Mazingaombwe (Jugglery) ni Sayansi au Uchawi?


Mazingaombwe ni moja kati ya aina za UCHAWI.Uchawi huu unahusisha zaidi katika KUHADAA UONI.Yaani kitu kilekile lakini kuna 'maarifa' yanafanyika ili kuyahadaa macho kukiona kitu kile katika HALI/SURA/MUONEKANO mwingine.Kwa mfano karatasi inaweza kufanyiwa 'utundu' na kuonekana ni pesa.
Na uchawi ni moja ya shughuli za SHETANI/IBILISI.Kaa mbali kabisa na haya mambo.Na wote wenye kushiriki kwenye masuala haya,wajue kabisa tayari wamekwishapanda treni ya ibilisi inayoelekea motoni.
 

Mazingaombwe ni UCHAWI mkuu.NI uchawi wa KUHADAA UONI,yaani kitu kilekile unachokiona yanafanyika maarifa kuwa kukiona katika muonekano mwingine.Na kwa kiasi kikubwa shughuli za kichawi zinatiwa nguvu sana MASHETANI YA KIJINI.Hawa wana uwezo wa kujibadilisha umbo lolote.
 

Mkuu unaweza kunipa tofauti kati ya uchawi na maarifa?
 

Tofauti ya miujiza, uchawi, na maarifa tafadhali!
 
Mbona kuna video series ya biggest secrets finally revealed aka 'breaking the magician code' inaonyesha uongo/tricks za wana mazingaombwe waziwazi
 
Wengi wanasema mazingaombwe ni uchawi, sasa je uchawi ni nini? Maana wengine tunasikia tu uchawi hatuelewi maana yake kiundani, hivyo ingekuwa vyema mwenye uelewa na ujuzi zaidi akaeleza nini maana ya uchawi, halafu afafanue mazingaombwe na kiini macho ni nini Ili tuelewe zaidi

..
 
Jaribu kufanya meditation ikianza kukolea hata kupaa inawezekana,
We human beings tumezaliwa na nguvu aina tofauti tofauti ila zinapotea kutokana na kutotumika kwa kadri miaka inavyosonga

hebu tuambie ww toka umeanza hiyo meditation unapaa angani live
 

upo sawa mkuu... maana hadi leo huwa najiuliza hivi uchawi maana yake ni nini?
yesu akitembea juu ya maji inaonekana ni miujiza ya Mungu lakini chriss angel au chief mwanamalundi akitembea juu ya maji ni mchawi... wachungaji na masheikh wakifanya miujiza ya kuponya watu kama ukimwi,saratani n.k ni nguvu za Mungu lakini akifanya mtu ambaye hajiusishi na hizi imani za dini mbili ni mchawi...
Swali langu ni kuwa, kwanini wengine wakifanya miujiza huonekana ni wachawi wakati wengine huonekana nguvu za mungu japokuwa nguvu zinazotumika hazionekani?
 

Watakwambia unakufuru kwa hili swali lako mkuu 😀
 

Mkuu una nondo za hatariii
 
Tatizo hakuna alieleta practical zana za utendaji kazi mpaka kuitua mazingaombwe,wengi ziori zimejaa.
 
Habari za sikukukuu
Ningpnda kupewa ufafanuz juu ya hawa wanamzingaombwe au magician jinsi wanavyocheza na akil za watu hii inatokana na mambo wanayoyafnya ambyo mengi yanakuwa yapo nje ya uwezo wa binadamu mfano kufanya.makaratsi kuwa hela kujikata na kisha kujiunga n mengine
Hapo ningepnda kupata ufafanuz kuna hawa wa kwetu na wale wa nje wazungu kwan nafikiri wanatofautiana kwa nje kuna mtu kma criss angel huyu jamaa anatembea mpka juu ya maji ana uwezo wa kutoa kitu nje kikiwa ndan ya Tv nashindw kuelewa anafanya kitu gani?
 
Mazingaombwe bado yako sema siku hizi sio Deal kwenda kufanya hiyo Michezo Shuleni, wadau wamegundua unapiga hela ndefu ukienda maeneo yafuatayo;

(a) Kuna mazingaombwe kwenye nyumba za Ibada.
(b) Kuna Mazingaombwe kwenye Vyama vya Siasa.
(c) Kuna Maziongaombwe kwenye Tiba Mbadala
(d) Kuna Mazingaombwe hadi kwenye mahusiano ya Mapenzi
(e) Kuna Mazingaombwe ya Kubadilisha Dola au Shilling kuwa nyingi.
(f) Kuna Mazingaombwe ya Madini Feki.


Chaguo ni lako unataka aina gani ya Mazingaombwe
 
Ngoja nimpigie lowassa anieleze mbinu anazotumia.wait nakupa majibu
 
Mazingaombwe na uchawi havitenganishwi, ila wafanya mazingaombwe hutumia ujanja huo kama michezo ya kuigiza, lakini wafanya mazingaombwe hao hao ambao hutumia michezo ya mazingaombwe kwa nia mbaya ya kudhuru na kwa siri ndio wachawi. Hakuna siri ya uchawi zaidi ya huo ujanjaujanja wa kimazingaombwe. Ndio maana inaelezwa watu kugeuzwa mizuka, kuonyesha mtu kafa na kisha mnamzika kumbe mwaziko dubwasa fulani wakati mhusika kageuzwa mzuka na kufichwa mahala. Tumeshuhudia matukio kadhaa waliokufa na kuzikwa wakaonekana hai na baada ya fahamu kuwarudia wameendelea kuishi na familia zao. Mazingaombwe na uchawi havitenganishwi, ila mfanya mazingaombwe anatofautiana na mtumia mazingaombwe kwa kudhuru mtu badala ya maigizo.
 
Sasa mkuu, mechanism ya mazingaombwe ipoje...? Huo ujanjaujanja ndio unafanywaje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…