Kuna siku itafika tutakuja kulia wote humu (uwe na kazi, usiwe na kazi, uliwahi kupata corona ama hukuwahi), wote yatatukuta. Kama corona ikiendelea kusimamia kucha hivi, sote tutaimba wimbo mmoja!!! Kuna watu washaziba masikio, wao washavaa jezi za kijani, kazi yao ni kusifu tu kama vile watakuwa salama! Ni wazi tuna haja ya kukubali, serikali yetu ina mambo mengi ya kufanya na kutathmini hali ya nchi wakati na baada ya corona. Kuna vitu ndiyo (kama hizi ajira kupungua) haiwezi zuia, lakini huu ni wakati wa kutumia sana rasilimali watu iliyonayo kujikita katika kufanya maamuzi ya kitaalamu zaidi kuliko kuendelea na "business as usual". Kuna wataalamu wa afya, uchumi, usalama, nk, kama tulikuwa tunawa'underutilize" huu ni muda wa kukamua utaalamu wao hasa. Huko mbele hatujui hata hali ya usalama itakuwaje!? Mfano mdogo tu, hivi tumefikiria hili kundi lote hapa lililosimamishwa kazi litaishije? Wapo watakaoishia kwa maji kwa siku, wapo watakaolala nje, wapo watakaochukuliwa mali zao na taasisi za fedha...na wapo watakaoanza kuvamia majumba ya wale waliokuwa na uwezo wa kujiwekea "lockdown" usiku (au hata mchana). Hii ngoma ikisimamia kucha, hata aliye mtoa mapambio wa rangi ya kijani hatokuwa salama. Serikali itupe mapumziko hata kidogo na siasa majitaka, tunahitaji tathmini na mpango kazi wa kitaalamu zaidi.