Wakuu,
Kuna msiba mkubwa mno kwa hawa wafugaji wa kuku wa mayai ya kisasa, takribani mwezi sasa mayai yamefurika mji mzima - hakuna soko kabisa.
Imefikia hatua sasa mayai yanaanza kuharibika kwa kukaa muda mrefu bila soko, inasemekana mayai yametoka nje ya nchi - tetesi ni kwamba yametoka Kenya kwa njia za panya. kwani ushahidi unaonyesha kwamba mayai yanayozalishwa Tanzania hasa Dar - es - Salaam hayawezi kabisa kujaza soko la ndani.
Bei ya mayai haya imeteremka toka 7500 - 8000 kwa Tray moja hadi kufukia 4500 - 6000 Tshs. Lakini pia hayanunuliki hata kwa bei hiyo.
Tunaomba wahusika na wadau wote wa mifugo hasa Wizara ya mifugo waliangalie suala hili kwani linaua kabisa wafugaji wadogo wadogo.
Nawakilisha kwa niaba ya wafugaji wa kuku wa mayai.