Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,158
Nilishika ujauzito tukiwa Honeymoon Mombasa. Nilistuka baada ya kurudi na kuanza kazi hali ya kutapika ilipoanza . Vyakula vingi vilinikataa, niliishi kwa banana milk shake. First trimester nililazwa siku tatu hospitali hakuna kilichokaa tumboni.
Nikisikia harufu ya mayai hata kama jirani anakaanga nitatapika vibaya sana. Mwisho ilikua hata nikiyaona tu. Mayai yalikua adui mpaka siku ninajifungua. Baada ya mama mkwe kupata habari ya uzazi kesho yake alikuja hospitali na chai, mayai, mikate na nguo za mtoto pamoja na madera ya mzazi.
Nilipoona mayai nilimwambia mama si unajua mayai siwezi kula. Alicheka sana alinijibu kula tu ugonjwa umepona. Niliyala na wala sikutapika.
Mimba ya pili ilinitesa kwa miezi mitatu ya kwanza lakini ya tatu nilikula kila kitu mpaka muda wa kujifungua.
Tupe experience yako ya mimba.