Mazingaombwe ni ujuzi gani?

Mazingaombwe ni ujuzi gani?

Kete 3 ni sawa na Karata 3 ni Utaperi...!

Mchezeshaji ndo anaamua ule wakati Gani, wakati Gani uliwe.

Mazingaombwe ni Uchawi/Majini.
 
Kete 3 ni sawa na Karata 3 ni Utaperi...!

Mchezeshaji ndo anaamua ule wakati Gani, wakati Gani uliwe.

Mazingaombwe ni Uchawi/Majini.
Maarifa ambayo huyaelewi usiyaite uchawi.

Uchawi maana yake kuna nguvu zisizo za kibinadamu (supernatural powers).

Mazingaombwe si uchawi.

Mazingaombwe ni maarifa ya kibinadamu ambayo wewe huyaelewi.

Hakuna uchawi.
 
Acha uvivu, nenda youtube tricks zote zipo zinaelezewa step by step!
 
Kuna jamaa tulisoma nae alikua akimeza ela inatokea mfukoni kwa mtu yoyote atakaemchagua...ikafika hatua walimu wakamtishia kumfukuza shule maana tulikua hatusomi ni mazingaombwe tu. uchawi upo.
Wewe umeshindwa kuelewa ni namna gani huyo jamaa anaweza kumeza hiyo hela, Halafu unasema ni uchawi.

Umejuaje ni uchawi na si maarifa ambayo wewe huyaelewi?
 
Hujanishawishi, Hivi umeshawahi kushuhudia Mwana-mazingaombwe live au unaangalia kwenye simu?

Siongelei tricks nyepesi unazozisemea wewe, Ila kama wewe ni wa kishua huwezi elewa pia.
1. Nimehudhuria mara nyingi sana maonesho live ya mazingaombwe nilipokuwa Shule ya msingi. Nikawa interested na ninashangaa sana. inakuwaje mchanga unageuka sukari, magazeti yanakuwa noti (fedha) mpya moto unawaka bila kiberiti n.k.
2. Nilijiunga kwenye Tuition ya kujifunza mazingaombwe (Privately) na sikumaliza vipindi baada ya kugundua kwamba iko siku watazamaji wangu waliolipa pesa yao watanigundua kwenye hiyo janja-janja na kuficha-ficha kwangu (hideout) na kwa hasira wataweza kuniadhibu vikali kwa kunibonda/kipigo na kujirudishia hela yao huku wakikuachia jeraha. Nika-Mute
Vipo vitabu unaweza kujisomea mwenyewe library, unaanza na simple tricks then complicated tricks. Utahitaji pia ujinunulie vifaa na mavazi yatakayokuwezesha "kudanganya/kuficha mambo yako" e.g. unahitaji kitambaa cheupe, nyuzi zile za hariri (silk)nyembamba sana, mashuka ya rangi moja, mabox n.k.
 
Maarifa ambayo huyaelewi usiyaite uchawi.

Uchawi maana yake kuna nguvu zisizo za kibinadamu (supernatural powers).

Mazingaombwe si uchawi.

Mazingaombwe ni maarifa ya kibinadamu ambayo wewe huyaelewi.

Hakuna uchawi.
Kazi inaendelea!!!
 
Basi tuachane na hilo la kuchanganya mikono kwa haraka.

Tuongelee hii ya Mwana-mazingaombwe kukata ndizi kwa distance ya mita 3, Yani assume wewe ni Mwana-mazingaombwe mkononi umeshikilia kisu na Mimi nipo distance ya mita 3 kutoka kwako lakini unafanikiwa kukata ndizi nilioshikilia mkononi. Je, hichi kitendo kinatokeaje? Hii nilishuhudia LIVE sijahadithiwa wala kuangalia YOUTUBE.
Mkuu; mbona unakubali ununuliwe kwa bei rahisi hivo? Hizo ndizi nani kazileta hapo? Je, ulizikagua vizuri kabla ya tendo la kukata? Zilikuwa ndizi mbivu au mbichi zile za kumenya? Hayo na maswali mengine yataweza kukupa mwanga wa nini kiliendelea.
 
Magic na Witchcraft ni maneno tu hayaondoi ukweli kuwa Mazingaombwe ni sanaa ya kushangaza sana.

Basi nimekubali ni magic. Je, hii magic inafanyikaje mpaka ipumbaze akili ya binadamu!!! Inashangaza.
Zile ni tricks tu ukizijua utashangaa ulidanganywaje,ingia you tube andika breaking magician codes
 
Zile ni tricks tu ukizijua utashangaa ulidanganywaje,ingia you tube andika breaking magician codes
Achana na vya YouTube, Naongelea Mazingaombwe kweli kweli, Au ile ya kuvuta pikipiki nayo kuna code wanafanya . Wakati kwa macho unashuhudia Mkulungwa akivuta pikipiki kwa shingo. C'mon man kuwa serious kidogo.

By the way ushawahi kushuhudia mazingaombwe live Zaidi ya hayo huko YouTube?
 
Wakati niko shule ya msingi Nyakabungo mwanza alikuja mwana mazingaombwe mmoja,kwa macho yangu nilishuhudia mfuko mtupu ambao ulikung'utwa na nilijiridhisha haukuwa na kitu chochote ndani jamaa yule aliuwekea makaratasi tupu ambayo niliyachana kutoka kwenye daftari langu ambalo nilikuwa sijaliandikia chochote na mara baada ya kumwaga chini makarasi yale zilitoka blue blue tupu yaani noti za elfu kumi elfu kumi maana kipindi kile zilikuwa za blue.Mpaka leo huwa najiuliza maswali kama kaweza kufanya uchawi wa kugeuza karatasi kuwa pesa ameshindwa nini kutoa nyingi za kutosha ili azitumie mwenyewe na badala yake alituchangisha wanafunzi shiling hamsini hamsini za kutazama onesho lake!!???

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
Mkuu; hongera sana. Kumbe ww ni school mate wangu! Mimi nilisoma S/M Mirongo.
Sasa kwa akili ya kawaida utaweza kujiuliza; Hizo hela mbona hazigawiwi kwa audience ila anazichukua tena mwenyewe? Halafu kwanini kwanza ayaweke hayo makaratasi kwanza ndani ya mfuko tena mfuko wa kwake?(Kwa nini sio openly) ili muone yanavyogeuka taratibu kuwa fedha? Laiti angetokea mmoja wenu akazinyakua halafu mngeona jinsi ambavyo angemkimbiza mwizi wake. (hahahaaa)
 
N
Mkuu; mbona unakubali ununuliwe kwa bei rahisi hivo? Hizo ndizi nani kazileta hapo? Je, ulizikagua vizuri kabla ya tendo la kukata? Zilikuwa ndizi mbivu au mbichi zile za kumenya? Hayo na maswali mengine yataweza kukupa mwanga wa nini kiliendelea.
Ndo ubaya wa kumwelewesha mtu ambaye anaangalia Mazingaombwe youTube.

Hiyo ndizi ilishikwa na Mwanafunzi na ilikuwa nzima kabisa.

Kuna baadhi ya Mazingaombwe kweli ni tricks ila mengine yamevuka ukomo.
 
Back
Top Bottom