Aisee! Pole nyingi ziwafikie. Kuishi hiyo miezi 3 na kuendelea bila salary siyo jambo jepesi hata kidogo. Kuhusu kubadili matumizi sidhani kama itasaidia maana mtaani zimetapakaa zile barakoa za mafundi cherehani.
Isitoshe tangu serikali ilipoanza kuficha kutoa taarifa za waathirika wa Covid 19, ni ukweli ulio wazi! Baadhi ya Wananchi wameanza kuipuuza Corona na hivyo hawana kabisa muda kuvaa barakoa kwa sasa.
Kwa hiyo hata kama hicho kiwanda kitabadili mbinu, bado kitakutana na changamoto nilizo zitaja hapo juu.