Mayai yamefurika Dar es salaam, Soko hakuna wafugaji ni Msiba

Mayai yamefurika Dar es salaam, Soko hakuna wafugaji ni Msiba

Sidhani kama kuna ukweli wowote juu ya kuingizwa kwa mayai kutoka nje ya nchi, yawezekana hizi ni hisia tu.
Ukweli ni kwamba biashara ya mayai hasa kwa dsm ilianza kuyumba kipindi kile cha mwezi mtukufu baada ya mfungo kuisha biashara ikatengamaa ila kwa kuwa uzalishaji umeongezeka kupita mahitaji ndio maana soko limefurika...

Ushauri wangu watu wasikimbilie tu kufuga kuku kwa kuwa jirani yako nae anafuga, na kama ukiamua kuiga basi tafuta hata hotel au mlaji wa uhakika uingie nae mkataba, pia wafugaji wawe wamoja kusaka masoko. Pia kufuga mifugo mingine kama ngombe mbuzi, sungura n.k
Mbona kitimoto soko lilishuka now
Liko fantastic

Wajipange tu
 
Mi situmii hizo vitu cauz ni cancer tupu..mi ni mwendo wa kienyeji..over
viroba ruksa siyo - maana vinajenga afya ya akili.

tumekusoma kwa ushauri wako.
 
Mbona kitimoto soko lilishuka now
Liko fantastic Wajipange tu

Pdidy- wapi soko zuri la kitimoto? Niko Arusha huku wenye mabucha ya Mianzini wanatutesaje?! Kweli hii changamoto ni ya majority ya wakuli na wafugaji.

Fuso - poleni mkuu. Chama cha wafuga kuku kipo/vipo. Sema kutafuta masoko haikawa priority. Kuna chama kimoja huku walivuta mikopo ya nguvu na tangu 2012 walikuwa na mikakati ya kulikabili soko la Comoro. Sijui wamefikia wapi ila wale walikuwa very serious... Members walikuwa wako na kuku 1000 or more.
 
umeongea point hapo, hakuna mtu anayeweza kufanikiwa in isolation, vyama/chama kama kipo kimechukua hatua gani?
Inasikitisha sana watu wanavyofanya juhudi kujikomboa ila wanakamishwa na mambo yanayozuulika kama bidhaa kutoka nchi jirani.
Moja ya kazi ya chama ni kuwalinda member kwenye bei na soko la bidhaa zao. Kuwatafutia na masoko nje ya Nchi kama ndani kumejaa.
 
Kuna wakati nilikuwa natafuta mayai. Yule mama alinijibu kwa maringo sanaa. Sasa nashangaa juzi juzi ananipigia simu huku amepanik na kwa unyenyekevu kunikumbushia kuhusu mayai. Nikamwambia mi hiyo biashara nilishaipotezea maana bei ya mayai ilikuwa sky rocketed at that time...
 
Kufanya biashara na hawa kina mama wanaoijua pesa ukubwani ni shidaaah!! Haukua peke yako mkuu.
 
wewe hata ukiacha kula, kama afya yao ni mgogoro itaendelea kuwa hivyo hivyo tu.

Ndiyo mdau hata akiacha kulavkm ni wa kufa na cancer atakufa nao tu. Huwezi kusema vibaya juu ya biashara ambazo wenzako zinawaweka mjini kwa ronours zisizokuwa za UONGO
 
ndo changamoto za biashara hizo.....kinachotakiwa ni kukubaliana na hali.....hata kama hakuna soko wewe endelea kuwalisha as if unalisha vifaranga...kuna siku demand itaongezeka...hiki ni chakula...hakina kupitwa na fashion
 
Ninavyo jua mayai kwa sasa hayaruhusiwi kuingizwa Twnzania, kuhusu Supply kuwa kubwa kuna factor nyingi sana zinazo sababisha kuwa hivyo.
1. Uzalishaji kuongezeka. Hiki ni kipindi cha joto Kari sana na utagaji unakuwa mkubwa sana na utakuta hata miji yenye baridi kama Arusha kwa sasa utagaji uko juu sana.

2. Producer kuwa wengi sana. Kipindi hiki kuelekea sikukuu watu wengi huingia kwenye game na hivyo kuingeza supply.

Kuhusu Mayai Kutoka Kenya.

Ukweku ni kwmnba Wakenya ukienda kwao wao wanalalamika mayai kuingia from uganda. mayai mengi sana yanaingia kenya kutoka uganda na wanacho fanya wakenya ni kupambana.

Nini kufanyike?

1. kureduce cost za uzalishaji. huwa nashindwa kujua ni kwa nini Kenya wauze mayai bei rahisi ilihali Gharama ya chakula cha kuku kwa kenya iko juu sana ukilinganisha na Tanzania.
Tanzania watu wanatafuta Super profit that is wht.
Kwa sababu tuko kwenye Dunia ya utandawazi no way out ni lazima kupambana na ukiona hali kama hii anza kufanya utafiti unawezaje punguza gharama za uzalishaji ili hataa mayai yakishuka bei bado uweze kupata profit.

2. Watu waache kufuata mkumbo. wengine fugeni kuki wa mayai, wengine wa nyama na wengine kienyeji na wengine tuingie kwenye uzakishaji wa chakula cha kuku.

3. Wewe kama mzalishaji ni lazima utafute soko, jaribu kutafuta siko la kudumu la product yako.

Baadae make kuna mambo uameingiliana tutaendelea wakati mwingine
 
umesema kweli Chasha kuongezea tu msimu wa mavuno chakula bei cheap na wafugaji bado wana mavuno hawahitaji kuwauza kuku wao kupata cash. Hivyo mayai yanakuwa mengi, chakula kikipanda, mavuno yameisha, mahitaji kwa sikukuu, fees mwisho wa mwaka ukichangia mvua kwa wale wa free range bei itapanda. Nafikiri ni kujifunza kupanda na kushuka na bei, pia kwanini hakuna viwanda vya mayonnaise to add value mayai. Mwisho muungane kushika tender kubwa na kukataa madalali.
 
Naomba kujua now bei ya chini kabisa ya mayai hapa dar... nijulisheni 0779420000
 
Hujataka tu kuelewa lakini amemaanisha hivi...

"... hii bei wabongo wanaisema ndogo na kuwasababishia hasara lakini kwa wenzao wa Kenya bei hiyohiyo inawaletea faida" ..

Wabongo bhana mnajifanya wajuaji sana ee
Unajua sometimes kama hujui kitu bora ukae kimya. Kuna sababu kadha wa kadha kufanya ya bongo yawe bei juu. Anza na gharama za umeme, then fuatisha vitu vingine. Unatakiwa uwe na literacy kidogo ya kiuchumi kiabla hujaanza kubwabwaja tu. Unaifahamu walmart? Walmart wana sifa ya kuua masoko ya ndani duniani kwa kuuza bidhaa kutoka nchi nyingine ambazo zimezalishwa kwa bei ndogo zaidi. Sasa kama nchi haina policy ya kuwalinda wazalishaji wa ndani ni shida. South Africa ni nchi mojawapo ambayo wanawalinda wazalishaji wa ndani. Tanzania ni soko holela halina mwenyewe. Serikali inatakiwa iwalinde wazalishaji wa ndani sababu kunakuwa hamna fair competition. Mkulima au mfugaji wa Tanzania anajaribu kuuza kwa bei ghali sababu ya nature ya gharama za uzalishaji. Inawezekana kuzalisha mayai Kenya ni bei rahisi zaidi kuliko TZ. LAkini kama serikali ipo makini then mayai ya bei rahisi hayawezi kuingia. Tunahitaji tujitosheleze sisi wenyewe kwa faida za kiuchumi. Tunahitaji kwanza soko la ndani tuli capitalize. Then kukiwa na upungufu na ya kutoka nje yanaruhuhusiwa kidogo kufidia upungufu. Wewe kufurahia ya Tanznaia kukosa soko inaonyesha kwa kiasi gani ulivyo mbumbumbu halafu kutwa unalalamika Tanzania. Unatakiwa ujivunie ukiona bidhaa za ndani zinafanya vizuri na sio kutoa negative commnets utadhani unafikiri kwa makalio. Ila sio kosa lako. Shule ya vidudu TZ.. Primary TZ.. Sekondari TZ..Chuo kikuu TZ. Then ukapata kazi DAR. Hujawahi safiri kwenda mbali kupata exposure. Halafu unakuja hapa unaonge ongea tu.
 
Labda kama umekosea mtu wa kumquate.
 
Zungumzieni na madhara ya kula mayai hayo sana!Naamini watu wengi wamepunguza sana ulaji wa mayai kutokana na jinsi yanavyopigwa vita!Kila ukisikia cholesterol,unene,uzembe!vyote hivyo huhusishwa na mayai hayo hayo!Wengi wameanza kuyaogopa

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hapo dodoma mayai viza yanauzwa ghali na yana soko kubwa kuliko mayai mazima.
 
Back
Top Bottom