Mazda kwanini hazipendwi Tanzania ilhali bei yake ipo chini?

Mkuu spea zipo siku hizi. Uhindini kama morogoro autospare, tuffy sparee wanazo. Pia Toyota watu wanaona services ni bei rahisi sababu wanaziabuse na hawafuati manual. Mfano gari za 2006 onward zinataka synthetic engine oil 5w30 au 5w40 au 10w40 sasa angalia bei zake Total au Castrol. Filter original ya Toyota pia ina bei. Tatizo tunaweka substandard stuff tunasema service bei rahisi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bei za makampuni haitofautiani sana autocom,autorec ,sbt ,enhance,trust,beforwad, trade car view bei zao za magari almost ni the same ila kinachotofautisha huwa ni km na mwaka wa gari
Watu wanaouza magari quality toka Japan wanaitwa Japanesevehicles.com humo bei zake unakaa...
 
Utakuwa unaishi kwa mtogole basi wewe.

Hii hapa ya $1500

View attachment 1421956....
Unazungumzia oil service ya gari gani ya Toyota kwa hio 50,000 mfano mimi natumia surf ya 1994 3000CC oil inahitajika ni 7.5 Litres nanua Total 7400 TIR lita i.e 8 au 10 kidumu cha lita 5 ni 45,000 kuongezea 10,000 x 3 = 30,000,

ATF Castrol Dex II 68,000 lita 4 nikiongezea 3 x 12,000 = 36,000 oil na fuel filter za bei rahisi 15,000 x 2 = 30,000, labour charge 20,000 = 75,000 + 104,000 + 50,000 = 229,000
 
Hebu cheki Lexus Ls460 ya miaka 11 iliyopita ambayo iko kwny category 1 na hio series 7 uone kama utaikuta hata 1 ambayo bei yake ina-range kwny hizo $2500-3000,huwezi kupata kamwe.
TRA ndo wanaharibu mambo sana yani Camry na Lexus IS 250 wameweka CIF kubwa sana yani inabidi kitengo cha valuation wakifumue waweke watoto wa mjini sio unaweka mtu katoka Misungwi au Sengerema halafu unamwambia aifanyie valuation gari za luxury matokeo yake wote tunanunua Altezza na Crown tukibadili ni Subaru
 

Hahah mzee baba umeongea bonge la point aisee,pale TRA wangemuweka muhuni anayejua magari mjini hapa kungekua na magari ya kifahari/maana hatari sana.

Cheki picha hapo chini,hio ni porsche Cayenne ya 2005 CIF yake $4,478 huko be forward,ila jamaa wa TRA wao wakaikadiria CIF yake ni $10,015.

Matokeo yake sasa,gari unanunua kwa Tsh mil. 10 afu ushuru TRA wanataka almost Tsh.26mil.

Biashara kichaa hio mzee baba.

 
Bora umenielewa mkuu ukimaliza nenda kaicheki valuation ya VW Jetta ya 2009 ni 17,000,000 wakati CIF ya gari $2800-3500
 
Nazungumzia Engine oil service, kwenye gari ya altezza nimefanya oil change ya 40,000 synthetic oil hio bei ina inlcude na oil filter. Sasa kwa gari ya altezza inafanana na BMW 5 series, hebu niambie oil change kiasi gani mnachajiwa.

Umeweka hesabu za transmission fluid, transmission lako bovu kiasi kwamba everytime ukifanya engine oil service inakulazimu ufanye na transmission fluid? Transmission fluid sio kitu cha kubadilishwa badilishwa kila unapofanya engine service.

Nna gari ambayo tangu ishuke nchini ni 5 years na hii ni gari ya mwaka 2000, sijawahi kubadilisha transmission fluid tangu ishuke, na sijawahi kupata tatizo lolote la transmission hadi leo, haijawahi kuguswa!
 
Gari nayoitumia mimi imefika Tanzania 2009 May, gari yenyewe manufactured ni 1994 ni kweli gearbox ilikua inasumbua ila hii hesabu ya transmission ni baada ya kuishusha chini na kuirekebisha lakini hata kama tukitoa hesabu ya transmission fluid bado oil na vitu vyengine kama filter etc.

Haipungui chini ya 120,000 labda sababu hii ninayotumia mimi ni SUV na unayotumia wewe ni sedan ila mpango wangu ni kununua hio Altezza nimeona maintenance yake ni ndogo sana sasa linganisha hapo ila pia nadhani kunatofauti kati ya service ya gari inayotumia Diesel na Petrol.
 

Sasa wewe unatumia SUV, mfano wake uwe SUV from German Brands, hapo ndio utaona tofauti. Put a cheap oil in a german brand you risk to damage the engine, which cant be said for Japanese cars.

Halafu Diesel cars maintainance cost zipo tofauti na petrol engines. Petrol engines ni cheap kuliko diesel.
 
'Nazungumzia Engine oil service, kwenye gari ya altezza nimefanya oil change ya 40,000 synthetic oil hio bei ina inlcude na oil filter.'

Hio oil ni lita ngapi unanunua na ni brand gani hio ya oil ambayo Synthetic inauzwa kwa pesa hio mkuu?
 
Bora umenielewa mkuu ukimaliza nenda kaicheki valuation ya VW Jetta ya 2009 ni 17,000,000 wakati CIF ya gari $2800-3500
Aisee hapo uwezekano wa kuishia kuziona tu kwa macho ni mkubwa aisee.
 
40,000/- synthetic engine oil pamoja na oil filter kwenye Altezza.....[emoji848][emoji848][emoji848]
Hatari sana....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee synthetic oil gani 40,000? Castrol 5w30 synthetic 5L ni zaidi ya laki
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…