Tetesi: Mawaziri wanne wa Awamu ya Nne kuanzisha Chama cha Siasa

Tetesi: Mawaziri wanne wa Awamu ya Nne kuanzisha Chama cha Siasa

Jaji joseph sinde warioba mungu akupe maisha marefu.
 
Wa
kwa asilimia nyingi Tanzania ina watu wasiosoma na kwa asilimia nyingi CCM inapendwa kwa hivyo usitegemee matokeo tofauti ya utafiti..
Conclusion yao ilitakiwa kusema kuwa CCM inapendwa zaidi hapa nchini.
Dr Mwakyembe,Pro Kabodi,Pro Muwongo Pro Tibaijuka,Pro Magembe,Prof Kapuya,hao mbona wasomi ni CCM
 
Kua
gazeti la Mawio la 27 April limeripoti mpango wa mawaziri wanne wa serikali iliyopita ya JK kuanzisha chama kipya
View attachment 501809 View attachment 501810
Mawaziri ktk serikali ya awamu ya nne kuanzisha chama kipya cha siasa ni jambo la heri na halizuiliwi. Ni haki ya Watanzania kikatiba.

Kuanzisha chama ni rahisi ila kukikuza na kukiimarisha ni kazi ngumu sawa na kupanda mlima mrefu kama ilivyoshuhudiwa kwa ACT Wazalendo ya akina ZZK. ACT iliwamega wafuasi wa CHADEMA. Ndivyo itakavyokuwa kwa chama kipya tarajiwa; watamega wafuasi wa vyama vingine. Zitto aliamini kuwa alikuwa na mtaji wa kutosha wa "umaarufu". Lakni mwisho wa siku matokeo yake yalionekana ingawa Mama Mghwira alifanya kazi nzuri sana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Umaarufu pekee wa wanzilishi wa chama cha siasa hautoshi. Rekodi zao nzuri za utumishi kwa umma na ajenda zao za kisiasa vinaweza kuwasaidia kupata wafuasi lakini si wa kutosha kukisukuma chama tawala ambacho kina muonekano wa mlevi kutoka madakani.

Mkakati sahihi ni kujiunga na vyama vya upinzani vilivyoko ili kuviboresha na kuviimarisha ili kuleta upinzani wa nguvu na wa kutosha dhidi ya mbinu za aina zozote za ccm na serikali yake. Mbinu mbadala ni mfano wa NASA (National Super Alliance) ya vyama vya upinzani vya Kenya vilivyoungana kumkabili Uhuru Kenyatta ktk uchaguzi mkuu ujao.

Aidha, katiba mpya ni muhimu sana kwa ajili ya kuondosha unyanyasaji wa upinzani nchini na kuweka uwanja sawa wa kufanyia siasa na uchaguzi mkuu ujao.
 
vyote kama ndo chanzo cha habari zako huwezi kuwa mwelewa. Yanaacha vitu vya msingi vingi zaidiya mahitaji ya watanzania wa kawaida.
Bora ya mawio kulikoni magazeti ya uhuru, mzalendo, tazama na kusikiliza radio uhuru ni hovyo kabisa.
 
ni Keli Mkuu vyama vote vya upinzani viungane na kumsimamisha mgombea mmoja mwenye nguvu na ushawishi mkubwa kwa watanzania kwani hawa viongozi wa upinzani waliopo sasa hawana uwezo wa kushinana na CCM tunamhitaji mgombea mwenye nguvu na hasa akiwa anatoka katika Serikali na CCM hakika atashinda kwani sasa tunahitaji mabadiliko!!!!
Mkuu hilo ndiyo tamanio LA wengi tatizo tawala wana vyama vyao huku navyo vinajiita upinzani sasa hoja hiyo ikiletwa wanaibuka na kupinga na kupewa sapoti na dola
 
ni Keli Mkuu vyama vote vya upinzani viungane na kumsimamisha mgombea mmoja mwenye nguvu na ushawishi mkubwa kwa watanzania kwani hawa viongozi wa upinzani waliopo sasa hawana uwezo wa kushinana na CCM tunamhitaji mgombea mwenye nguvu na hasa akiwa anatoka katika Serikali na CCM hakika atashinda kwani sasa tunahitaji mabadiliko!!!!
Viongozi wa kitanzania hasa wa vyama vya upinzani wakiacha ubinafsi na kuangalia maslahi yao kupitia ruzuku basi watafanikiwa!
 
Back
Top Bottom