cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Hii pia iko vizuri.Umekosea kumwambia Dunia imebadilika Kama sehemu ya kumshutumu na kutomuamini.
Hapakuwa n haja ya kumueleza mambo hayo.
Mosi,
Ungemwambia tuu Nyumba yenu ni ndogo, na hutajisikia vizuri yeye kulala Sebuleni, hivyo unashauri muende mkatafute Lodge ya kulala ili awe Comfortable kuliko kulala pale sebuleni.
Pili,
Kama alikuja Kwa kushtukiza, ungemfuatilia mapema kabla ya saa mbili usiku kujua Kama atalala hapohapo au Ratiba yake imekaaje, kisha Kama Ratiba yake alipanga kulala hapohapo basi ndio ungemueleza Hali halisi ya Nyumba yako.
Tatu,
Kama anaukariby Mkubwa na wewe ya Mkeo mbali na undugu.
Basi ungemchukua mtoto mkalala naye kisha Mgeni akatumia chumba cha mtoto.
Hata hivyo ni lazima kesho yake umuweke wazi kuwa ulimpokea Kwa heshima yake tuu lakini hupokei wageni wanaokuja Kwa kushtukiza.
Hiyo ingemuambia kuwa hatakiwi na pia ingemfanya siku nyingine akija atoe taarifa.
Pia Kwa jitihada ulizofanya za kumlaza hapo au kumlaza Guest angeona umemuheshimu.
Pia ungejifanya unaulizia pesa ya Guest Kwa mke wako kama ipo, ili kumfanya ashtuke kuwa amekuja kuvuruga Bajeti za watu.
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app