Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilikua naangalia kipindi cha The Carbonaro Effect on truTV. Kipindi hiki kinahusu sanaa ya kiini macho au mazingaombwe ukipenda. Kwenye kipidi muigizaji anafanya "miujiza" tofauti tofauti, mara abadilishe unga kuwa bia, rangi za nguo huku kazivaa, gari kuwa kiti n.k.
Pindi niko shule ya msingi nilishuhudia hii sanaa kwa macho japo sikumbuki vizuri, leo ilishika kidogo akili yangu na kujiuliza mazingaombwe ni nini hasa!? Ni uchawi? Ni uwezo tu wa ajabu ndani ya baadhi ya watu? Na kidini inachukuliwaje hii sanaa?
Kwa upande mwingine, mimi ni mgumu sana kuamini uwepo wa uchawi kama siamini kabisa.
Nitoeni tongotongo hapo wadau..
Nimekua nikishuhudia wana mazingaombwe maarufu Duniani kama DYNAMO (Magician impossible) na TROY jinsi wanavyofanya Mazingaombwe mfano kuingiza smart phone kubwa kwenye chupa na Ikawa ndogo.
au kusoma mawazo yako na kukuambia ulichokiwaza katika fikra zako. ama kupoteza pete pete ikakutwa kwenye dafu baada ya kulipasua,,kutembea kwenye maji, nk.
![]()
![]()
![]()
![]()
Dynamo
Ni rahisi kumuuliza mtu Kile ulichoona kwenye Michezo ya Mazingaombwe akakujibu SI KWELI BALI kile Ni KIINI MACHO Tu..
Q; NiNI maana ya KIINI Macho? Na nini maana ya UChawi?
![]()
Troy
Je hakuna Uhusiano wowote wa MAzingaombwe na UCHAwi. wakina Pasco na wachangiaji wengine ningeomba maoni yenu????
Mazingaombwe ni moja kati ya aina za UCHAWI.Uchawi huu unahusisha zaidi katika KUHADAA UONI.Yaani kitu kilekile lakini kuna 'maarifa' yanafanyika ili kuyahadaa macho kukiona kitu kile katika HALI/SURA/MUONEKANO mwingine.Kwa mfano karatasi inaweza kufanyiwa 'utundu' na kuonekana ni pesa.
Na uchawi ni moja ya shughuli za SHETANI/IBILISI.Kaa mbali kabisa na haya mambo.Na wote wenye kushiriki kwenye masuala haya,wajue kabisa tayari wamekwishapanda treni ya ibilisi inayoelekea motoni.
Mazingaombwe ni UCHAWI mkuu.NI uchawi wa KUHADAA UONI,yaani kitu kilekile unachokiona yanafanyika maarifa kuwa kukiona katika muonekano mwingine.Na kwa kiasi kikubwa shughuli za kichawi zinatiwa nguvu sana MASHETANI YA KIJINI.Hawa wana uwezo wa kujibadilisha umbo lolote.
Jaribu kufanya meditation ikianza kukolea hata kupaa inawezekana,
We human beings tumezaliwa na nguvu aina tofauti tofauti ila zinapotea kutokana na kutotumika kwa kadri miaka inavyosonga
Wengi wanasema mazingaombwe ni uchawi, sasa je uchawi ni nini? Maana wengine tunasikia tu uchawi hatuelewi maana yake kiundani, hivyo ingekuwa vyema mwenye uelewa na ujuzi zaidi akaeleza nini maana ya uchawi, halafu afafanue mazingaombwe na kiini macho ni nini Ili tuelewe zaidi
..
upo sawa mkuu... maana hadi leo huwa najiuliza hivi uchawi maana yake ni nini?
yesu akitembea juu ya maji inaonekana ni miujiza ya Mungu lakini chriss angel au chief mwanamalundi akitembea juu ya maji ni mchawi... wachungaji na masheikh wakifanya miujiza ya kuponya watu kama ukimwi,saratani n.k ni nguvu za Mungu lakini akifanya mtu ambaye hajiusishi na hizi imani za dini mbili ni mchawi...
Swali langu ni kuwa, kwanini wengine wakifanya miujiza huonekana ni wachawi wakati wengine huonekana nguvu za mungu japokuwa nguvu zinazotumika hazionekani?
upo sawa mkuu... maana hadi leo huwa najiuliza hivi uchawi maana yake ni nini?
yesu akitembea juu ya maji inaonekana ni miujiza ya Mungu lakini chriss angel au chief mwanamalundi akitembea juu ya maji ni mchawi... wachungaji na masheikh wakifanya miujiza ya kuponya watu kama ukimwi,saratani n.k ni nguvu za Mungu lakini akifanya mtu ambaye hajiusishi na hizi imani za dini mbili ni mchawi...
Swali langu ni kuwa, kwanini wengine wakifanya miujiza huonekana ni wachawi wakati wengine huonekana nguvu za mungu japokuwa nguvu zinazotumika hazionekani?
Sasa mkuu, mechanism ya mazingaombwe ipoje...? Huo ujanjaujanja ndio unafanywaje...Mazingaombwe na uchawi havitenganishwi, ila wafanya mazingaombwe hutumia ujanja huo kama michezo ya kuigiza, lakini wafanya mazingaombwe hao hao ambao hutumia michezo ya mazingaombwe kwa nia mbaya ya kudhuru na kwa siri ndio wachawi. Hakuna siri ya uchawi zaidi ya huo ujanjaujanja wa kimazingaombwe. Ndio maana inaelezwa watu kugeuzwa mizuka, kuonyesha mtu kafa na kisha mnamzika kumbe mwaziko dubwasa fulani wakati mhusika kageuzwa mzuka na kufichwa mahala. Tumeshuhudia matukio kadhaa waliokufa na kuzikwa wakaonekana hai na baada ya fahamu kuwarudia wameendelea kuishi na familia zao. Mazingaombwe na uchawi havitenganishwi, ila mfanya mazingaombwe anatofautiana na mtumia mazingaombwe kwa kudhuru mtu badala ya maigizo.