SoC04 Mawazo thabiti ya namna ya kuyafikia maendeleo nchini Tanzania

SoC04 Mawazo thabiti ya namna ya kuyafikia maendeleo nchini Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Massawe John

New Member
Joined
Jun 13, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Uwazi na uwajibikaji thabiti katika uongozi; ikiwa taifa litatunga sera,sheria na miongozo ambayo itakwenda kuzilazimisha tawala/watawala kua wawazi katika utendaji na utekelezaji wa shughuli za kiserikali hii itaenda kupunguza au kuondoa kabisa ubadhirifu wa rasilimali za taifa na kodi za watanzania,mfumo wa utawala ulipo hivi sasa hauweki maswali ya uwazi katika utawala wa taifa letu kwa sasa hii ndio maana hata bajeti mbalimbali hasa za ofisi za viongozi za viongozi wakuu wa nchini haziwekwi wazi jambo ambalo linziweka pabaya rasilimali za taifa letu kwani kiongozi anaweza kufanya jambo lolote bila wananchi kujua na huenda wakafahamu baadae wakat ambao tayari madhara yameshaonekana na ngumu kuzuia au kulithibiti

Mabadiliko katika mfumo wa elimu;sote ni mashahidi kwamba mfumo wa elimu wa sasa hauendani na uhalisia wa soko la ajira la sasa licha ya hilo kwa kiasi kikubwa mitaala yetu inayotumika mashuleni kuanzia elimu ya msingi mpaka chuo kikuuu haina uhusiano wa moja kwa moja na mazingira,tamaduni,mila na hata desturi za kitanzania,ili kuyafikia maendeleo kama taifa ni lazima yafanyike mabadiliko mathubuti ambayo yataenda kuwaandaa vijana au wanafunzi (wahitimu) kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira uliopo hivi sasa,elimu itakayolenga kumpa mwanafunzi ujuzi,elimu itakayolenga kumwandaa kijana sambamba na mazingira halisi ya kitanzania

Ushirikishwaji wa wananchi katika kutoa maamuzi;mara nyingi wanachi wamekua wakiachwa nyuma katika kutoa maoni hata maamuzi katika mambo ambayo yanawagusa wao wenyewe moja kwa moja.Mfano wakati fulani tulikua tukizungumza na wavuvi wanaoendesha shughuli zao katika ziwa Victoria katika Wilaya ya nyamagana mtaa wa Sweya lengo likiwa kutaka kujua changamoto wanazozipitia hasa wakati ziwa linapofungwa ili samaki na dagaa wakue mmoja wa wavuvi wale alilalamikia maamuzi yale na kudai kua hawakushirikishwa kwenye kutoa maoni na maamuzi jambo ambalo hata sasa limebaki kuwaumiza hivyo tunaweza kuona kwa hakika ipo haja ya
kuwashirikisha wananchi na wadau katika kutoa maamuzi hasa katika mambo ambayo yanawagusa moja kwa moja.

Kuwekeza nguvu katika kukuza sayansi na teknolojia nchini;sote ni mashahidi kwamba ulimwengu wa sasa umebadilika sana,dhana halisi ya sayansi na teknolojia imebeba maendeleo ya ulimwengu wa sasa kwa kiasi kikubwa,ni wakati ambao sasa taifa linapaswa kutunga sera wezeshi zitakazo pelekea kuinua sayansi na teknolojia nnchi,hizi zinaweza kua kuanzishwa kwa ushirikiano thabiti wa taifa letu na nnchi nyingine katika bunifu za kisayansi hasa katika kuwafundisha vijana wakitanzania katika hili tumebaki kua watu wakuiga tuu badala ya kubuni au kushirikiana katika kubuni vitu mbalimbali hii itasaidia maendeleo katika sekta mbalimbali kama vile afya na kilimo kwani kama taifa tutaweza kubuni mashine mbalimbali ambazo zitaenda kurahisisha ufanyaji wa majukumu katika maeneo haya.

Kuwasaidia vijana wenye nia na waliojaribu katika bunifu mbalimbali;siku za hivi karibuni tumeona hata kushuhudia bunifu mbalimbali zinazofanywa na vijana mbalimbali,Mfano ni kijana Leonard Shayo aliyebuni satelite kwa kutumia nguvu na jitihada zake binafsi ata hivyo kutokana na kasumba na kudharauliana sisi kwa sisi wenyewe halijawashtua wengi na hii inadhihirishwa na mapokeo ya watanzania wenyewe hata serikali ambayo haijaonesha nia ya kumsaidia kijana huyu aliyefanya ubunifu mkubwa huu.Zipo bunifu nyingi ambazo serikali imeshindwa kuziendeleza kumbe huenda taifa letu lingekua na uwezo wa kujitegemea katika mambo mbalimbali ambayo tungweza kuzalisha kwa teknolojia yetu wenyewe (ya ndani)

Maboresho na uwekezaji katika miundombinu ya usafiri nchini hasa vijijini;mara nyingi tumeona serikali ikiweka vipaumbele na nguvu kubwa katika maeneo ambayo tayari yameendelea (Mijini) na kusahau vijijini ndiko zinapotoka rasilimali muhimu na hata Malighafi zinazohitajika mijini,vipi tutaweza kusafirisha malighafi hizi kama hatutawekeza katika miundombinu vijijini? Hivyo ni wakati sasa serikali ikageukia vijijini na kuboresha miundombinu kwani hii itasaidia na kurahisisha usafirishaji wa malighafi na bidhaa nyingine muhimu kutoka vijijini na kwenda mijini.

Kuhakikisha upatikaniji wa nishati ya umeme wa uhakika;Changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara maranyingi imeendelea kua kikwazo katika maendeleo hasa katika maeneo ya uzalishaji kama vile viwandani na maeneo mengine ambayo yanategemea nishati ya umeme katika uzalishaji,vipi tutawavutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini kama hatuna nishati ya umeme ya uhakika? Jibu ni kwamba haiwezekani hivyo ni wakati sasa Serikali ikawekeza nguvu kubwa katika sekta hii ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini hii itasaidia kuwavutia wawekezaji na hata kusonga kwa shughuli muhimu nchini.

Kubana na kupunguza matumizi ya serikali;limekua jambo la kawaida sana kuona misafara ya viongozi mbalimbali nchini ikiwa imesheheni magari na vyombo vingine vya usafiri kama vile pikipiki vyombo hivi vinaulazima gani kuambatana ? Vipi kama bajeti ya kuendesha misururu hii ya magari tena ya bei ghali itaelekezwa katika shughuli nyingine muhimu? Hivyo ni muhimu kupunguza bajeti ya ziara za viongozi mbalimbali na badala yake fedha hizo zielekezwe katika mambo mengine muhimu na ya msingi kama vile ujenzi wa miundombinu ya barabara,Mahospitali na shule mbalimbali nchini.Si hivyo tuu hata kupunguza mishahara ya watumishi wa serikali katika ngazi mbalimbali nchini mfano wabunge ambao inakadiriwa hupokea zaidi ya Milioni 10 kwa mwezi kiasi kiasi ambacho kama kitaelekezwa katika matumizi mengine msingi inaweza kuchangia katika maendeleo kwa kiasi kikubwa.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom