Asante sana Murutongore kwa pole zako. Ila kuna kitu kimoja inabidi uelewe kuwa migororo ya nchi jirani inatuathiri na imekuwa ikituathiri kwa miaka mingi kwa kuigeuza nchi yetu kuwa kimbilio la wakimbizi wa mataifa mbalimbali ikiwemo Rwanda, Uganda, Burundi, DRC, Somalia, Zimbabwe, South Africa, Mozambique, Malawi na mengineyo. Na kila wanapokuja wamekuwa wanasababisha matatizo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kwa nchi yetu. Ndio maana inabidi mtuelewe tunapowashauri mkae na wapinzani wenu muongee kwani lengo letu ni moja tu kuwa na amani kwenye huu ukanda wetu ili tujikite kwenye kuubadilisha uchumi wa nchi zetu na kuboresha maisha ya wananchi. Sisi tunabishana na kupingana bila kupigana ndio maana kila inapotokea kutokuelewana kati ya chama tawala na wapinzani Rais wetu huwakaribisha Ikulu kufanya mazungumzo ya kutatua matatizo na mara zote tumekuwa tukifikia muafaka. Mnaweza pia kujaribu hilo. Nelson Mandela asingekubali kukaa na wauwaji wa waafrika na watu waliomfunga yeye binafsi kwa miaka ishirini na saba (yaani makaburu) leo hii Afrika Kusini isingekuwa hii tunayoiona. Kagame anaweza kujifunza mambo mengi toka kwa Nelson Mandela.