Baada ya kuwaza sana nimeona kabisa kua naweza jifunza kua mtu mzima nikiwa bado kijana, mtu mzima in sense that niko na busara, uchumi uliotulia nk.
Katika kufikia malengo ya kuishi kama mtu mzima mwenye busara na heshima huku nikiwa mdogo nitafanya yafuatayo
1. Nitaanza kuvaa nguo za heshima, sio vimodo vilivyobana na jinsi za kuchanika ( sijawahi kuvaa vimodo tho)
2. Nitajifunza ujuzi ambao utanipatia kipato na nitaifanyia kazi kwa muda mrefu hasa upande wa cyber, like cyber security
3. Nitakua nafanya mazoezi na kula vyakula visivyo na athali sana kiafya, nitaepuka procecced sugar, mafuta mengi nk
4. Nitaepuka madeni kwa gharama yoyote
5. Nitaanza ku invest na kununua ardhi
6. Nitatulia na mwenza wangu mmoja
7. Nitajiepusha na dhulma na maovu, kuwatendea watu wema na kujitenga na watu waovu as soon as i can.
8. While I do all that, nitajitahidi ku enjoy life as much as i can with peace to be the my priority.