Mazishi ya Dkt. Augustine Philip Mahiga kijijini kwake Tosamaganga mkoani Iringa. Mkewe ashindwa kuhudhuria baada ya kuwa Kenya akiuguza mtoto

Mazishi ya Dkt. Augustine Philip Mahiga kijijini kwake Tosamaganga mkoani Iringa. Mkewe ashindwa kuhudhuria baada ya kuwa Kenya akiuguza mtoto

Sasa kwanini yule mkuu wa wilaya Mtwara walimzika kwa namna ile?

Nani aliyetoa yale maelekezo?

Mbona nae kwa cheo chake alistahili heshima kama siku hizi kuzika mwili wa mtu tunaangalia "status" yake kwenye jamii kwanza, that was not fair.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini huyo alikuwa na nyadhifa kubwa,,halafu Ni kada wetu yule ujue...
Hahaha @Elunga. Najua ila kwa UTARATIBU si kuzikwa na serikali na watu wasiozidi 10? Huo mwili umeandaliwaje kitaalam usilete madhara kwa hao makasisi? Hawatafukiza ubani na kurusha maji ya Baraka jirani na jeneza? Wabebaji jeneza ni kina nani? Haya bwana.
Rest in Peace Jasusi Mbobevu.
 
Members,Hivi kuna ugumu gani wakaamua kufunga haya makanisa

Leo wameaga mwili ukiwa haujafunuliwa ndani ya sanduku,kwanini msiruhusu na wanyonge wakaaga ndugu zao

Watawala wanaruhusiwa kuaga ndugu zao bila kufungua sanduku ila wanyonge wao wanalalamika kuwa hawapewi muda wa kuaga ndugu zao

Picha mapadri wakisoma misa ya kuaga mwili wa Augustine Mahiga Iringa

Ingekuwa ni wanyonge usitegemee misa kama hii

Ukiondoa mawaziri,Majaji na wabunge wengine wote mnaitwa wanyonge

Wakuu wa wilaya na Mikoa wote ni kundi la wanyonge kumbuka yule mkuu wa mtwara View attachment 1437426


Tuko ktk vita na Virus vya Corona, acha siasa za majitaka, unajua vita au sbb unaweza kuandika humu unatoa useless idea
 
Sasa kwanini yule mkuu wa wilaya Mtwara walimzika kwa namna ile?

Nani aliyetoa yale maelekezo?

Mbona nae kwa cheo chake alistahili heshima kama siku hizi kuzika mwili wa mtu tunaangalia status yake kwenye jamii kwanza, that was not fair.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haswa umenena kiongozi. Barikiwa mno. Maana alizikwa na serikali na wakivalia rasmi kwa shughuli Ile. Sijajua kama hata ibada ya misa ilifanyika.
 
Hao watu toka wakiwa hai maisha yao hayana usawa na sisi, sasa ajabu wakati wa kufa ndio tuone tuna haki sawa.
 
Tuko ktk vita na Virus vya Corona, acha siasa za majitaka, unajua vita au sbb unaweza kuandika humu unatoa useless idea
Corona sio vita ni ugonjwa unaohitaji tafiti na tiba
Nyie mazwazwa muwe mnachuja mambo ,kila unaloambiwa wewe wanapiga matarumbeta tupo kwenye vita vya corona

Tumia akili soma Fasihi ya mwandishi anamaanisha kitu gani

Povu jingi huelewi kilichoandikwa
 
Una tatzo lakuchambua Mambo ungesoma kwa makini sidhan Kama ungeandika ujinga huu, hujaelewa alichomaanisha mwandishi!! Jifunze kusoma mara kadhaa acha kuendeshwa na mihemko
Ameandika nini cha maana ambacho sijakielewa.Zaidi upuuzi tu. Kwani watu wengine wanaofiwa sasa hivi hawaruhusiwi kuzika ndugu zao na kuzingatia kujilinda na hili janga. Acha ubwege wa kukariri.
 
Mambo ya hovyohovyo tuuhh...
 
Aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mahiga amezikwa leo kijijini kwake Tosamaganga mkoani Iringa.

Serikali iliwakilishwa na makamu wa Rais mama Samia Suluhu ambaye aliuelezea wasifu wa Balozi.

Bunge liliwakilishwa na Naibu Spika Dr Tulia Ackson ambaye baada ya kumuelezea Dr Mahiga alisema amekuja na rambirambi za wabunge lakini watazikabidhi kwa mke wa marehemu pindi atakaporejea kutoka Nairobi Kenya anakouguza mtoto.

Hata hivyo mwisho wa shughuli za mazishi Waziri wa Ardhi mh Lukuvi aliagiza DC Kasesela wa Iringa Mjini akabidhiwe michango yote ya rambirambi hadi aitunze hadi atakapopewa maelekezo rasmi na familia.

Chanzo: ITV!
 
Back
Top Bottom