seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,655
Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga leo atamaliza safari yake duniani kwa kuzikwa kijijini kwake Tosamaganga. Viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiongozwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu watamsindikiza katika safari yake hii ya mwisho.
Aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mahiga amezikwa leo kijijini kwake Tosamaganga mkoani Iringa.
Serikali iliwakilishwa na makamu wa Rais mama Samia Suluhu ambaye aliuelezea wasifu wa Balozi.
Bunge liliwakilishwa na Naibu Spika Dr Tulia Ackson ambaye baada ya kumuelezea Dr Mahiga alisema amekuja na rambirambi za wabunge lakini watazikabidhi kwa mke wa marehemu pindi atakaporejea kutoka Nairobi Kenya anakouguza mtoto.
Hata hivyo mwisho wa shughuli za mazishi Waziri wa Ardhi mh Lukuvi aliagiza DC Kasesela wa Iringa Mjini akabidhiwe michango yote ya rambirambi hadi aitunze hadi atakapopewa maelekezo rasmi na familia.
KIFO: TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia - JamiiForums