amranik
Member
- Sep 13, 2019
- 17
- 15
MAWAZO BIRIANI CHANZO CHA KUCHELEWESHA MAENDELEO KWA VIJANA
Biriani ni kati ya chakula maarufu kinachotumia viungo vingi ili kuweza kukamilisha pishi lake na vinapo changanywa viungo vingi ndio utamu unaongezeka. Lakini katika maisha ya vijana ni tofauti, kupata maendeleo kwa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja ni ngumu sana na kufanikiwa kwa kufanya kitu kimoja ni rahisi zaidi. Kama kijana katika mawazo yako kumi uliyonayo basi chagua moja uende nalo na hapo kwa hakika utajiongezea nafasi yako ya kufikia maendeleo yako ya kiuchumi au kijamii tarajiwa.
Kwenye neno “maendeleo" kuna neno “LEO" likimaanisha ili kufanikiwa ni lazima uamue leo sababu kesho huwa haifiki asilani abadani, haiwezi ikatokea siku ukaiita kesho kila siku ni leo. Kijana amua leo kuacha kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja huku ukitaka mafanikio. Waswahili wanasema mshika mawili moja humponyoka. Chukua sasa nguvu zako ulizosimbasa kwenye matawi ya kazi zako na uanze kuwekeza nguvu hizo kwenye shina la kazi yako ambayo ndio msingi wa maendeleo yako na hapo kufanikiwa kutaongezeka zaidi ya matarajio yako.
Acha kufanya maisha yako kama biriani kila kiungo unataka kuweka, kama biriani huwa linabadilika rangi pale linapo kuwa tayari kuliwa basi tambua maisha yako yenye kazi na malengo mseto ni lazima yabadilike na yawe tofauti na matarajio yako. Kijana jitahidi sana kuwekeza muda wako mwingi kwenye kitu kimoja na wazo moja na kwa wakati sahihi na baada ya kuona matokeo chanya ya kitu hicho ni na wazo hilo itakuwa ni ruksa kuendea jambo lingine kwa kadri ya uwezo wako. Siku zote kwenye kilima kimoja huwezi kukuta chui wawili, ni lazima aishi chui mmoja mwenye nguvu ili maisha yake yawe rahisi katika kutimiza malengo yake ya kujipatia mlo wake wa kila siku. Na katika maisha huwezi kuendelea wala kufanikiwa kama utakuwa na tabia ya kufanya biashara nyingi au kazi nyingi kwa wakati mmoja, hii ni dalili mojawapo ya kufeli.
Hakuna kisicho wezekana kama utafanya sasa na wala usijaribu. Kwenye maisha ya kijana kuna machaguo mawili, ni kufanya au kutofanya na wala hakuna kujaribu. Na hakikisha unachofanya sio kwakuwa rafiki yako au ndugu yako amefanya hii si sahihi, fanya kile kilicho ndani ya uwezo wako. Kila mtu yupo vizuri kwenye sehemu yake, unaweza kuwa vizuri kwenye kubuni au kufanya au kutoa ushauri au kuchanganua mawazo ya watu na huwezi kuwa bora katika kila eneo na hii haimaanishi uache kufanya jambo la mafanikio. Jitahidi sana kijana uweze kujua je wewe upo bora sehemu gani? Nikikumbuka enzi zile za kidumu na mfagio, nilipenda hisabati na kiswahili kuliko kiingereza na sasa ndio naelewa kuwa nilikuwa sipo bora kila somo lakini nilifanya vizuri kwa yale niliyokuwa bora zaidi. Kwa kutambua wapi nipo bora zaidi kulifanya nione shule ni kama kucheza na kamwe sijawahi kufikiria kufeli.
Udhaifu wako kwenye jambo moja ni ubora sahihi kwenye jambo jingine, kama unaogopa nyoka haimaanishi utaogopa mende na kama utatumia dakika kumi kunywa lita moja ya maji basi robo dakika itakutosha kunywa robo glasi ya maji. Kama kijana usilazimishe mafanikio yako yatokee sehemu ambayo haupo bora, tambua udhaifu wako, tambua ubora wako, chagua nyenzo zako za mafanikio na katu usirudi nyuma kwa kuogofya kutofanikio. Kama ukifeli kupata kile unachokitarajia haimaanishi kuwa ndio haupo bora, kufeli kutakufanya uwe bora zaidi kwakuwa utaweza kupata uzoefu na nafasi ya kurekebisha pale ulipo kosea na mwisho wa siku kuna uwezekano mkubwa kufanikiwa zaidi ya vile ulivyo ulivyotarajia hapo awali. Kama siku moja ulishawahi kuweka pesa kwenye mfuko uliotoboka basi siku za usoni utakagua mfuko wako hata kama ni mzima. Aliyewahi kung'atwa na nyoka hata akiguswa na jani ni lazima ashtuke na kuwa na tahadhari kwa hatua anayopiga lakini hawezi kuacha safari kwa kuogopa nyoka.
Kuwa na mafanikio ni lazima uwe na matamanio, matamanio ya kupata matokeo ya kile unachokifanya na kukiamini, ni ngumu kupata matokeo sahihi kama utakuwa na mawazo mseto ya jinsi gani ya kufanya malengo yako. Na vivyo hivyo bila kuwa na matamanio ya maendeleo au mafanikio kwa kazi au biashara unayoifanya ni sawa na kwenda shule na hutamani kupata elimu iliyo kupeleka shule. Kwanza ni lazima uwe na tamaa ya kufanya, tamaa ya kumiliki, tamaa ya kuanza, tamaa ya kufanikiwa katika maisha. Kutamani mafanikio sio dhambi wala sio kitu kibaya, ubaya unaweza kuletwa na njia utakazo zifanya uli kupata kile unacho kitamani.
Vijana wengi matamanio ya maendeleo huwafanya kukiuka maadili na hata kuvunja sheria kwa kudhani kuwa hawana njia sahihi ya kutimiza malengo yao zaidi ya njia ovu. Mkataa pema pabaya panamuita. Kama ukikataa kujituma ili kupata unachokitaka basi njia mbaya itakufata popote ulipo na popote uendapo.
Kiujumla kijana fikiria ni wapi upo bora zaidi na ni vipi utaacha mawazo mseto na kuwa na lengo au wazo kuu moja. Hii itakuongezea umakini wa kina na urahisi wa kufanikisha lengo lango. Miluzi mingi hupoteza mbwa, mawazo mengi hupoteza dira na mwanga kwa kijana kufanikiwa na hasa vijana wengi waliomaliza vyuo walikuwa na mawazo mengi sana ya kimaendeleo. Vijana wakiwa bado wapo chuo kauli zao huwa ni kama vile ‘zabibu inapesa sana ‘, ‘tikiti inapesa hatari’, ‘naanza kuuza nguo ili nikimaliza niwe na duka langu kubwa la nguo’, ‘biashara za mtandaoni zinalipa’, ‘forex siachi mwamba’, ‘kuna app hiyo inalipa sana', ‘kusoma hakuna ishu’ cha ajabu ni kwamba baada ya kumaliza vyuo vijana haohao wenye mawazo mengi ambayo waliamini watafanikiwa utawakuta mitaani hawajafanya hata kimoja na bado wanalalamika kila uchau kwamba hakuna ajira. Hii ni mfano wa kuwa na mawazo mseto au mawazo biriani kwa vijana katika kutafuta mafanikio yao. Tafadhali vijana tuchague wazo moja bora na tulifanjie kazi kwa kupambana nnaimani tutafanikiwa
Chukua wazo moja, ishi ndani ya wazo lako, lifikirie liwaze na hatimae utaliweka kwenye vitendo na kufanikiwa. Mawazo bila vitendo haina maana.
Mwandishi: CHALI
Mawasiliano: 0718167997

Upvote
4