Maxence Melo: 2017 niliwahi kufuatwa na watu wasiojulikana ila Balozi wa Umoja wa Ulaya akaninusuru!

Maxence Melo: 2017 niliwahi kufuatwa na watu wasiojulikana ila Balozi wa Umoja wa Ulaya akaninusuru!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
IMG_20220621_174429_555.jpg

Akihojiwa kwenye kipindi cha kinagaubaga ndugu Maxence Melo amesema walikuja watu wasiofahamika wakitaka kumchukua ili wakamhoji kwanini amefanya mahojiano na Balozi wa Umoja wa Ulaya, lakini Balozi aliwakatalia katakata akisema hamuwezi kumchukua nikiwa naye mimi.

Kweli nchi ilikuwa ngumu sana

======

Kwenye #KurunziLive leo tunaungana na Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji wa #JamiiForums (@macdemelo) anayehudhuria kongamano la vyombo vya habari ulimwenguni hapa mjini Bonn.

Tutaangazia baadhi ya masuala yanayojadiliwa kwenye kongamano lenyewe. Vilevile mafanikio na changamoto zinazokumba vyombo vya habari nchini mwako ikiwemo mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ya kidijitali.

Je matarajio yako ni yapi kwenye kongamano hilo? Je una swali ungetaka tumuulize Maxence Melo? Na je vyombo vya habari vimefanikiwa kwa kiwango gani kuangazia masuala yanayokugusa?

Tuandikie maoni yako, na usikose kuungana nasi mubashara itimiapo saa kumi kamili majira ya Afrika Mashariki.
 
Akihojiwa kwenye kipindi cha kinagaubaga ndugu melo amesema walikuja watu wasiofahamika wakitaka kumchukua ili wakamhoji kwa nini amefanya mahojiano na balozi wa umoja wa ulaya, lakini balozi aliwakatalia katakata akisema hamuwezi kumchukua nikwa nae mimi.

Kweli nchi ilikuwa ngumu sana
Na bado nchi ngumu, labda ninyi mnalamba asali.
 
Akihojiwa kwenye kipindi cha kinagaubaga ndugu Maxence Melo amesema walikuja watu wasiofahamika wakitaka kumchukua ili wakamhoji kwanini amefanya mahojiano na Balozi wa Umoja wa Ulaya, lakini Balozi aliwakatalia katakata akisema hamuwezi kumchukua nikiwa naye mimi.

Kweli nchi ilikuwa ngumu sana
Huu uongo kwanini wasubiri awe na balozi ndo watake kumchukua? Kwani hawazijui ofisi zake zilipo? Au huwajui nyumbani kwake?
 
Kama taifa tulipitia wakati mgumu miaka sita iliyopita, lakini hata sasa bado magumu yapo hasa kwenye upandaji bei wa bidhaa mbalimbali, chini ya utawala wa CCM ni kubadilisha matatizo tu.
 
Hayajakufika!!! Utajua Ni kweli au uongo. Ila Wewe si Chawa na upo kazini!!? Sikushangai. Endelea kujipekecha.
Hao waliiuwa walamba asali kipindi cha utekaji mkuu
 
Back
Top Bottom