwa hawa wateule wa jk,issue hapa ni gharama kubwa wanazotumia kujenga hizo nyumba.hii hali inanipa "question mark" ni kweli haya majumba wanayojenga wanaweza ku justfy pesa wanozojengea wanazipata wapi?
Je? Ni mishahara na posho tu kweli? Kamati ya maadili ipo wapi?



Uwe waziri tena uliye na exposure ya kutosha ushindwe kujenga nyumba na mshahara wako plus marupupu plus ubunge labda uwe na laana kama Bashite
 
Leo hii Nyalandu ni shujaa wenu chadema!
Uzi ulitoka 2012 iweje leo ndo uamke? All in all twende Lushoto tuangalie nyumba na mashamba ya Mkapa, twende nchi nzima tuwakague akina Kagasheki na wenzao wengi tu tukirudi mumkague huyu ndugu yenu Nyarandu. Huyu ana wafadhiri ndo maana aliweza kusaidia kupeleka watoto US kwa matibabu hategemei kodi zetu.
 
Nyalandu is the next generation brain you guys. Mtachonga sana lakini mwenzenu siyo wa kizazi hiki. Amewazidi mbali mno. Hangaikeni na shida zenu, huyu chalii mwacheni kabisa.
 
Back
Top Bottom