luckyline
JF-Expert Member
- Aug 29, 2014
- 15,160
- 21,676
Kweli mbona ni maumivu makubwa? Jamani dahJamani msilolijua nyamazeni. Mama Mahiga mwanawe ni mgonjwa sana, kitu kilichopelekea mama kuitwa aende kumuuguza. Alipofika Nairobi kuna karantini ya siku 14! Bado hajamaliza hata hiyo karantini mumewe anafariki ghafla, mwanawe yuko taabani. Ombeni yasiwakute. Huyu mama anapitia kipindi kigumu sana. Watoto wake wengine wawili (wa ndoa) mmoja yuko Switzerland mwingine yuko Marekani! Hamuujui uchungu wake, nyamazeni muombe Mungu Awaepushe yasije kuwapata hayo!
Sent using Jamii Forums mobile app