Mazda CX-5: Gari yenye muonekano mzuri sana Interior na Exterior

Hapana wewe second gen unasema ndo unasema first
We unaongelea Mazda Demio, mi nikawa na refer Mazda 2.

Nafanyaga ivo kwakua nina Mazda 6 (sio Atenza) na mshikaji wangu ana 3 (sio Axela).

Demio = Japan ina 4 generations.
Mazda 2 = Europe ina 3 generation.

Means Mazda 2 yenyewe ilianza wakati Demio yupo 2 Gen yenyewe ndio ikawa 1st Gen.

Kumradhi boss.
 
Mkuu samahani naomba elimu hapo juu ya mazda ya diesel kwanini unatakiwa kuwa mtu wa trip?
 
Mkuu samahani naomba elimu hapo juu ya mazda ya diesel kwanini unatakiwa kuwa mtu wa trip?
Hii ni kwa magari yote ya diesel mkuu, sio tu Mazda.

Kila baada ya muda flani, mfumo wa kutoa moshi tuseme unatabia ya kujenga kutu (carbon) sasa iyo carbon ili itoke inataka gari lifikie joto flani ndio iingie katika stage inaitwa regeneration ndio inatoa iyo kutu.

Kuna kitu kinaitwa EGR na DPF ndio vinavyohusika kutoa iyo kitu.

DPF ni kama chujio hivi lipo kwa chini kwenye exhaust pipe, unaweza kulitoa kisha uka program gari inakua inafanya kazi kama Petrol tu ila niliongea na mafundi wakasema 850k nikasema no way.

So kila baada ya wiki moja la kuendesha gari vitrip vifup vifup ninachofanya natafuta trip ndefu moja ili gari ifanye regen.

Kwa Dar kama hauna trip unajiendea Bagamoyo au Usiku hii njia ya Kimara Mwisho to Kibaha ni nzuri.

Gari linachotaka ni kuendeshwa kama kwa 30 minutes nonstop kwa speed ya 50kph kwenda juu.

Sema sijaeleza vizuri ila unaweza tafuta kusoma Google: Diesel car DPF au Mazda DPF
 
Shukrani sana nimefahamu.
 
Unaanza kidogokidogo kaka .

Unanunua gari ndogo,unajichanga unaenda tena unanunua kubwa kidogo.


Badae unanunua gari ya ndoto yako.

Wengine tunanunua gari yoyote kuokoamuda na kuepuka msongamano wa kwenye basi na daladala
Nitaanza na sientaπŸ˜‚
 
Mkuu kama hutojali naomba ufafanuzi zaidi kwenye hiyo sentensi

Kwa bei yake, hata ya second generation unapata gari yenye better power, technology na fuel economy kuliko gari nyingi za aina yake. Mfano tu Harrier 2nd generation ya kabla ya 2013 ni bei ghali kuliko hizi gari miaka ya 2013
 
Toka kitambo meli zote za magari zinapitia bandari ya Mombasa alafu inakuja DAR na ikishafika DAR inaenda Durban
Meli iliyoleta chombo yangu ilitoka Japan ikaenda India na Singapore, kisha Durban, Maputo, Dar, ikaendelea mbele. Ilikuwa June 2023.
 
Maisha haya tafuta lakini usisahau kukata β€œKIU YAKO”

Kama unapenda kusafiri safiri

Kama unapenda gari yoyote nunua

Hela utaziacha
Very true !! Tunahangaika na maisha hadi tunashindwa kuishi maisha yenyewe,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…