Hata mimi mkuu hilo nilijiuliza sana. Ila baada kufatilia kwa undani sana nikagundua kama siyo Mayweather basi ana washauri wanapenda pesa sana. Pia Pacquiao aliona ngoja akubali tu 60/40 ili mradi mashabiki wapate wanachokihitaji la sivyo pambano lingekuwa hamna.
Hili pambano limeanza kuzungumziwa tangu 2010, Mayweather akaanza kutoa sababu baada ya sababu; Pac apime damu, Pac alivyokubali kupima damu, akaja na 20M kwanza, Pac akakataa akang'ania 50/50, Mayweather akaja na 40M ikakataliwa, Pac baada ya kupigwa na Marquez akaona pambano halitakuwepo tena, Pac akaanza kulisaka pambano tena, kukawa na mabishano tena ya makampuni yanayowawakilisha HBO na Showtime. Mpaka walivyokutana januari Pac na Mayweather uso kwa uso sasa ndiyo wenyewe wakakubaliana 60/40. Na bila Pacquiao kukubali kujishusha kukubali vitu ambavyo Mayweather anavihitaji pambano lisingekuwepo.
Kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia ndiyo maana hakuna hata mkataba wa marudiano, lakini tushukuru yote yamepita na yamekubaliwa sasa tuone mpambano kwanza.